Friday 27 February 2015

Tibaijuka abishana dakika 415, Chenge aenda Mahakama Kuu

Wakati Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka jana alitumia dakika 415 (takribani saa 7) akibishana katika mpambano mkali wa kisheria kuhusika kwake katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge aliamua kutimkia Mahakama Kuu kukwepa kuhojiwa na Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Jana, mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Hamisi Msumi alitoa uamuzi kuhusu pingamizi la Chenge aliyetaka baraza hilo lisisikilize shtaka lake la kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
Hata hivyo, Chenge alikwamisha kwa mara ya pili baada ya kuomba kwenda Mahakama Kuu kutafuta tafsiri iwapo baraza hilo linaweza kusikiliza shauri lake kinyume na amri ya mahakama iliyoagiza lisijadilie na taasisi kwa kuwa kuna kesi kadhaa mahakamani zinazohusiana nalo.
Profesa Tibaijuka na Chenge kila mmoja aliingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye akaunti zao binafsi kutoka kwa mkurugenzi wa VIP Engineering iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa za kampuni ya Independent Power Solution Limited (IPTL).
Baraza hilo, linasikiliza mashauri hayo kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 katika vipengele vya matumizi mabaya ya madaraka na sakata la escrow.
Chenge, juzi katika baraza hilo alipoitwa kuhojiwa aliibua hoja ya zuio la Mahakama Kuu na baada ya mabishano ya kisheria, Jaji Msumi alisema angekwenda kuisoma amri huyo kisha kutoa uamuzi wake jana.
Akisoma uamuzi huo, Jaji Msumi alisema: “Mlalamikiwa ametoa hoja ya amri ya Mahakama Kuu kuwa ndiyo hiki kinachojadiliwa, chimbuko lake ni miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo chimbuko lake ni bungeni na mahakama ilizuia lakini amri hiyo haizuii mamlaka hii.”
“Orodha ya taasisi zilizotajwa hailihusu baraza hili, wadaiwa wote pamoja na mawakala, watumishi, wasaidizi wao au watu wengine wanaofanya hili. Amri iliyoandikwa, Baraza si mlengwa wa hili. Kinachozuiwa kufanywa ni kupelekwa bungeni au kujadiliwa taarifa ya (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na umiliki wa IPTL,” alisema.
Akihitimisha kusoma uamuzi wa baraza hilo, Jaji Msumi alisema: “Hoja iliyotolewa na mlalamikiwa haina msingi na tunaomba kuendelea kulisikiliza.”
Mara baada ya kumaliza, Chenge aliyekuwa amevalia shati la kitenge na suruali nyeusi akiwa haonyeshi kuwa na wasiwasi alisema: “Nashukuru kwa uamuzi huo lakini sina nia ya kubishana, natoa hoja ya kukata rufaa ya kwenda Mahakama Kuu ili mahakama itafasiri kama Baraza lina mamlaka ya kujadili suala hili.”
Chenge ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema: “Kama wanasheria wa sekretarieti wangejituma kidogo kwenda masijala ya Mahakama Kuu kupitia wangeliona hili. Amri hii ya zuio ni pana kuliko uamuzi wa Baraza lako uliofikia, naomba nitumie nafasi hii kwenda Mahakama Kuu.”
Akihitimisha hoja hiyo, Jaji Msumi alisema: “Nakuruhusu, niongeze tu sina hakika kama kanuni zimetengenezwa kuruhusu rufaa na kama hazipo kutakuwa na utaratibu. Ukipeleka itasaidia kujenga Baraza lakini Mahakama Kuu ina haki, kila mtu ana haki kwa suala lolote, mimi siwezi kukuzuia.”
Mara baada ya uamuzi huo, Chenge akiwa anatoka ukumbini waandishi wa habari walianza kumpiga picha huku wengine wakimtaka kuzungumzia uamuzi wake wa kupeleka suala hilo Mahakama Kuu, lakini yeye alisema: “Nani anataka nimpeleke tuisheni,” kauli iliyowafanya waandishi hao kucheka.
Profesa Tibaijuka
Shauri la Profesa Tibaijuka lililoanza kusikilizwa saa 3:16 asubuhi hadi saa 5:18 asubuhi kabla ya kuahirishwa na kurejea tena saa 6.30 mchana hadi lilipohitimishwa saa 11.23 jioni, lilivuta hisia za wananchi na watumishi mbalimbali wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansso wakiongozwa na Mkuu wa Shule hiyo, Halima Kamote.
Mashtaka
Akisoma hati ya malalamiko dhidi ya mbunge huyo wa Muleba Kusini, mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili, Wemaeli Wilfred alisema: “Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka kwa kutumia wadhifa wake (waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi) alishawishi na kuomba na kupokea fedha Sh1.617 bilioni kutoka kwa James Rugemalira.
Mara baada ya kumaliza kusoma hati hiyo, Wakili wa Profesa Tibaijuka, Rugemeleza Nshala alisimama na kusema: “Tunayakataa yote.”
Kutokana na kauli hiyo, Jaji Msumi aliingilia kati na kusema: “Hii siyo mahakama ya kisheria, taratibu zetu siyo za kimahakama, hivyo ni vizuri kuyafikiria hayo.”
Ushahidi
Baada ya kauli hiyo shahidi wa Sekretarieti, Waziri Kipacha ambaye pia ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa ya Sekretarieti alisimama na kuanza kutoa ushahidi wake akiongozwa na Wilfred.
Shahidi huyo alisema alichokifanya Profesa Tibaijuka (kuomba na kupokea fedha hizo) wakati huo akiwa waziri, ni kinyume na sheria za maadili ya vingozi wa umma.
“Kuna tatizo, kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba maslahi ya kiuchumi kutoka kwa mtu yeyote, mheshimiwa Tibaijuka Februari 12 mwaka 2014 alipokea fedha kutoka VIP Sh1.617 bilioni...hapa kuna tatizo la kimaadili.”
Kipacha aliendelea kulieleza baraza hilo kuwa: “Kiongozi wa umma haruhusiwi kupokea maslahi ya kiuchumi lakini mheshimiwa Tibaijuka alifanya hivyo akijua kuwa ni makosa kutokana na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

“Profesa Tibaijuka kupokea kiasi kikubwa cha fedha kama hicho na wadhifa aliokuwa nao wa uwaziri ni ukiukwaji wa sheria za viongozi wa umma mheshimiwa mwenyekiti. Viongozi wa umma wanapaswa kuzingatia maadili wanapokuwa na uhusiano na kampuni au taasisi binafsi.”
Baada ya maelezo hayo, Wakili Nshala alimuuliza Kipacha kuwa ni kosa gani alilolifanya kupokea mchango wa shule kama alivyokwishaeleza?
Kipacha alijibu: “Hapa ni ukiukwaji wa sheria ya maadili, Profesa Tibaijuka alipokea mchango ambao ni kiasi kikubwa cha fedha tena kwa kupitia akaunti yake binafsi, jambo ambalo ni kinyume kabisa cha sheria hii.”
Nshala aliuliza tena: “Je, kama kiongozi wa nchi yetu ana jukumu la kuhamasisha na kusaidia watoto wetu kupata elimu, sasa hapa Profesa Tibaijuka kosa lake ni lipi?
Kipacha alijibu: “Kama kusaidia kwa kutoa fedha zake mfukoni siyo kosa na kama unachangisha au kuhamasisha watu kuchangia elimu na fedha hizo zinakwenda moja kwa moja kwa walengwa siyo kosa, lakini fedha hizo zikiingia moja kwa moja kwako hapo ni makosa kwa mujibu wa sheria hii ya maadili ya viongozi wa umma.”
Nshala aliendelea kumuuliza, “Baada ya kufuatilia ninyi kwa uchunguzi wenu baada ya yeye (Profesa Tibaijuka) kuingiziwa fedha mlibaini nini?”
Kipacha kwa upole na kujiamini wakati wote alijibu: “Tulibaini fedha hizo zilianza kutoka kwa mafungu. Februari 18, 2014 zilitoka Sh1 bilioni kwenda Bank M na Machi 12, 2014 zilitoka Sh500 milioni kwenda Bank M na kubakiwa na Sh117 milioni katika akaunti yake ambayo hatujui alizifanyia nini. Lakini mwenyekiti hapa lalamiko ni ukiukwaji wa maadili tu.”
Nshala aliuliza tena: “Kwa nini katika uchunguzi wenu hamkwenda kuwahoji Bank M au bodi ya wadhamini wa shule kwa kuwa ndiko fedha zilikwenda na iwapo wao walitoa uamuzi huo?
Kipacha alisema: “Kwa mujibu wa sheria hii sisi hatukuona sababu ya kwenda kuwahoji wao.”
Baada ya kauli hiyo, Jaji Msumi aliingilia kati na kusema: “Katika uchunguzi wenu kwa nini hamkwenda kuhoji zaidi wakati mnasema kuna taasisi imenufaika kwa nini hamkwenda huko?
Akijibu hoja hiyo, Kipacha alisisitiza kuwa hawakuona sababu ya kufanya hivyo.
Sh10 milioni za mboga 

Hoja iliyoibua vicheko barazani ni kauli ya Profesa Tibaijuka kuwa kati ya fedha hizo alichota kwanza Sh10 milioni za kununua mboga.
Akitoa utetezi wake ambao mara zote ulikuwa ukiwafanya watu waliojaa ukumbini humo kuangua vicheko, Profesa Tibaijuka akihojiwa na mwanasheria wa sekretarieti hiyo, Getiruda Cyriacus aliyetaka kujua kama fedha hizo ziliingia Februari 12, 2014 kwa nini zilitoka Februari 18, mwaka huo na wakati huo huo kuna kiasi cha Sh10 milioni kilitoka mapema?
Profesa Tibaijuka alisema: “Nilitoa kiasi hicho kwenda kununua mboga, kwani kuna kosa gani.”
Akiendelea, Profesa Tibaijuka alisema: “Uongozi mzima wa shule ya Babro wanafanya kazi kwa uadilifu, uwazi na ukweli wa hali ya juu na mimi kuomba mchango wa kuwasaidia watoto wa kike waliokuwa hawana fursa ya kupata elimu bora sioni kosa lake.
“Harakati hizi zitaendelea kwani nimekuwa nikizifanya nje na ndani ya nchi na ndiyo maana Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitupa kiwanja cha shule hiyo inayopigiwa kelele na yeye alishachangia fedha na watu wengine wakiwamo wafadhili wakubwa, mfano Serikali ya Sweden iliyochangia zaidi ya Sh8 bilioni lakini leo hii Sh1.6 inanidhalilisha hapa.”
Aliongeza: “Mimi ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa nina mafao yangu napata na nina akaunti za benki kama 10 ndani na nje ya nchi, sasa hii ya Rugemalira kama ningetaka angeiingizia katika akaunti nyingine, lakini yeye alisema ili asaidie shule nifungue akaunti Benki ya Mkombozi, sasa ningefanyaje?
Profesa Tibaijuka aliongeza, “Leo hii nadhalilishwa na kusimamishwa hapa kwa harakati zangu za kumkomboa mtoto wa kike, niwahakikishie kuwa nitaendeleza harakati hizi na malengo yangu ni kuhakikisha kila kanda kunakuwa na shule hizi za mfano, tulianza na Dar es Salaam, Bukoba sasa tunatafuta kiwanja Mwanza na Mbeya.”
Mbunge huyo aliambatana na mashahidi wake wawili, Balozi Paul Rupia ambaye ni mlezi wa Bodi ya Wadhamini wa shule hiyo na mwenyekiti wa bodi hiyo, Simon Odunga ambao wote kwa pamoja walisema fedha walizopokea kutoka kwa Rugemalira kupitia akaunti ya Profesa Tibaijuka zilitumika kulipa deni la Sh2 bilioni walilokuwa wakidaiwa na Bank M, ambalo hata hivyo halikumalizika.
Baada ya utetezi huo, Jaji Msumi alizitaka pande zote ziandae majumuisho ambayo yatawasilishwa kabla ya Machi 13 mwaka huu, ili Baraza liandae mapendekezo ya siri yatakayopelekwa kwenye mamlaka za juu.

Yanga kujitupa uwanjani leo Kombe la shirikisho

Kikosi cha Yanga ya Tanzania
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Yanga Leo hii watajitupa uwanjani kuwakabili BDF XI huko Gaborone, Botswana.
Huu ni mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa awali Yanga walishinda magoli 2-0 mchezo ulifanyika Jijini Dar es Salaam Tanzania.
Jumamosi Timu nyingine mbili za Tanzania, Azam FC na KMKM, zitakuwa Viwanjani kwenye Mechi za raundi ya pili ya Klabu bingwa barani Afrika CAF
Wakati Polisi ya Zanzibar itacheza Mechi yake ya Pili ya raundi ya kwanza ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho hapo Jumapili.
Yanga na Azam FC, ambao wako Ugenini wanahitaji Sare ya aina yoyote au ushindi kuweza kusonga mbele kwa hatua inayofuata.

Mwanamume aliyejitolea kuuza ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Mwanamume mmoja amejitolea kutoa ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.
Sorin Gorgian Salinievcici mwenye umri wa miaka 24 amejitolea kuuza ubikira wake kwa pauni 1,476 baada ya kusoma kuhusu wanawake wanaofanya hivyo.
Alielezea kuwa :''mimi husoma kuhusu wasichana wanaofanya hivyo na nikafikiri kwamba iwapo wanafanya hivyo hata mimi naweza kufanya''.
Amesema kuwa mwanamke yeyote atakayenunua ubikira wake ni sharti awe mwenye heshima.
''Sisemi kuwa ni lazima awe mrembo lakini awe mwanamke wa kawaida, mzuri na mwaminifu''.alisema.
Katika bango aliloandika nyumbani kwake huko Romania,alisema kuwa inaweza kuwa zawadi nzuri katika maadhimisho ya siku hiyo ya wanawake mnamo mwezi machi tarehe 8.

Mchezaji wa Simba aitwa TP Mazembe

KAMA dili ikifanyika kwa haraka kabla msimu haujamalizika, Simba inaweza kuandika rekodi nyingine ya kuuza mchezaji kwenye timu kubwa zenye hadhi Afrika tena kwa fedha nyingi.
Kiungo wa Simba aliyeko kwa mkopo kwenye klabu ya Stand United ya Shinyanga, Haruna Chanongo ameitwa kwa majaribio kwenye klabu tajiri ya TP Mazembe na ataondoka nchini wiki ijayo.
Iwapo Chanongo atafuzu na kusaini Mazembe kabla ya msimu huu kumalizika Simba itaula, lakini kama akisaini baada ya msimu kumalizika itakuwa imekula kwa Mnyama kwa vile mkataba wake na mchezaji huyo utakuwa umemalizika na atakuwa huru.
Kuondoka kwa mchezaji huyo huenda kukaipa ahueni Yanga kwa vile atakosa mechi baina ya timu yake ya sasa ya Stand United dhidi ya Jangwani kwenye Uwanja wa Taifa wiki ijayo.
Mazembe ndiyo klabu wanayochezea Watanzania; Mbwana Samata (aliyetokea pia Simba) na Thomas Ulimwengu.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand, Muhibu Kanu alisema kuwa wataweza kumkosa Chanongo kwa kuwa amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe.
“Kwa sasa kocha wetu anamwandaa kwa ajili ya kufanya majaribio, hivyo amemwandalia programu ya peke yake nia ni kutaka kuona kijana anafuzu kwa kuwa hii ni sifa ya Tanzania nzima kama akiweza kusajiliwa na TP Mazembe,” alisema Kanu.
Alisema pia itakuwa ni pengo kubwa kwao kwani wana mechi mbili kubwa ya Kagera Sugar na Yanga huku tayari tiketi ya ndege ikitarajiwa kutumwa kwa ajili ya safari hiyo.
Meneja wa Chanongo ambaye ni Jamal Kisongo amekiri kuwa mchezaji huyo ataondoka nchini wiki ijayo kuifuata Mazembe huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
“Chanongo ataondoka wiki ijayo na hilo viongozi wa Stand wanalielewa ijapokuwa wamesikitishwa mchezaji huyo kuondoka wakati anahitajika sana katika timu hiyo, lakini kwa ajili ya maendeleo yake lazima akajaribu bahati yake,” alisema.
Meneja huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kukuza Soka kwa vijana kinachojulikana kwa jina la ‘Jaki’ kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam, alimtaka Chanongo kutumia vema nafasi hiyo ingawa ataenda kukutana na changamoto ya viungo waliopo Mazembe.
“TP Mazembe wana viungo vya ushindani wa hali ya juu, lakini Chanongo akifanya vizuri ana nafasi kubwa,” alisema.

Tottenham na Liverpool zafungasha virago Europa

Wachezaji wa Liverpool

Timu za Liverpool na Tottenham Hotspur za England jana zilifungasha virago rasmi kwenye mashindano ya ligi ya Europa baada ya kukubali vichapo kutoka kwa wapinzani wao.
Liverpool wakiwa ugenini walikwaana na Besiktas ya Uturuki na kuondolewa kwa mikwaju ya penalti 5 kwa 4 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya jumla ya goli moja kwa moja na hata baada ya kuongozewa dakika 30 hakupatina mshindi.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye alirudi tena England Demba Ba alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Besitkas waliofunga penalti.
Nayo Tottenham imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupata kichapo cha magoli 2 -0 kutoka kwa Fiorentina na hivyo kuondolewa kwa jumla ya magoli 3 - 1.
Wakati Tottenham na Liverpool zikiondolewa na kwenye michuano hiyo Everton yenyewe imesonga mbele katika hatua ya kumi na sita bora baada ya kuifunga BSC Young Boys ya Uswis kwa jumla magoli 3 -1.
Matokeo mengine Inter Milan ya Italia imesonga mbele baada ya kuifunga Celtic 1 - 0.
Zenit St Petersburg ya Urusi nayo imesonga mbele baada ya kuifunga PSV Eindhoven kwa magoli 3 kwa 0.
Matokeo ya mengine ya mechi za Europa ligi zilizochezwa haya hapa chini
Besiktas 1 - 0 Liverpool (agg 1 - 1)
Fiorentina 2 - 0 Tottenham (agg 3 - 1)
Inter Milan 1 - 0 Celtic (agg 4 - 3)
Everton 3 - 1 BSC Young Boys (agg 7 - 2)
Feyenoord 1 - 2 Roma (agg 2 - 3)
Dinamo Moscow 3 - 1 Anderlecht (agg 3 - 1)
Zenit St P 3 - 0 PSV
Borussia Mönchengladbach 2 - 3 Sevilla (agg 2 - 4)
Dynamo Kiev 3 - 1 Guingamp (agg 4 - 3)
FC Red Bull Salzburg 1 - 3 Villarreal (agg 2 - 5)
Legia Warsaw 0 - 3 Ajax (agg 0 - 4)
Ath Bilbao 2 - 3 Torino (agg 4 - 5)

Chid benzi ahukumiwa miaka miwili jela

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Siri Nzito zzaibuka kuhusu viungo vya albino

Kila kiungo kimoja cha ‘albino’, huuzwa kwa bei kubwa, hali inayotajwa kuwa kiini cha kukithiri kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, mahakama mkoani Geita ilielezwa jana.Ingawa bei ya viungo vya albino ilitajwa jana mahakamani, lakini hatuwezi kutaja thamani hiyo ili kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi.
Akitoa ushahidi katika kesi namba 43/2009 ya mauaji ya albino, Zawadi Magimbu, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru wilayani Geita, shahidi wa 12 ambaye ni polisi wa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam aliibua mambo lukuki ya ajabu yanayofanywa na wauaji wa albino.
Mambo hayo ni pamoja na thamani ya fedha wanazolipwa watu kwa kila kiungo kimoja cha albino kiasi cha (tunahifadhi)katika Kanda ya Ziwa, huku viungo hivyo pia vikitofautishwa ubora kwa kupimwa na redio, wembe na Sh1 ya zamani.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Masaru Kahindi, Ndahanya Lumola, Nassoro Charles na Singu Siantem. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 5 itakapotolewa hukumu.
Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Joacqiune Demello, shahidi huyo (jina linahifadhiwa), alidai upelelezi wa polisi ulibaini kuwa wakati wa mauaji ya mwaka 2008, watuhumiwa walikuwa wanashawishiwa kulipwa kiasi kikubwa kwa kila kiungo kimoja cha albino.
“Nilitoka Dar es Salaam kuja Mkoa wa Shinyanga kufanya upelelezi wa mauaji ya albino. Nikiwa Shinyanga, tulipata taarifa kutoka kwa msiri wetu aliyetueleza kuna watu wanafanya biashara ya viungo vya albino,” alidai shahidi huyo.
Alidai baada ya kupata taarifa hizo, waliamua kuweka mtego ili kuwakamata watu hao waliokuwa wakijishughulisha na biashara hiyo.
“Tulitafuta albino wawili kwa ajili ya mtego na kafanikiwa kuwakamata watu wawili, ambao ni Robert Magoma na Ndahanya Lumola waliokuwa wakijishughulisha na biashara hiyo,” alidai shahidi huyo.
“Katika uchunguzi wetu, tuligundua kuwa kuna mganga aliyetajwa kwa jina la Gerald Mazuri, mkazi wa Kijiji cha Kakoyoyo, Kata ya Ushirombo, Wilaya ya Bukombe kuwa anafanya biashara hiyo na Wazungu kutoka Wilaya ya Geita (hawakutajwa).
Alidai kuwa wembe, redio na shilingi hutumika kama vipimo vya kujua ubora wa viungo vya albino.
“Niliendelea kuwadadisi, wakasema walipeleka mifupa hiyo kwa Mganga wa Jadi, Mussa Ally wa mjini Katoro, mkoani Geita ikapimwa kwa kutumia wembe, redio inayozungumza na Sh1 ya zamani,” alidai shahidi huyo na anamnukuu mmoja wa washtakiwa:
“Ukichukua wembe ukauweka kwenye mfupa wa albino na kunasa, basi mfupa huo ni dili, kinyume chake hauna ubora. Pia, ukichukua Sh1 ukaiweka kwenye mfupa na kunasa, nao ni bora na redio inayozungumza ukiisogeza kwenye mfupa huo na kuzima, ujue kiungo hicho ni dili.”
Desemba 27 mwaka jana, mtoto Pendo Emmanuel (4), alitekwa na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Ndami, Wilaya ya Kwimba.
Februari 15, mwaka huu, mtoto Yohana Bahati (1), alitekwa kabla ya kuokotwa akiwa amekufa na miguu na mikono yake kukatwa.
Hivi karibuni, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, ilipiga marufuku waganga wa jadi kupiga ramli.

Tuesday 24 February 2015

Ccm yaburuzwa na Chadema


 Wafuasi wa Chadema wakishangilia katika Kata ya Chanji baada ya chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa uliofanyika juzi mjini Sumbawanga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeigaragaza vibaya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika juzi katika kata tatu za Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ambazo hazikufanya uchaguzi Desemba 14, mwaka jana.
Uchaguzi katika kata hizo uliahirishwa kutokana na kasoro mbalimbali jambo lililosababisha mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela kusimamishwa kazi.
Msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika katika kata za Msua, Chanji na Kizwite na mitaa mingine miwili iliyorudia uchaguzi, Hamid Njovu alisema Chadema ilinyakua jumla ya mitaa 37 kati ya 44 na kuiacha CCM ikiambulia mitaa mitano.
Matokeo hayo mapya yanaibuka sasa wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilishahitimisha kutangaza matokeo ya jumla ya mitaa katika uchaguzi huo ikisema ulikuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tamisemi, Kalist Luanda alisema Desemba 24, mwaka jana kuwa mitaa yote 3,875 nchini ilifanya uchaguzi na kukamilika kwa asilimia 100 huku CCM ikipata asilimia 66.66 baada ya kuzoa mitaa 2,583, ikifuatiwa na Chadema iliyopata mitaa 980 (asilimia 25.3), CUF mitaa 266 (asilimia 6.9), NCCR Mageuzi mitaa 28 (asilimia 0.7), TLP mtaa mmoja (asilimia 0.03), ACT mitaa 12 (asilimia 0.31), UDP mitaa mitatu  (asilimia 0.08), NRA mtaa mmoja (asilimia 0.03) na UMD mtaa mmoja (asilimia 0.03).
Matokeo mapya
Akitangaza matokeo hayo jana, Njovu alisema katika Kata ya Kizwite kati ya mitaa 15 iliyofanya uchaguzi Chadema ilishinda mitaa 13 dhidi ya CCM iliyoambulia mitaa miwili, Kata ya Msua mitaa yote 13 iliyofanya uchaguzi ilikwenda kwa Chadema na CCM kuambulia patupu.
Alisema kwa Kata ya Chanji ambayo ilikuwa na mitaa 14 iliyofanya uchaguzi, Chadema ilishinda mitaa 10 na CCM mitatu huku mtaa mmoja wa Nankasi kura ziligongana katika nafasi ya uenyekiti, hivyo kuamuliwa uchaguzi utarudiwa Jumapili.
Njovu alisema katika uchaguzi wa marudio uliofanyika kwenye mitaa miwili kila chama, CCM na Chadema, kiliibuka na ushindi katika mtaa mmoja ambao mtaa wa Bangwe Kata ya Izia ulichukuliwa na CCM na ule wa Tambazi katika Kata ya Sumbawanga ukaenda Chadema.
Uchaguzi huo uliofanyika kwa amani na utulivu tofauti na ilivyokuwa Desemba 14, mwaka jana ambapo ulivurugika katika kata hizo kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza ikiwa pamoja na vituo kuchelewa kufunguliwa.
Hali hiyo ilisababisha wananchi waliokaa vituo kwa zaidi ya saa nane wakisubiri kupiga kura kuhamaki na kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Kizwite na Chanji na kuteketeza nyaraka zote za kupigia kura, hivyo kufanya mchakato mzima wa uchaguzi huo kufanyika upya.
Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Rukwa, Zeno Nkoswe aliwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na kufanya Chadema kuibuka na ushindi wa kimbunga na kuwa huo ni mwanzo wa kuelekea ukombozi wa Taifa kutoka mikononi mwa CCM.

Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Rukwa, Clement Bakuli alisema wameyapokea matokeo hayo kwa masikitiko, lakini katika mpambano wowote lazima mshindi apatikane, hivyo chama kitakaa kufanya tathmini kuona wamekosea eneo gani ili waweze kujirekebisha katika uchaguzi ujao.
Pamoja na matokeo hayo, timu nzima ya CCM ngazi ya wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wake wa mkoa, Emmanuel Kilindu na Mbunge wa Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly walipiga kambi na kufanya kampeni za nguvu katika kata hizo lakini haikufua dafu.
Ushindi huo ni mwendelezo wa mafanikio ya Chadema ndani ya Ukawa katika uchaguzi huo Desemba 14 na kurudiwa Desemba 21 katika baadhi ya maeneo, yaliyoonyesha kuwa uungwaji mkono wa CCM katika maeneo ya mijini umeporomoka kwa kasi huku wa upinzani ukiimarika.
Katika uchaguzi huo, chama kipya cha ACT-Tanzania kilichomoza na kuviacha baadhi ya vyama vikongwe ambavyo havikupata hata nafasi ya ujumbe katika uchaguzi ulioelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kuwa ulikuwa umekamilika kwa asilimia 99.
Katika maeneo ya vijiji na vitongoji, CCM ilipata ushindi wa asilimia 79.81 (vijiji) na 79.83 katika vitongoji, wakati kwenye mitaa ambayo ipo sehemu za mijini kilishuka zaidi na kupata asilimia 66.66, ikilinganishwa na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 1999, ambapo chama hicho kilipata asilimia 89.2 katika mitaa, asilimia 91 katika vitongoji na asilimia 91.6 katika vijiji.

Roboti aingia darasani na kujifuza

Robot inayo msaidia Cole

Mwanafunzi mmoja katika mji wa Pennsylvania nchini Marekani alipata ajali ya gari na kuumia vibaya na sasa anahudhuria masomo kwa msaada wa njia ya roboti.
Cole Fritz alikuwa alikuwa hawezi kuhudhuria masomo yake mara baada ya ajali mwezi mmoja uliopita,lakini kwa sasa anaouwezo wa kufuatilia kila kinachoendelea kwa msaada wa roboti.
Pennsylvania ilikodisha kifaa hicho kutoka katika kampuni inayotoa mafunzo ya namna ya kutumia roboti hizo katika mitandao ya kijamii.Kimsingi kifaa hicho ni sawa na iPad ambayo imeinuliwa juu vya kutosha.Naye Cole huwa anakiendesha kifaa hicho kupitia kinakilishi chake na vitufe vya kubofyea kitu ambacho yeye anakielezea kuwa sawa na kifaa cha michezo ya kinakilishi ya runinga.ana sema Roboti hiyo inamsaidia kufuatilia masomo yake bila taabu yoyote na pia awapo shuleni anakutana na marafiki zake .
Ni vyema na furaha kubwa kuonana na kila mmoja niliye mzoea na kuzungumza nao.
Wakuu wa shule anakosoma Cole wanasema roboti hiyo inawasaidia kupunguza gharama za mwanafunzi huyo.na wanajaribu kuzungumza kuwa hawajui ingekuwaje kwa mwanafunzi huyo bila kifaa hicho,pengine ingewalazimu kumpeleka mwalimu kila siku nyumbani kwa akina Cole kumfundisha,lakini roboti hiyo inamsaidia Cole kupata elimu bora,kwa kumpa maelekezo kupitia waalimu wake kama kawaida na roboti hiyo imekuwa sehemu ya darasa la Cole.
Kwa muujibu wa maelezo ya Cole, roboti hiyo si sanifu sana lakini si haba ni mwanzo mzuri na maendeleo yako wazi mbele yake.
Madaktari wanaofuatilia afya ya kijana huyo ,wanasema kwamba Cole atarejea shuleni akiwa hali ya kawaida mapema mwezi ujao.

Monday 23 February 2015

Kova atoa ufafanuzi juu ya kutekwa kwa Kiongozi wa JKT





KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema aliamini kwamba Mwenyekiti wa Umoja wa Wa wanajeshi waliokuwa kwenye mafunzo JKT ,wanaoshinikiza Serikali iwatafutie Ajira kwamba ametekwa na watu wanadaiwa ni Usalama wa Taifa,badala yake Jeshi hilo limesema litafanya Uchunguzi ili kujilidhisha juu ya Sakata hilo.AnaripotiKAROLI VINSENT Endelea nayo.
Kauli hiyo ya Jeshi hilo la Polisi imekuja huku bado Mwenyekiti huyo Bwana GEORGE S/O GALUS MGOBA,Miaka 28 akiwa amelezwa kwenye Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na kutupwa kwenye Msitu ulioko Pugu Mkoa wa Pwani huku mwili huo ukiwa umechoka kutokana na kipigo alichopigwa watekaji hao.
Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa mda huu Jijini Dar es Salaam,na Kamishna wa kanda Maalumm ya Dar es Salaam Suleimani Kova wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kova huku akisema kwa kujihamini amesema jeshi hilo haliamini kama kiongozi huyo ametekwa mpaka pale watakapofanya uchunguzi na kulidhisha.
“Taarifa za kutekwa siwezi kuziaamini mpaka tuunde tume ichunguze na tufahamu nani kamteka huyo mtu,ili tujue harafu tuweze kubaini maana isije kuwa watu wanataka umahaarufu kwa kutumia mipango hiyo,na tukimaliza kuchunguza kama ni kweli ametekwa tutachukua hatu”
“Kwasababu huyo mwenyekiti anasema ametekwa na amechomwa sindano ya sumu na watekaji,kwanini sasa anakataa kupimwa na madaktari,kuna nini hapa tena anataka hadi kutoroka hospitalini na juzi tulimkamata nje ya mrango wa hospitali akitaka kukimbia sasa hapa kuna nin jamani kwahiyo lazima tufanye uchunguzi suala hili”amesema Kamishna Kova.
Mtifuano wa Kamishan Kova na Waandishi wa Habari
Katika hali ya kushangaza wakati wa mkutano huo na waandishi Wa Habari ulibadilika na kuwa sehemu ya Mabishano pale Waandishi hao walipokuwa wanataka ufafanuzi kuhusu kurudia mara kwa mara kwa matukio hayo ya utekaji kwa watu mbalimbali kwaanzia—
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dokta Steven Ulimboka na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya NewHabari nchini Bwana Kibanda na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mawio Saed Kubenea ambao wate walifanyiwa vitendo viovu na vya kihalamia.
Kamishna huyo akageuka mbogo na kuwataka Waandishi wa Habari waache maswali ya Uchochezi kwani matukio hayo yalishafanyiwa kazi na ufumbuzi ulishapatikana na aliwataka waandishi wakitaka kuuliza maswali ya hayo waandae siku maalum kwa ajiri ya maswali na yeye atakuwa tayari kuwajibu.
Katika hatua Nyingine Jeshi hilo Kanda maalum ya Dar es Salaam limesema limewakamata vijana wapatao watano ambao ni viongozi wa “Umoja wa Kikundi cha wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa” kwa makosa ya uchochezi na mikusanyiko isiyo halali jijini Dar Es Salaam. Watu hao wanatabia ya kujikusanya kwenye kundi la vijana wasiopungua 300.
Kamishna Kova amesema Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa umoja huo hauna usajili kisheria na hakuna ahadi yeyote ambayo kikundi hicho kimepewa.
Ambapo Kamishna huyo amewataja Wanaohojiwa mpaka sasa ni pamoja na Mwenyekiti wa kikundi hicho aitwaye GEORGE S/O GALUS MGOBA, Miaka 28, Mkazi wa Mabibo Loyola.
Mwingine ni Katibu wa kikundi hicho aitwaye LINUS S/O EMMANUEL, Miaka 28, Mkazi wa Tabata.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa umoja wa vijana waliohitimu JKT anayejulikana kwa jina la PARALI S/O ARUWERA KIWANGO, Miaka 25, Mkazi wa Temeke Mikoroshini, anatakiwa kujisalimisha haraka katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Polisi Kanda Maalum Dar es salaam au kituo chochote cha Polisi cha karibu na mahali aliko. Mtuhumiwa huyo alitoroka baada ya kugundua katibu wake amekamatwa hivyo anatakiwa ajisalimishe kuhojiwa kwa matukio hayo.
Kamishna huyo amesema Katika suala hili la wahitimu wa JKT, kuanzia sasa Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kudhibiti mkusanyiko au mkutano wa aina yeyote kwani haina uhalali wowote kisheria. Imegundulika kwamba mikusanyiko ya vijana hawa ni uchochezi na siyo halali kisheria hivyo haikubaliki. Yeyote atakayejaribu kushiriki katika mkusanyiko wa aina hiyo awe ni kiongozi au mjumbe atachukuliwa hatua kali haraka sana.
Historia ya kutekwa
Mnamo tarehe 22/02/2015 majira ya saa 11:45 jioni mtuhumiwa GEORGE S/O GALUS akiwa chini ya ulinzi alijaribu kutoroka kutoka wodini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa lakini Polisi walimbaini na kumkamata kabla hajatokomea. Jalada la utoro chini ya ulinzi halali limefunguliwa na uchunguzi linaendelea.
Aidha tukio la mtuhumiwa GEORGE S/O GALUS kudai kutekwa kati ya tarehe 16/02/2015 hadi 19/02/2015 linaendelea kuchunguzwa kwa ushirikiano kati ya Mkoa wa Pwani na Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kubaini ukweli wa taarifa hiyo na kuwajua wanaosemekana kumteka

Waziri Majaliwa ataka shule kufanya tambiko

Mpwapwa. Ingawa Serikali ya Tanzania haiamini katika ushirikina wala matambiko, kuna watu mbalimbali na jamii tofauti zinaamini katika mambo hayo.
Serikali imekuwa ikipinga na kulaani vitendo vinavyoashiria ushirikina hata kuwashughulikia watu wanaonaswa wakishabikia imani hizo potofu.
Hata hivyo baadhi ya maeneo nchini bado watu wake wanaendeleza imani za kishirikina pamoja na matambiko.
Hata hivyo siyo jambo la kawaida kwa kiongozi hasa wa Serikali kusikika akihimiza kufanyika kwa matambiko ingawa kimsingi tukio hilo linahesabiwa kuwa ni namna ya kutafuta ufumbuzi kwa njia za kiakili na siyo ushirikina.
Ndivyo ilivyotokea hivi karibuni wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Ni kama hadithi, lakini katika tukio la Februari 8 asubuhi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa maagizo ya kufanyika kwa tambiko muda mfupi baada ya kuwasili eneo la Sekondari ya Mpwapwa kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wanafunzi wa kike ambao bweni lao liliteketea kwa moto.
Baada ya maelezo kutoka kwa mkuu wa shule hiyo pamoja na mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu, naibu waziri aligeuka na kutoa maagizo ya kufanya matambiko mazito katika eneo hilo.
Ilivyokuwa
Mkuu wa Sekondari ya Mpwapwa, Nelson Milanzi alianza kwa kutoa simulizi ya tukio la moto ulioteketeza mabweni ambalo lilitokea Januari 20 mwaka huu akisema kuwa vituko vilianza siku moja kabla ya tukio.
“Wanafunzi walitoa maelezo kwamba kulikuwa na nyoka mkubwa aliyeonekana akishuka kutoka katika paa la bweni na alipodondoka chini, uliwaka moto mkubwa. Lakini cha ajabu, moto huo uliunguza shuka mbili za bluu mashati mawili na ghafla ulizimika. Majivu niliyakuta,” anasimulia Milanzi.
Mkuu huyo anasema kuwa tukio hilo lilikuwa na ajabu kiasi cha kumfanya akusanye wanafunzi wa kiume na walimu zaidi ya 10 na kuwapandisha katika dari na kuanza kufanya msako mkali, lakini hawakumuona nyoka huyo.
Siku iliyofuata, mambo yaligeuka, nyoka yule yule aliyeungua jana, alitua chini ghafla na safari hii kukiwa na mwanafunzi mmoja wa kike na moto uliwaka na kushika kasi ya ajabu, ambapo kila kilichokuwa ndani kiliteketea.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi huyo, aliyemnukuu mwanafunzi aliyekuwa ndani ya bweni, hii ni mara ya pili kukutwa na mambo ya ajabu kama hayo.
Anasema kuwa mwanafunzi huyo alieleza kuwa katika kipindi cha mitihani mwaka jana alitokewa na mambo ya ajabu ambayo yalimfanya kushindwa kuhitimu kidato cha sita, hivyo kulazimika kurudia darasa hilo.
Kwa mujibu wa walimu, mwanafunzi huyo (jina tunalo) ni miongoni mwa wasichana wenye vipaji vya hali ya juu, lakini inasemekana kuwa bibi yake anayetajwa kuwa mganga wa kiasili anataka kumrithisha mikoba, lakini binti huyo alipokataa ndipo mambo hayo yalimkuta.
Mbali na tukio hilo, Milanzi anakiri kuwapo kwa matukio mengine ya ajabu yanawakumba hata wanafunzi wa kiume ambao mara kadhaa hulazimika kuita viongozi wa dini kwa ajili ya kuombewa.
Simulizi ya mbunge
Mbunge wa Mpwapwa Mjini, Gregory Teu ni miongoni mwa watu waliohudhuria ujio wa naibu Waziri Majaliwa, ambaye kwa kinywa chake anaeleza kuwa alikulia eneo hilo wakati huo baba yake (George) akiwa mwalimu shuleni hapo, kilipokuwa chuo cha kilimo kabla ya kuwa shule ya sekondari.
Maelezo ya mbunge huyo yanafanya watu wengi kupatwa na mshangao, hasa pale anaposisitiza kuwa taarifa za ‘redio mbao’ kuhusu ushirikina, zina ukweli ndani yake juu ya kilichojificha nyuma ya moto huo.
Teu anasema kuwa mambo yaliyotokea ingawa wengi hawaamini ni ya kweli na kwamba ni lazima kuwaita viongozi wa dini zote ili kuliombea eneo hilo na kuondoa mikosi na mapepo. “Mimi nimekulia hapa, baba yangu alikuwa mwalimu wa kilimo enzi hizo. Hili bweni lililoungua ndipo ilipokuwa maabara ya kilimo, nasema lazima hapa watu waje kuombea na tutaandaa utaratibu kwa gharama yoyote,” anasema Teu.
Anabainisha kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yaliyokuwa tulivu nyakati zote na halikuwahi kukumbwa na mambo ya ajabu kama yanatokea sasa.
Majaliwa ashituka
“Kabla sijasema mambo mengi, naomba kuagiza na hili liwe ni agizo kwamba, lazima wazee waje hapa ili kufanya mambo yao maana haiwezekani nyoka akageuka kuwa moto. Hii ni ajabu kweli, ndugu zangu, isiwe viongozi wa dini pekee yao tu,” anasema Majaliwa.
Naibu waziri huyo anasema kuwa katika Tanzania mambo kama hayo kwa siku hizi ni ya kawaida na kwamba kuna maeneo mengine mbali na kuwaita viongozi wa dini zote huanza na wataalamu kama wazee wa mila.

Anatoa mfano kuwa katika Shule ya Sekondari ya Mahuta, mkoani Lindi kuliwahi kutokea mambo kama hayo, lakini walipoitwa wazee walipita na kuimba na hali ikatulia.
“Unaweza kukuta wakaja hapa na kuimba tu na wakitoka mambo yote yanakuwa safi, huenda kuna mzee yupo hai au alishatangulia mbele za haki, lakini ana manung’uniko ya miaka mingi kwamba ardhi yake ilitwaliwa bila ya kulipwa fidia”, anasema
Anasisitiza kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya utamaduni ambao jamii haina budi kuukubali na usikwepwe ili kunusuru na kuondokana na athari zinazoigharimu Serikali.
Agizo la waziri linaeleza kuwa lazima mambo hayo yafanyike katika kipindi kifupi kijacho, kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo jingine kwani bila ya kufanya hivyo inaweza kuwa sawa na kudharau mizimu.
Wazee wakubali
Mzee Mohammed Athuman Mwile (86), mmoja wa wakazi jirani na shule hiyo anakiri kuwa yanapotokea mambo ya ajabu kama hayo ni lazima kuikumbuka mizimu pamoja na watu waliotangulia mbele za haki kwa kutumia utaratibu maalumu.
“Agizo la naibu waziri kwetu ni jambo la kheri, tunachoweza kufanya sasa ni utekelezaji wa haraka, ili tutimize wajibu wetu na kuwaachia mambo yao nao,” anasema Mwile.
Mzee huyo anasema kuwa suala la matambiko katika mambo yanayoleta migogoro ni la kawaida na la muda mrefu linalostahili kuendelezwa katika nyakati hizi.
Anasimulia kuwa zamani eneo la Mpwapwa lilisifika kwa matambiko ikiwamo kuomba mvua kupitia mizimu na kila lilipofanyika hali ilikuwa nzuri na mambo yalirejea bila kuleta madhara.
Hata hivyo, Mwile anaeleza kwamba anaamini kuna dini zinazoweza kuombea mapepo yakatoka, lakini inapobidi kufanya matambiko hakuna shida yoyote.
Kuhusu vifaa, mzee huyo anasema kuwa tambiko huhitaji kondoo pamoja na nguo nyeusi na kwamba kama watajiridhisha kuwa ni tambiko dogo, hakuna haja ya kufanya yote, bali ni wazee kusema maneno yao tu. Mwinjilisti Jackson Emmanuel wa Kanisa la EAGT, anasema yupo tayari kufanya maombi, lakini pia anakubali wazee kufanya matambiko kama imani yao inawatuma hivyo.
“Tunachoamini sisi ni kwamba tutalifunika eneo hilo kwa damu ya Yesu na hakuna kitu kitakachotokea tena. Mambo ya matambiko siamini, lakini kama wako wanaoamini, basi watangulie ili sisi tukasafishe,” anasema Emmanuel.
Wakati maandalizi yakiendelea, hofu inazidi kuenea kwa wanafunzi ambao wanaona kuwa mambo hayo yakianza tena, huenda milango itakuwa ikifunguka kukaribisha mizimu.
Mwanafunzi Rhoda (si jina lake) anamtaka mkuu wa shule kuachana na mambo yote kwa madai kuwa yanaweza kuita mapepo wabaya ambao mwishowe yatawadhuru zaidi.

SOURCE; MWANANCHI

Chupi inayobana yamtoa mbunge kwenye kikao cha bunge

suruali ya ndani iliobana yamtoa mbunge ndani ya bunge Canada
Mbunge mmoja wa Canada alitoa sababu ambayo haijawahi kusikika iliomlazimu kutoka bungeni kwa haraka.
Amesema kuwa suruali yake ya ndani ndio iliomlazimu kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ikim'bana.
Mbunge huyo wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika kwamba vazi hilo lilimbana sana na kumzuia kuweza kuendelea na kikao cha kupiga kura.
Hatahivyo alifanikiwa kurudi kwa wakati na kupiga kura yake.
Baadaye mtandao wa twitter ulijaa ujumbe wa kisa hicho.
Mbunge huyo alizua ucheshi miongoni mwa wabunge wenzake liposema kwamba alinunua suruali hiyo kwa bei ya chini bila kujua kwamba ilikuwa ndogo.
Spika wa bunge hilo alisema kwamba alimuagiza mbunge huyo kuketi chini wakati alipotaka kutoka.

Akata vidole ilikuonyesha mapenzi kwa wapendwa wao walioaga dunia

 
Jamii moja inawakata viganja wapendwa wao ilikuonyesha mapenzi kwa wapendwa wao walioaga dunia
Duniani kuna afua mbili. Kufa au kupona.
Jamii nyingi hutofautiana jinsi wanavyomkaribisha mwana wao humu duniani na pia jinsi wanavyopuaga anatangulia mbele ya haki.
Katika jamii nyingi duniani, kuna tamaduni tofauti za kuomboleza,kuadhimisha, na kuwazika wapendwa wao.
Jamii moja inayoonesha mbinu za kipekee za kuomboleza na ya kupigiwa mfano ni ile ya Dani, iliyoko Magharibi mwa Papua New Guinea.
Tabaka hilo huwa linaomboleza wapendwa wao kwa kujikata vidole vyao, kama dhihirisho ya kuwa kweli ulikuwa unampenda yule aliyeaga dunia !
Tamaduni hiyo ambayo inaonekana ya kutisha imekita mizizi sana miongoni mwao na si ajabu unapotembeatembea kijijini utashangaa kuwaona watu waliokatwa viganja vyao vikaisha.
Hilo likiwa dhirisho kuwa amefiwa na wapendwa wake.
Wakaazi hao wa bonde la Baliem wamekuwa wakifuata tamaduni hiyo kwa miaka na mikaka na hivyo sio jambo ambalo linawezatoweka kwa haraka.
Mtindo huu hufanyika kwa yeyote ule mwenye uhusiano na marehemu, wakiwajumuisha wazee, wanawake na hata watoto.
Utamaduni huo huanza kwa ibada kwa minajili ya kufukuza mapepo ya marehemu, na pia kama njia ya kutumia maumivu ya kimwili kuonyesha huzini na mateso ya kufiwa.
Vidole vyao hufungwa kwa kamba, kisha kukatwa na shoka, vipande vilivyokatwa huchomwa kwa moto na jivu huhifadhiwa.
Jamii ya Dani
Wakati mwengine vipande hivyo huzikwa pamoja na marehemu.
Vidole hukatwa hususan kuonyesha upendo kwa marehemu.
Kwa mfano, mume au mke hukatwa kidole na kukizika pamoja na maiti ya mume au mke wake, kama ishara ya upendo.
Haijabainika ni kidole kipi kinachopendelewa ama ishara ya mwili na roho kuunganishwa pamoja milele.
Idadi ya vidole vinavyokatwa ni shara ya wale waliofiwa na waliopendwa katika jamii.
Jitihada zimeanza kufanywa ilikusimamisha matambiko ambayo yanahusisha utamaduni huu ambao madhara yake yanabainika katika jimbo lote wakaoishi jamii hii.

Kuchelewa uwanjani kwalobesha Sadio Mane

Sadio Mane anayechezea Southampton

Meneja wa Southampton Ronald Koeman ametoboa siri kuwa jana alilazimika kumwondoa Sadio Mane ambaye ni raia wa Senegal kwenye orodha ya wachezaji watakaonza katika mechi dhidi ya Liverpool kwa kosa la mchezaji huyo kuchelewa kuingia uwanjani.
Koeman amesema ilibidi kumweka mchezaji huyo pembeni na kumpanga mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Benifica Philip Jurisichi kuchukua nafasi yake.
Koeman alisisitiza kuwa timu hiyo imejiwekea kanuni ambazo ni lazima kila mtu azifuate .
Katika mechi hiyo Southampton wakiwa nyumbani walipata kichapo cha magoli mawili kwa bila majibu kutoka kwa Liverpool katika mechi ya lidi kuu ya England.
Hata hivyo Koeman amejitetea kwamba pamoja na kipigo hicho cha jana bado ana matumaini kuwa timu yake itamaliza msimu wa ligi hiyo ikiwa katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi.

Monday 9 February 2015

Matokeo ya kidato cha Nne yakaribia kutoka

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, umekamilika.
Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde aliliambia gazeti hili wiki hii kuwa “usahihishaji umekamilika na baraza lipo katika uchambuzi wa kuyapanga na tutakapokamilisha tutayatangaza”.
Alipoulizwa ni lini hasa matokeo hayo yatatangazwa, Dk Msonde alisema: “Tumemaliza kusahihisha na mchakato wa kuyapanga ukikamilika tutawaeleza hivyo msiwe na shaka.”
Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo, mwaka 2012 na 2013, Necta ilitangaza matokeo ya kidato cha nne mwishoni mwa Februari na mwanzoni mwa Machi.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka 2013 yalitangazwa Februari 22, mwaka jana na 2012 yalizua gumzo kutokana na asilimia 60 ya watahiniwa kufeli.
Kwa kawaida, muhula wa masomo kwa kidato cha tano huanza Julai, huku Machi na Aprili mchakato wa kuwapangia shule hufanyika wakati Mei na Juni hutumiwa kwa maandalizi kwa wanafunzi hao.
Katika matokeo ya 2013 kama ilivyokuwa katika matokeo ya mwaka 2012, shule binafsi zilikuwa na matokeo mazuri kulinganisha na za Serikali zilizokuwa zikitamba miaka ya nyuma.
Kwa mujibu wa Necta, matokeo ya mwaka 2013, shule kongwe za Serikali na zile za vipaji maalumu, zilishindwa kuingia kwenye orodha ya shule 30 bora.
Shule kongwe kihistoria zimekuwa zikitoka kapa katika matokeo ya Mtihani wa Taifa. Tofauti na matarajio ya wengi, shule hizo nyingi hazikuwamo hata katika orodha ya shule 100 bora.
Baadhi ya shule hizo ni Fidel Castro ambayo ilishika nafasi ya 83, Malangali (172), Ifunda Ufundi (205), Jangwani (226), Bwiru (242), Songea Wavulana (257), Pugu (325) na Azania (333).
Ikiwa ni mwaka mmoja umekamilika tangu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ulipoanzishwa, taasisi ya Hakielimu ilitoa matokeo ya utafiti wake yanayoonyesha hakuna kilichofanyika.
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura alisema Serikali isitumie kigezo cha kuongezeka ufaulu kama ishara tosha ya kuimarika kwa elimu, kwani licha ya ufaulu huu kuonyesha kupanda ghafla, kuna changamoto nyingi katika sekta hiyo ambazo bado hazijatatuliwa na juhudi kubwa zinahitajika.“Mfano migogoro ya mara kwa mara kati ya walimu na mwajiri, utoro wa walimu, ukosefu wa maabara, vifaa vya kufundishia na tofauti kubwa iliyopo katika gharama za utoaji elimu nchini kati ya shule za serikali na shule za binafsi,” alisema Boniventura.

Ivory Coast Mabingwa wa Afrika 2015/2016


Ivory Coast wamekuwa mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya kufuinga Ghana kwa penalti 9 - 8 katika mchezo wa fainali ulichezwa katika uwanja wa Estadio de Bata huko Equatorial Guinea.
Mlinda Mlango wa Ivory Coast Boubacar Barry ambaye alikuwa hapangwi mara kwa mara lakini ndiye aliyeibeba Ivory Coast baada ya kudaka penati na kufunga penalti ya mwisho

Ajali ya Moto ya Ua watu Sita Dar , Waombolezaji walalamikia Jeshi la zima moto

Waombolezaji kwenye msiba uliotokana na ajali ya moto ulioteketeza watu sita wa familia moja, wamelaumu Kikosi cha Zimamoto cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushindwa kufika kwa wakati eneo la tukio.
Juzi familia ya watu sita ya Mzee David Mpira na mkewe Celina, iliteketea kwa moto ikijumuisha Lucas Mpira, Samwel Yegela, Pauline Emmanuel na Celina Emmanuel. Chanzo cha moto huo inadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ndiye pekee aliyenusurika katika ajali hiyo kwa kuwa wakati moto unatokea yeye alikuwa ametoka kwenda matembezini.
Jana, waombolezaji hao ambao wengi ni wakazi wa Kipunguni A ilipoteketea nyumba hiyo, kwa nyakati tofauti walisema hakuna haja ya kuwepo kikosi hicho ambacho mara kwa mara kimekuwa kikifika kimechelewa kwenye maeneo ya matukio ya ajali na hata kama wakiwahi wanakuwa hawana maji.  “Tumepiga simu tangu saa 10.00 usiku mara baada ya kuona moto unateketeza nyumba lakini wamefika hapa saa 12.00 asubuhi wakati moto umeshateketeza kila kitu,” alisema Abdallah Mlele mkazi  wa eneo hilo.
Mlele alikuwa akiungwa mkono na wenzake ambao walisema kwa utendaji unaonyeshwa na chombo hicho ni bora kisiwepo.
“Hakuna haja ya kuwapigia simu ‘fire’ wakati wanakuja kuzima moto wakiwa wamechelewa na wakati mwingine hawana maji,” alisema.
Akizungumzia hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya ambaye ni ndugu wa familia hiyo, alisema si vizuri kuzungumzia suala hilo katika kipindi hiki bali kinachotakiwa ni kusubiri uchunguzi.
“Huwezi ukawalaumu zimamoto kwa sasa, au Tanesco kutokana na hili, tusubiri uchunguzi ndipo tupate pa kuzungumzia,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema jana kuwa wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu chanzo cha moto huo.
“Bado haijafahamika thamani ya vitu vilivyoungua na chanzo cha moto huo, tunaendelea kuchunguza ili kubaini chanzo hasa,” alisema Nzuki.
Naye Msemaji wa familia hiyo, Godfrey Mwandosya ambaye ni mdogo wake na Profesa Mwandosya alisema shughuli zote za mazishi zitaanza kesho saa 5.00 asubuhi kwa kuaga miili ya marehemu kabla ya kupelekwa kwenye Kanisa Katoliki la Ukonga kwa ajili ya ibada.


Alisema baada ya hapo, miili hiyo itapelekwa kwenye makaburi ya Airwing Ukonga kwa maziko yatakayofanyika kuanzia saa 10.00 jioni
Kuhusu ndugu  yake, Emmanuel ambaye amenusurika, alisema: “Emmanuel tunamwacha apumzike…tumeona ni vizuri akakaa sehemu ambayo hataona yanayoendelea hapa nyumbani kwani hali hiyo inaweza kumuathiri kisaikolojia,” alisema.
Hata hivyo, Emmanuel ambaye alikuwa kwenye nyumba ya jirani hakuzungumza chochote wala kujibu salamu ya mwandishi wa habari.
Waliokaribu, walisema amekuwa akizungumza mara chache na marafiki zake na muda mwingi amekuwa akikaa kimya.
Majirani
Majirani walisema Celina Mpira mke wa Mzee David enzi za uhai wao waliishi kwa upendo na majirani zake na kwamba walikuwa wameanza kuwaaga majirani zake.
Neema Kalinga ambaye ni jirani alisema familia hiyo ilikuwa inataka kuhamia eneo la Kibeberu Kitunda kwa sababu wakazi wote wa Kipunguni A wanatakiwa kuhama eneo hilo ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.
“Walikuwa wanakamilisha ujenzi wa nyumba yao nyingine huko Kibeberu, alikuwa ameshaanza kutuaga, kumbe ilikuwa ni safari ya milele,” alisema.
Jirani mwingine Athumani Ismail alisema marehemu David enzi za uhai wake alikuwa mshabiki wa mpira, “tulikuwa tunataniana sana kuhusu vilabu vyetu vya ndani na nje ya nchi,”
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonna Kaluwa ambaye alikuwa miongoni mwa waombolezaji alisema, “huu ni msiba wa wana Kipunguni wote kwa sababu moto umeteketeza familia yote, tushirikiane katika kipindi hiki kigumu.”
Wanafunzi
Miongoni mwa waliokufa ni watoto Pauline Emmanuel anayesoma Shule ya Chekechea ya Tumaini na Celina Emmanuel anayesoma darasa la nne katika shule ya msingi ya Minazi Mirefu, Ukonga, Dar es Salaam.

Hao ni watoto wa Emmanuel Mpira aliyenusurika katika ajali hiyo na mama Mwajuma Issa. Watoto hao walikuwa wakiishi na babu yao.

Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq Marehemu Saddam Hussein kuuzwa

Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq Marehemu Saddam Hussein kuuzwa

Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq marehemu Saddam Hussein imedaiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4.

Licha ya Saddam kunyongwa mwaka 2006,watu bado wanamuenzi na mtu mmoja amejitolea kulipa dola millioni 7 kununua kamba hiyo iliokatiza maisha ya kiongozi huyo wa zamani.

Kulingana na gazeti la Metro,Baadhi ya watu matajiri wanaoitaka kamba hiyo wanatoka mataifa ya Kuwait,Iran na Israel.

Kamba hiyo kwa sasa inamilikiwa na Dr Mowaffak al-Rubaie,mshauri wa usalama wa zamani nchini Iraq,ambaye aliongoza eneo ambalo rais huyo wa zamani aliuawa.

Aliamua kuihifadhi kamba hiyo baadaye na sasa anataka zaidi ya dola millioni 7 kuiuza kamba hiyo

Vifo vya mashabiki Misri vya sababisha Ligi Kusimamishwa

Mashabiki wanadai kuwa mamlaka zilisababisha vurumai zilizotokea baada ya kufungua lango moja pekee

Misri imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.

Kati ya waliofariki ni wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.

Mtandao mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti.Tukio hilo limetokea baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.

Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali ya uma isiharibike.

Polisi wamesema mashabiki hao walikuwa wanataka kuingia uwanjani bila tiketi, wamenukuliwa wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi kutokana na msongamano mkubwa wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.

Ndani ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili ya Watu waliopoteza maisha na wengine waliolala wakiwa majeruhi.

Mashabiki wa Zamalek wanadai kuwa vurumai zilianza mamlaka ya uwanja ilipofungua Geti la waya kuwaruhusu kuingia ndani.

Mashuhuda wanasema uzio ulianguka wakati Watu walipokuwa wakipigania kuingia ndani hali iliyosababisha msongamano mkubwa, mara askari wa usalama walianza kurusha mabomu ya kutoa machozi.

Watu walianza kukanyagana hali iliyosababisha Watu kupoteza maisha.

Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa soka zaidi ya 70 walipopoteza maisha wakati vurugu zilipotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.

Baada ya tukio hilo idadi maalum iliwekwa kwa watakaohudhuria Mechi kwa hofu ya hali ya usalama ,inaelezwa kuwa mipaka hiyo iliyoondolewa hivi karibuni huwenda ikawekwa tena baada ya tukio la mwishoni mwa juma lililopita.

Madrid yapigwa 4 0 na Ateltico madrid

Cristiano Ronaldo ashangaa baada ya kucharazwa mabao 4-0 na Atletico Madrid

Viongozi wa ligi ya La Liga Real Madrid siku ya jumamosi waliona cha mtema kuni waliposakamwa mabao 4 bila jibu na wapinzani wao Atletico Madrid katika mechi ya Derby iliochezwa katika uwanja wa Vincente Calderon.

Real iliokuwa ikiuguza majeraha mengi ililazimika kutaja mabeki m'badala katika mechi yao ya ugenini.

Hatahivyo mabeki hao hawakuweza kuhimili kishindo cha mashambulizi ya mabingwa wa ligi Atletico Madrid.Ateltico madrid

Mabao ya haraka yaliofungwa na Tiago,Saul Niguez yaliiweka Atletico kifua mbele katika kipindi cha kwanza,kabla ya mabao mengine mawili yaliofungwa katika kipindi cha pili na Antoine Griezman na Mario Mandzukic kupiga msumari wa matumaini ya Real.

Baadaye wachezaji pamoja na mashabiki wa Atletico walisherehekea sana ushindi huo.