Wednesday 11 March 2015

Ndege inayotumia umeme jua imetua India

http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/03/09/150309053101_solar_impulse_2_test_flight_640x360_epa.jpg
Ndege ya kwanza inayotumia umeme jua imejaribiwa leo

Jaribio la ndege inayotumia umeme jua kuzunguka dunia pasi na kutumia hata tone moja ya petroli imeingia mkondo wa pili jana baada ya ndege hiyo kufaulu kutua nchini India
Ndege hiyo imetua katika uwanja wa ndege wa Ahmedabad na kuweka rekodi ya kuwa ndege ya kwanza isiyotumia petroli kupaa juu ya bahari ya Arabian zaidi ya kilomita 1468 kuanzia Muscat Oman hadi
Ahmedabad India.
Safari hiyo ilichukua zaidi ya saa 15.
Marubani hao wawili sasa wanapumzika kabla ya kuendelea mbele na mikondo mingine 10 zilizosalia katika jitihada za kuzunguka duniani bila ya kutumia petroli.
Kiongozi wa ujumbe huo Rubani Bertrand Piccard amesema wamefurahishwa mno na jinsi mpango wao unavyoendelea.
Rubani Bertrand na mswisi mwenza Andre Borschberg wanapanga kutumia miezi 5 ijayo kukamilisha safari hiyo.
Ndege hiyo inauwezo wa kupaa hata usiku kutokana na betri zenye uwezo wa kuhifadhi umee kutoka kwa jua
Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi.
Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa sawa na ya ndege kubwa za jumbo zinazotumika kwa uchukuzi wa abiria inamabawa yenye upama wa mita 72.
Hata hivyo inauzani wa tani 2.3 tu uzito sawa na wa gari.
Mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels.
Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku.
Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao.

No comments: