Thursday 30 April 2015

Jeshi la ufaransa latuhumiwa kunajisi watoto

Unyanyasaji wa kijinsia unadaiwa kufanywa kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na mwezi Mei mwaka 2014. Wanajeshi 16 wa Ufaransa wanatuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo.Unyanyasaji wa kijinsia unadaiwa kufanywa kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na mwezi Mei mwaka 2014. Wanajeshi 16 wa Ufaransa wanatuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo.

Serikali ya Ufaransa imetangaza kuanzisha uchunguzi kufwatia tuhuma zinazowakabili wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kutekeleza vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi dhidi ya watoto.

Nakala ya Ripoti inayobaini vitendo hivyo imewakilishwa kwenye gazeti la The Guardian la Uingereza na shirika lisilo la kiserikali “Aids Free World” ambapo wizara ya sheria ya Ufaransa imekiri tayari kuanza uchunguzi unaosimamiwa na Mwendesha mashtaka wa mjini Paris.
Akihojiwa na RFI, mkurugenzi wa shirika hilo, Paula Donovan, amesema wamefanya mahojiano na wasichana wadogo sita ambao walifanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji wa kingono na kubaini kuwa walifanyiwa kitendo hicho zaidi ya wasichana 20 wenye umri kati ya miaka minane na kumi na mbili.
Inaarifiwa kuwa zaidi ya wanajeshi kumi na tano wa Ufaransa walihusika katika kitendo hicho.
Vitendo hivyo vya aibu vilitekelezwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mpoko, karibu na uwanja wa ndege wa Bangui, walikokua wakipiga kambi wanajeshi wa Ufaransa, kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na Mei mwaka 2014. Mahojiano na wasichana hao yalifanyika kati ya mwezi wa Mei na Juni mwaka 2014.
Viongozi wa Ufaransa walifahamishwa hali hiyo. Wizara ya sheria imethibitisha kwamba uchunguzi wa mwazo ulianzishwa mwezi Julai mwaka 2014.
Wakati hayo yakijiri, jukwaa la vyama vya siasa la msaada kwa serikali ya mpito AFDT, linapinga ushiriki wa marais wa zamani Francois Bozizé na Michel Djotodia katika kongamano la kitaifa linalotarajiwa kwa vile viongozi hao wamechangia kuiweka nchi hiyo katika hali isio sawa kama anavyobainisha Nicolas Tiangaye Mwenyekiti wa Jukwaa hilo.

Kocha wa leicester city amtusi mwandishi wa habari baada ya kupokea kichapo toka kwa Chelsea

Kocha wa Leicester City, Nigel Pearson
Meneja wa Leicester City, Nigel Pearson amemshambulia kwa matusi Mwandishi wa habari akimfananisha na ndege aina ya mbuni.
Pearson alifanya kitendo hicho baada ya timu yake kupata kichapo cha 3-1 toka kwa vinara wa ligi Chelsea.
Bosi huyo wa Leicester alimtukana mwandishi Ian Baker aliyemuuliza swali kuhusu madhaifu ya wachezaji wake yaliyosababisha timu kuboronga msimu mzima.
Pearson, hakufurahishwa na namna alivyoulizwa na kuamua kumtukana mwandishi akisema: “Wewe lazima ni punguani sana, sana”.

Wednesday 29 April 2015

Barca yazidi kujikita kileleni baada ya kuichapa Getafe 6-0

Messi,Neymar,Suarez waichakaza vibaya Getafe
Vinara wa La Liga FC Barcelona Jana Usiku wameishindilia Getafe Bao 6-0 na kupanda kuwa mbele ya Timu ya Pili Real Madrid kwa Pointi 5.
Mabao ya Barca yalifungwa na mshambuliaji wao hatari Lionel Messi aliyefunga mara mbili huku, Luis Suarez nae akitupia kambani mabao mawili , Neymar na Xavi wakifunga bao moja moja.
Mabao hayo ya washambuliaji wa Barca, Messi, Suarez na Neymar yamewafikisha zaidi ya mabao 100, kwa Msimu huu.
Hii Leo, Real Madrid walioko nafasi ya pili watakua na kibarua cha kupetetana na Almeria Uwanjani Santiago Bernabeu.
Vita ya kuwania kiatu cha mfungaji bora kiko kwa Cristiano Ronaldo mwenye magoli 39 akifuatiwa na Messi mwenye mabao 38.

Liverpool yaichapa Hull City

Wachezaji wa Liverpool wakipewa maagizo na kocha wao
Liverpool imezidi kujiweka katika hali ngumu ya kuingia katika nne bora ya ligi hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Hull City.
Kipigo hicho cha ugenini walichokipata vijana hao wa Anfield kinawafanya waendelee kubaki nafasi ya tano na pointi zao 58 nyuma Manchester Utd yenye pointi 65.
Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa wakati Chelsea itakapokuwa ugenini kukipiga dhidi ya Leicester City.

Jeshi la Nigeria laokoa wanawake 293 waliokuwa wametekwa

Jeshi nchini Nigeria
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote.

Rais kikwete azindua Meli kubwa za kivita yenye ukubwa wa mita 60

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini ambazo zitakazowezesha usalama wa uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.
Mara baada ya uzinduzi Rais. Kikwete amezikabidhi kwa kamandi ya jeshi la wanamaji hafla iliyofanyika makao makuu ya kamandi hiyo yaliyopo kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema meli hizo zinafanya Tanzania iandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za kisasa kwa mara ya kwanza nchini.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,Dk.Hussein Mwinyi, amesema, meli hizo zitakuwa tegemeo kubwa katika kulinda eneo la maji ya tanzania na rasilimali zake ikiwamo gesi asililia,samaki kwani zina uwezo wa kasi kubwa katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hasa uharamia.
 
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema,lengo la kuwa na meli za jinsi hiyo ni katika jitihada za kuhakikisha jeshi linakuwa na silaha za kisasa za kivita na kutoa mafunzo huku balozi wa china nchini, Lui Youging, akimpongeza Rais Kikwete kwa jitihada za kuimarisha ulinzi wa taifa lake.
 
Meli hizo zimepewa majina ya melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na  melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete ambaye anatarajia kumaliza kipindi chake cha uongozi Novemba mwaka huu.

Tuesday 28 April 2015

Henry asema Arsenal haiwezi kuchukua Kombe kama inamtegemea Oliver Giroud

28080E2600000578-0-image-m-17_1430085416130Thierry Henry ameikosoa sera ya usajili ya Arsenal ya hivi karibuni na ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kununua wachezaji wa wanne wa kiwango cha juu majira ya kiangazi mwaka huu.
Mfaransa huyo anaamini kuwa Arsenal inahitaji golikipa, beki wa kati, kiungo mkabaji na mshambuliaji kama wanataka kushinda kombe la ligi kuu England.
Akizungumza baada ya suluhu ya jana ya Arsenal dhidi ya Chelsea, Henry, amemshambulia Olivier Giroud akidai kuwa The Gunners wataendelea kuhangaika kutafuta ubingwa kama Mfaransa huyo mwenzake ataendelea kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza.
“Nadhani wanahitaji kununua wachezaji wanne-bado wanahitaji golikipa, kiungo mkabaji na nina wasiwasi wanahitaji wachezaji wa juu, wanahitaji mshambuliaji wa kiwango cha juu kama wanahitaji kuchukua ubingwa tena”.
“Tuna mfano mzuri wa Chelsea. Walikuwa wanahangaika kushinda kombe msimu uliopita. Waliingia sokoni walimnunua [Thibaut] Cortouis, [Nemanja] Matic, Cesc [Fabregas] na [Diego] Costa, sasa mambo ni mazuri”.

Dau la Eden Hazard latangazwa

Zinedine Zidane alimsifia Gareth Bale kwamba ni mchezaji wa tofauti sana, baada ya summer kufika mwaka 2013 akahamia Real Madrid. Sasa wasiwasi umetanda kwa Hazard kuwa na uwezekano wa kuhamia Real baada ya Zidane kumsifia hivyo hivyo Hazard akimfananisha kama Cristiano na Messi kwa sasa.
Jose Mourinho akijibu kuhusu maneno ya Zidane alisema kwamba kama Real inamtaka Hazard, yeye (Mourinho) angekua wa kwanza kujua.Lakini kama ni kweli wanamtaka nay eye hajui basi itawagharimu £100 million kwa kila mguu wa Hazard.Mourinho alisema naweza kumuuza kwa Pauni 100 milioni, ikichanganywa na staa mwingine wa dunia (mwenye thamani ya Pauni 100 milioni) kwa hiyo inakuwa Pauni 200 milioni. Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha maana katika msimu huu na jana Jumapili alikuwa akiwania tuzo ya PFA.
Mourinho ambae leo ana mechi na Arsenal alisema kwamba haamini kama Real wanajaribu kum-sign Hazard kwasababu bado hawajamwambia. Uhusiano wake na rais wa timu na CEO hautoi nafasi ya kitu kama hicho kutoka nyumba ya mgongo wake. Lazima wangemwambia kwasababu wana aminiana kikamilifu.
Chochote kinaweza kutokea na Real Madrid kwenye kuweka mzigo mzito kumpata yule wamtakae, sio tatizo kubwa kwao. Tusubili tuone.

Vurugu za zuka Marekamini mjini wa Baltimore

vurugu Baltimore
Vurugu kubwa za mapigano baina ya polisi na waandamanaji zimetokea nchini Marekani katika mji wa Boltimore, baada ya maziko ya kijana Freddie Gray ambaye alikufa kutokana kujeruhiwa alipokuwa mikononi mwa polisi mapema mwezi huu.
Hali ya hatari na kutotembea hovyo imetangazwa katika mji huo kufuatia vurugu hizo.
Kifo cha Freddie Gray ambaye ni kijana mweusi mmarekani mwenya asili ya kiafrika kimesababisha maswali mengi kuhusu matumizi ya nguvu za ziada ya polisi dhidi ya raia wa marekani wenye asili ya kiafrika.
Hata hiyo Msemaji wa polisi wa Baltimore Captain Eric Kowalczyk amesema vurugu hizo pia zimesababisha maafisa wake kujeruhiwa na wengine wapo katika hali mbaya.

Monday 27 April 2015

Yanga mabingwa wapya Tanzania 2014/15

Kikosi cha yanga
kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mwaka 2014/2015
Tmu ya Yanga wamekuwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania kwa mwaka 2014/2015 na hivyo kuivua rasmi ubingwa Azam iliyokuwa ikishikilia taji hilo.
Ubingwa wa Yanga unakuja baada ya kuizamisha timu ya Polisi Morogoro kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jumatatu, jijini Dar es Salaam, ilikuwa inahitaji ushindi wa pointi tatu kutangazwa bingwa mpya ikibakiwa na michezo miwili mbele.
Kabla ya mchezo huo Yanga ilikuwa inaongoza kwa pointi 52 ambapo sasa imefikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote ya ligi hiyo ya Vodacom.

Baba wa Kim Kardashia ajitangaza kuwa ni shoga

Bruce Jenner
Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla ya kuwa nyota wa kipindi cha televisheni na familia moja maarufu duniani ''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha kwa miaka mingi.
''Kwa nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia Sawyer kutoka ABC katika mahojiano maalum yaliopeperushwa hewani siku ya Ijumaa.
''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini moyo na roho yangu na kila kitu ninachofanya maishani ni sehemu yangu.'' Jenner ambaye ana umri wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa kike ni sehemu yangu.
hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Bruce Jenner
Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New York na California, Jenner alielezea kwa kina mapambano yake ya kuwa na jinsia mbili tangu utotoni.
''Akili zangu ni za kike sana kuliko za kiume.'' Ameongezea. '' Ni vigumu sana watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''
Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu shati na suruali ndefu alisema kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili kujitangaza kwa kuwa hakutaka kuwavunja moyo watu.
Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na madada zake waliweka siri kuhusu jinsia yake na kwamba walikuwa watu waliokuwa wakijua siri hiyo.
Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .
Jenner ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja na watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.

mabomu yarindima Arusha, wanafunzi wa Patandi teaching College waandamana na kufunga barabara

Image result for mgomo wa chuo
Jeshi la kutuliza Ghasia wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanyisha waandamanaji
Mabomu ya rindima Arusha tena baada ya wananfunzni wa chuo cha ualimu Patandi kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha maeneo ya Tangeru, ili kuishinikisa serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kumwondoa au kumfuta kazi Mkuu wao wa chuo,
Mwandishi wetu aliyekuwepo katika eneo la tukio alimtafuta rais ya seriikali ya wanafunzi wa chuo hicho na kumhoji “Alisema chanzo cha Mgomo huo ni tabia ya mkuu wa chuo kuwakandamiza na kuwanyima uhuru wao wa kufanya mambo , aliongeza kwa kusema Mkuu wetu wa chuo huwa anatushinikiza kuchapisha na kutoa kopi za “notes’kwa ajili ya kusoma katika stationary yake angali zipo stationary nyingi chuoni pia amekuwa akiwalazimisha wanachuo kula katika mgahawa wake (Cafeteria) huku ikitoa huduma kwa gharama ya hali ya juu, hivyo kufanya wanafunzi hao kushindwa kuhimili hali ya maisha katika chuo hicho
Image result for mgomo kufunga barabara
Askari wakitunza usalama
Pia mkuu wa chuo hicho aliwazidishia hasira wanachuo hao kwa kupiga makofi mwanafunzi  hii nai baada ya mwanafunzi huyo kuchukua kibali toka kwa mkufunzi wa zamu ili akasuke nywele zake ndipo alikutana na mkuu wa chuo na kumdai kibali na kukichana , haikutosha aliitisha wita mwanafunzi huyo ofisin na kumpiga kipara nywele zake , wanafunzi wenzake walipona kuwa mkuu wao  kamdhalilisha huku akijua kuwa mwanafunzi  huyo ni mjamzito , Kitu ambacho serikali ya wanafunzi wa chuo iliona ni unyanyasaji wa hali ya juu  ndipo walipoona wafunge barabara kwa kuchoshwa na tabia za Mkuu wao wa chuo .

Buyern Munich yatangaza ubingwa mapema

Wachezaji wa Bayern Munich ya Ujerumani wakishangilia ushindi
Klabu ya soka ya Ujerumani Bayern Munich ya Ujerumani imenyakuwa taji la ligi kuu ya nchi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo huku shukrani zikienda kwa klabu ya soka ya Borussia Monchengladbach kwa kuichabanga Wolfsburg kwa bao 1-0 siku ya jumapili.
Kipigo hicho walichokipata Wolfsburg ndicho kilichofanya mashabiki wa Bayern kusherehekea ubingwa kwa kuwa timu hiyo ndio inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 61, wakati vijana wa Pep Guardiola yaani Bayern Munich wawakiwa kileleni kwa pointi 76 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutokana na idadi ya mechi zilizobaki.
Lakini wachezaji wa wa Bayern hawatokuwa na muda wa kutosha kusherehekea ubingwa huo kutokana na majukumu mazito yanayowakabili ya klabu bingwa Ulaya ambapo watavaana Barcelona mnamo May 6 katika mchezo wa nusu fainali.

Nigeria wafunga ubalozi wa Afrika kusini nchini mwao

Maandamano ya kupiga chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini
Nchi ya Nigeria imewaita mabalozi wake waishio nchini Afrika Kusini warejee nyumbani kufuatia mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya wenyeji .
Mpaka sasa watu saba wameshapoteza uhai kufuatia mashambulizi hayo, yaliyoanza wiki tatu zilizo pita.mali zimeharibiwa vibaya na mashambulizi hayo yamizusha hofu kubwa miongoni mwa raia wa kigeni .
Balozi wa Nigeria mjini Pretoria,mji wa kibiashara na kwingineko wanatarajiwa kurejea Nigeria kwa ushauri zaidi .
Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki ilieleza wazi baadhi ya waafrika kusini walia andaa maandamano ya Amani na shutuma za Jacob Zuma kulaani mashambulio hayo na kama ambavyo alifanya mfalme Zulu King Goodwill Zwelithini, ambaye anashutumiwa kuwa maoni yake ndiyo chanzo cha vurugu hizo.
Wabunge nchini Nigeria wameitaka serikali ya Afrika Kusini kulipa uharibifu uliotokea na kikundi cha kutetea haki cha Nigeria kimesha peleka malalamiko yake katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC.
Mwishoni kwa wiki iliyopita,katika taarifa iliyotolewa nchini Afrika Kusini,kutoka katika kitengo kinachoshughulikia mahusiano ya kimataifa na ushirika kimerusha lawama zake kwa serikali ya Nigeria kwa hatua waliyoichukua na kuielezea kama isiyo bahati na ya kusikitisha
Katika utetezi wake serikali ya Afrika Kusini imesema kwamba hatua ya mashirika ya kiraia kulaani na kukemea mashambulizi hayo na kutoa wito wa kusitishw akwa mashambulio dhidi ya wageni kutokana na hayo utekelezaji, utulivu wa kijamaa na utaratibu na amri ilitolewa .
Kipekee,wizara ya mambo ya mambo ya nje ya Liberia katika taarifa iliyotolewa Jumapili pamoja na mambo mengine, imeipongeza Afrika Kusini kwa kuadhimisha miaka kadhaa leo April 27 tangu kuondolewa kwa ubaguzi wa rangi nchini humo na uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika nchini humo mnamo mwaka 1994,wizara hiyo imezungumzia hali ngumu nchi hiyo iliyokuwa inapitia ,katika taarifa hiyo Rais Ellen Johnson Sirleaf, mshindi wa tuzo ya Amani,alisema kwamba alikuwa akiiombea nchi hiyo kupata ujasiri na nguvu ya pamoja kwa umuhimu mkubwa iweze kuongoza watu wake katika maamuzi sahihi katika harakati za kutaka kuufunga ukurasa wa kiza uliokuwa ukiiandama nchi hiyo dhidi ya raia wa kigeni.

Waganga wajadi wajitolea kumtibu Wema sepetu

Waganga wa kienyeji wanaotoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania wamejitolea kumtibu Msanii WemaSepetu aweze kupata mtoto.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya Waganga hao waliojitolea walipiga simu kwa mtandao wa Bongo Movies.com baada ya kukiri kwa nyota huyo wa filamu kwamba hawezi kupata mtoto.
Wameapa kumtibu tatizo hilo.''Wajua kuna wanawake wanaopata matatizo madogo kama kutoweza kupata mtoto licha ya kwamba kuna matabibu wanaoweza kutatua matatizo yao.
Tatizo la wema sio la kumtia wasiwasi,linaweza kutibika''walisema.
Mpatie nambari yangu ya simu na umwambie anipigiemmoja wa waganga hao alisema.
Na ili kutaka kujua vile Wema alijibu ombi hilo ,inadaiwa kuwa alikubali kusaidiwa na watabibu hao lakini kwa masharti.
''Kuna wengi zaidi mbali na waganga ambao wamejitolea kunisaidia.nina zaidi ya ujumbe 400 niliyotumiwa katika mtandao wangu wa WhatsApp huku simu nyingi zikipigwa.Ukweli ni kwamba niko tayari kupokea usaidizi huo.'',alijibu.

Eden Michael Hazard atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka England

Image for the news resultBaada ya kusubiri kwa misimu miwili hatimae Eden Hazard wa Chelsea ameibuka mchezaji bora wa mwaka wa England na kutwaa tuzo ya PFA.
Hazard mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 13 na na kusaidia wafungaji (assists) 8 katika michezo 33 ya ligi kuu ya nchi hiyo na kuisaidia timu yake kushika ususkani katika msimamo wa ligi.
Naye Harry Kane mwenye umri wa miaka 21 ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku naye Ji So-Yun wa Chelsea akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake.
Hazard ambaye msimu uliopita aliibuka mshindi kwa upande wa chipukizi alikabidhiwa tuzo yake katika hoteli ya Grosvenor jijini London jana Jumapili. " ninafuraha sana. Nataka siku moja niwe mjichezaji bora kabisa na na nilichofanya msimu huu ni kucheza vizuri na timu yangu imecheza vizuri sana" alisema Hazard baada ya kupokea tuzo hiyo. "sijui kama nastahili kushinda lakini jambo hili ni zuri kwangu. Ni jambo zuri kupigiwa kura na wachezaji kwasababu wanajua kila kitu kuhusu mpira" aliongeza mchezajia huyo.

Watu wawili wauawa kwenye vurugu Burundi

Wawili wauawa kwa risasi za polisi Bujumbura BurundiRaia wawili wa Burundi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika machafuko yaliyotokea leo huko Bujumbura mji mkuu wa Burundi. Machafuko hayo ya leo yametokea katika maeneo mengi ya mji mkuu Bujumbura, wakati watu walipoandama kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo ya kuamua kugombea urais kwa muhula mwingine wa tatu. Watu walioshuhudia wameongeza kuwa mmoja wa waandamanaji katika machafuko ya leo huko Bujumbura ameuawa katika wilaya ya Ngagara na mwingine katika wilaya ya Musaga huko huko Bujumbura. Habari zinasema kuwa polisi wa Burundi walitumia silaha za moto, gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya waandamanaji. Leonce Ngendakumana Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Frodebu amesema kuwa, wameitisha maandamano ya amani, hata hivyo polisi na wanamgambo wa chama tawala cha Burundi wamewafyatulia risasi hai waandamanaji.

Rais Kikwete awaongoza maelfu ya watanzania kuadhimisha miaka 51 ya Muungano

Rais Jakaya Kikwete ambaye pia amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama amewaongoza maelfu ya watanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru jijini dar es salaam.
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na maelfu ya watanzania,mabalozi,viongozi wa serikali na vyama vya siasa,Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo akiwa katika gari la wazi akiwa  na mkuu wa majeshi ya ulinzi Janerali Davis Mwamunyange na kuzunguka uwanja wa uhuru akiwapungia mkono watanzania.
Rais kikwete kisha alipanda katika jukwaa maalum lililoandaliwa na kisha mizinga 21 ilipigwa pamoja na wimbo wa taifa na hatimaye alikagua vikosi mbalimbali vya majeshi ya ulinzi kabla ya kupanda katika jukwaa kuu nakusalimiana  na viongozi waandamizi wa serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha vikosi mbalimbali vya majeshi ya ulinzi vilipita mbele ya jukwaa kuu na kuonyesha ukakamavu na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya viongozi wastaafu walioshuhudia mkataba wa muungano  mwaka 1964 akiwemo Spika Mstaafu Pius Msekwa wamewataka vijana kuuenzi muungano Tanzania na Zanzibar huo hususani katika kipindi hiki taifa linapokabiliwa na uchaguzi mkuu pamoja na mchakato wa katiba pendekezwa.
Burudani mbalimbali zilipamba sherehe hizo ikiwemo vijana na halaiki kuchora maumbo na kuandika maeneo mbalimbali,huku kikosi cha vijana wengine wakionyesha ukakamavu wa kupita kwenye moto pamoja na kutambaa katika kamba,pamoja na ngoma za asili zilikuwa kivutio kikubwa uwanjani hapa.

Sunday 26 April 2015

Nesi amcharaza mjamzito viboko,asababisha kifo cha mtoto

Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani hapa, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya. Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy. “Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji. “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo. Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

Muuguzi aliyemchapa mjamzito asakwa na polisi

Jana kulikuwa na habari iliyomuhusu mwanamke mmoja wa Dodoma ambaye alikuwa amepelekwa kituo cha afya cha Muungano wilayani Chamwino kwa ajili ya kujifungua, lakini akakutana na vitendo vya kikatili vilivyochangia mtoto afie tumboni.
Kwa mujibu wa habari hiyo, muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo aliamua kumchapa viboko mjamzito huyo baada ya kumuona anashindwa kujikakamua ili kumsukuma mtoto atoke na alikuwa akifanya hayo akidai kuwa mwanamke huyo ni mzembe na anadeka ndio maana alikuwa anashindwa kujifungua.
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikiri kuwapo kwa taarifa za mama huyo kuchapwa viboko akiwa chumba cha kujifungulia na kwamba wameagiza uchunguzi ufanyike ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo na hatua zichukuliwe.
Wakati uchunguzi huo ukifanyika, hatutaki kuamini kuwa kifo cha mtoto huyo kimesababishwa na kupigwa kwa mama yake, lakini kinachotushangaza ni jinsi mama huyo alivyoshughulikiwa hadi kupoteza kiumbe hicho alichokitunza tumboni kwa miezi tisa.
Muuguzi huyo ni mmoja tu kati ya wengi ambao wamekuwa wakiwafanyia vitendo visivyo sahihi wagonjwa wanapoenda hospitalini kwa ajili ya kupata tiba, hasa wajawazito ambao hulundikiwa mzigo wa maneno kuanzia wanapofika hadi wanapojifungua. Imekuwa ni kawaida kwa kina mama wajawazito kusimangwa, kutolewa maneno machafu na kucheleweshewa huduma na matokeo yake baadhi hujikuta wakipoteza watoto na wengine kulazimika kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji.
Wengine wamekuwa wakilalamika kuwa wauguzi huwaomba rushwa na wasipotoa, hufanyiwa vitendo hivyo vya kikatili na kudhalilisha.
Mambo hayo husababisha wanawazito wanaoishi kwenye maeneo ya nje ya miji, kuona ni heri kujifungulia majumbani au kwa waganga wa jadi ambako wanaona hakuna unyanyasaji kama wanaofanyiwa hospitalini na matokeo yake hukumbana na athari kubwa zaidi.
Tunatambua kuwa wauguzi wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na Serikali kutotenga fedha za kutosha kwenye sekta hiyo, lakini hatuamini kuwa hali hiyo ndiyo inayosababisha wauguzi wafanye vitendo vya unyanyasaji kwa wagonjwa, na hasa wajawazito.
Tunaamini kuwa katika mazingira hayo magumu, bado wauguzi wanaweza kuonyesha moyo wa upendo, kufanya kazi kwa weledi na maadili angalau kwa kiwango kinacholingana na mazingira waliyonayo ili juhudi za kuhimiza kina mama wajifungulie hospitalini au kwenye vituo vya afya zizae matunda.
Itakuwa ni kitu cha ajabu kama Serikali inapiga kelele kuhimiza wananchi kwenda kwenye vituo vya afya au hospitalini wakati wauguzi nao wanafanya vitendo ambavyo vinakatisha tamaa wananchi kwenda sehemu hizo.
Wakati mama huyo akiendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, ni vizuri kwa uongozi wa mkoa kufanya uchunguzi wa kina kama ulivyoahidi ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo lililotokea Aprili 3 mwaka huu, takriban siku 20 zilizopita.
Imekuwa ni kawaida kwamba tukio lolote baya likiripotiwa na vyombo vya habari, wahusika huwa wepesi kusema wanafuatilia kupata taarifa kamili na wanapoona hali imepoa, nao wanachana nalo na hakuna hatua zinazochukuliwa. Matokeo yake ni vitendo hivyo kuendelea kuwa sugu.
Hatutarajii kwamba uongozi wa mkoa wa Dodoma utaingia kwenye mkumbo huo wa kusubiri hali ipoe, bali utatekeleza ahadi yake ya kufanyia kazi taarifa hizo ili wahusika wachukuliwe hatua.
Na kwa kuwa huduma duni ni tatizo sugu hospitalini na kwenye vituo vya afya na hospitalini, Serikali haina budi kufuatilia vitendo hivyo ili kuvikomesha.

Raia wa Tanzania walioko Afrika kusini warudishwa Nyumbani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benardb Membe.
Serikali imewarejesha nyumbani Watanzania 26 walioathiriwa na mashambulizi yanayofanywa na wazawa dhidi ya wageni katika Jiji la Durban nchini Afrika Kusini.
Habari za uhakika zilizopatikana jana Jijini Dar es Salaam, zilieleza kuwa Watanzania hao, walirejea nchini jana alfajiri na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Precision Air.
Hata hivyo, jitihada za kumpata Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe hazikuzaa matunda lakini Naibu wake, Mahadhi Juma Maalim alithibitisha habari hizo.
“Ni kweli tumewarejesha Watanzania 26 waliwasili leo (jana) asubuhi kutoka Afrika Kusini na hii ilikuwa ni ahadi ya Serikali siku zote tunajali usalama wa raia wetu popote walipo,” alisema Maalim.
Hivi karibuni, Waziri Membe alisema kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kuwarudisha Watanzania hao baada ya kutokea machafuko hayo kwa wenyeji kuwapiga na kuwaua wageni kwa kile walichodai ‘kuwaminya’ kwenye ajira zao.
Habari zaidi zilisema Watanzania hao walisafiri kwa ndege kutoka Durban juzi usiku hadi Pretoria na usiku huo huo, wote wakafanikiwa kupata nafasi kwenye ndege ya Precision na kurejea nchini jana.
Wiki iliyopita, Membe alisema Watanzania 23 waliokuwa wamewekwa kwenye kambi maalumu ya Isipingo nchini Afrika Kusini ili kupewa ulinzi kutokana na mashambulizi yanayofanywa na wazawa.
Miongoni mwa Watanzania hao, 21 walikuwa wameridhia kurejea nyumbani na wanatarajia kuwasili nchini muda wowote lakini wengine wawili waliomba kuendelea kubaki nchini humo.
Membe alitumia mkutano huo kukanusha taarifa kuwa wapo Watanzania waliofariki nchini humo kutokana na vurugu hizo akisema watanzania waliofariki, walikufa kwa sababu mbalimbali.
Hata hivyo taarifa hizo zimekuwa zikipingwa kupitia baadhi ya Redio na mitandao ya kijamii hapa nchini, huku Redio moja ikimkariri mtanzania mmoja akidai alishuhudia watanzania wanne wakifa

Dk. Augusine adai anashawishiwa ili agombe Urais

Balozi wa zamani wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), Dk Augustine Mahiga amesema anafuatwa na makundi ya watu wanaomshawishi achukue fomu kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CCM, lakini hajatoa jibu.
Balozi Mahiga anaingia kwenye orodha ya watu ambao wamejitangaza au wanatajwa kuwania nafasi hiyo ya juu kwenye siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba utakaochagua Serikali ya Awamu ya Tano.
Tayari makada 21 wa chama chake wanatajwa kuwamo kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa miaka 10 baada ya kuongoza nchi kwa vipindi viwili, ambavyo ndio kikomo kwa mujibu wa Katiba.
Tayari makada 21 wa chama chake wanatajwa kuwamo kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa miaka 10 baada ya kuongoza nchi kwa vipindi viwili, ambavyo ndio kikomo kwa mujibu wa Katiba.
Dk Mahiga,(pichani) ambaye pia alikuwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia, alisema makundi hayo yalianza kumfuata baada ya Rais Kikwete kutangaza kwenye sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika Songea kuwa kama wanachama wanaona kuna mtu anafaa kugombea urais na hajajitokeza, wamfuate na kumshauri achukue fomu.
“Nimepata makundi ya watu na mtu mmoja mmoja wakinishauri  nichukue fomu ya kuwania urais baada ya Rais Kikwete kutoa kauli kule Songea mkoani Ruvuma, lakini bado sijakubali wala kukataa ushawishi huo,” alisema mwanadiplomasia huyo alipoongea na Mwananchi mara baada ya kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga iliyopo Iringa.
Lakini akaongeza kuwa kushawishiwa kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo nyeti kwa Taifa, ni jambo moja, lakini kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni jambo jingine akisema kuwa CCM ina mchakato na masharti ambayo ni lazima yatimizwe.
Hata hivyo, Dk Mahiga hakusita kumwaga sera zake iwapo atajitosa kuwania nafasi hiyo na kuchaguliwa kuongoza nchi.
“Nitaimarisha demokrasia, kuongeza uwajibikaji, kuimarisha maadili, kuboresha mwelekeo wa uchumi, kilimo, kuimarisha reli na kupambana na rushwa,” alisema balozi huyo ambaye ni mhitimu wa shahada ya umahiri ya sanaa.
Kuhusu sifa za mgombea urais, Dk Mahiga alisema ni vema Rais ajaye akawa na sifa zinazoenea na kuelezeka ili kuweza kupokea kijiti kutoka kwa Rais Kikwete wa sasa na kulipeleka mbele Taifa katika kipindi cha miaka mitano mingine. Alisema Rais ajaye anatakiwa kuwa kiongozi wa watu, aliye tayari kujifunza, kuchukua uamuzi mgumu, uwezo wa kutawala hasira na kuwa na marafiki.
Pia alisema anatakiwa kuwa na uwezo wa kutatua changamoto ambazo hazijaweza kutatuliwa kwa sasa ikiwemo ya ugaidi.
Nyingine ni kuwaunganisha Watanzania kuwa kitu kimoja, muadilifu na mwenye mtazamo wa mbali kwa Watanzania na Taifa, kuhimili mfadhaiko, awe mchapakazi, subira ya kupima mambo na kuwa juu ya yote kama hasira, wivu na fitina.

Akizungumzia hali ilivyo kwa sasa katika mbio za kuelekea Ikulu, Dk Mahiga alisema kumekuwepo na hali ya wanaowania nafasi ya urais kutumia fedha na kuonya kuwa suala hilo linaweza kulifikisha Taifa mahali pabaya kwa kumpata mtu asiyestahili.
Dk Mahiga aliwahi kuongea na Mwananchi wakati wa mchakato wa Katiba akielezea msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano.
Dk Mahiga alisema wakati huo kuwa suala la muundo wa serikali tatu kwenye Muungano limekuja wakati muafaka kwa kuwa umekuwa ukilalamikiwa na wananchi wa pande zote kwa muda mrefu na kwamba Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Kamati ya Mabadiliko iliyokuwea chini ya Jaji Joseph warioba ilikuwa na jibu la kero za Muungano.
Dk. Mahiga pia amepata kuwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Liberia wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati akifanya kazi ya kuongoza shughuli za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UN (UNHCR).
Akiwa balozi wa kudumu UN, Balozi Mahiga alisifika kwa kurejesha heshima ya heshima ya nchi kiasi cha kuwa mojawapo ya zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Katika kipindi cha kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1983, Mahiga alikuwa kaimu mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, nafasi ambayo ilimpa fursa ya kuifahamu Tanzania nje na ndani.
Dk Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945, ameoa na ana watoto watatu.
Alihitimu shahada yake ya sanaa mwaka 1971 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na shahada yake ya uzamili aliipata Chuo Kikuu cha Toronto. Alipata shahada yake ya uzamivu katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa kwenye Chuo Kikuu cha U of T mwaka 1975.

maelfu ya wananchi Nepoliwalala nje

Watu walala nje Nepal

Maelfu ya watu nchini Nepal wamelala nje usiku kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo jana Jumamosi ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa na kupotea kwa maisha.
Wakazi wa mji wa kathmandu walisema kuwa hawangerudi manyumbani mwao kutokana na hofu ya kutokea kwa mitetemeko zaidi.
Serikali ya Nepal inasema inaamini kuwa takriban watu 1500 wameaga dunia lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati makundi ya uokoaji yanapotafuta kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Hali mbaya ya hewa inalikumba eneo hilo na watoa huduma za dharura wanasema kuwa huenda ikavuruga jitihada za uokoaji.

Chadema yajipanga kuifanyia kufuru CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimeweka mkakati utakaowafanya makada wake wavamie majimbo yanayoshikiliwa mapema na CCM, huku wakichelea kuingia kwenye majimbo yaliyo chini ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini hapa, mkutano ambao ulifurika maelfu ya watu.
Mbowe alitangaza kupiga marufuku wanachama wa Chadema kuanza kutangaza nia kwenye majimbo ambayo wenzao wanayashikilia hadi hapo Bunge la Jamhuri ya Muungano litakapovunjwa.
Lakini alisema wanachama wa Chadema wanaruhusiwa kuanza purukushani kwenye majimbo ambayo yanashikilia na vyama vingine hasa chama tawala cha CCM ambacho kinashikilia majimbo mengi.
“Naomba ifahamike Chadema ni zaidi ya ubunge, tunahitaji amani na siyo kuharibu chama. Chadema itasimamisha watu makini kwenye maeneo yote katika uchaguzi huu,” alisema mwenyekiti huyo ambaye yuko kwenye ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mbowe ambaye hakugusia suala la Ukawa katika mkutano huo, alisema kuwa utaratibu utaandaliwa wa kupata wagombea na kwamba hata waliokuwa wabunge, wasijihakikishie kuwa watapitishwa tena kwenye maeneo yao wanayoyaongoza sasa.
“Tutakuja na utaratibu mwingine. Hata wabunge wa Chadema waliokuwa katika maeneo hayo, wasidhani kwamba watabakia hapo. Tutasimamisha mtu anayekubalika na watu wote, na utaratibu ukiwekwa, hata aliyekuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema Mbowe.
Alisema kuwa Chadema inaamini kuwa katika kila eneo kuna mtu wake ambaye ni makini na ni wazi atashinda.
Vyama vinne vya upinzani, Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia kwenye uchaguzi wa madiwani hadi rais. Vyama hivyo, vilivyo chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimekubaliana kuwa kila chama kipate mgombea wake na baadaye vitachambua anayekubalika na wengi.
Ainanga Nec
Akizungumzia mwenendo wa uboreshaji wa Daftari la Wapigakura, Mbowe alisema Taifa kwa sasa liko kwenye giza nene kutokana na maandalizi mabovu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec).
Mbowe alisema kucheleweshwa kwa kazi ya uandikishaji wapigakura ni sehemu ya njama za CCM kupitia Serikali yake inayotamani kutumia nafasi hiyo ili kuendelea na hujuma katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Mbowe, ambaye aligombea urais mwaka 2005, alisema Nec inachelewesha kazi hiyo ili kuibeba CCM katika uchaguzi mkuu kwani kukamilika kwa daftari hilo kunaonekana kunaitia hofu CCM.
“Kuna wananchi wengi, zaidi ya milioni 26 wanatakiwa kuandikishwa na muda uliobakia ni mfupi. Walichelewesha kwa makusudi ili kuisaidia CCM iendelee kututawala kwa nguvu ya watu wachache watakaokuwa na sifa za kupiga kura, “ alisema.
“Kwa njama hizo, tunamuomba Rais (Jakaya) Kikwete amalizie muda wake kwa amani na asituharibie amani ya nchi yetu kwa kutengeneza hujuma. Bora amalize muda wake ili akapumzike kijijini kwao.”
Mbowe alisema mpaka sasa Rais Kikwete ndiye wa kulaumiwa kwa maandalizi hayo ya Uchaguzi Mkuu kutokana na dalili zinazoonekana kwa sasa.
“Kampeni ni siku 72 kabla ya Uchaguzi Mkuu na mpaka sasa ni miezi mitatu tu imebakia kabla ya kuanza kampeni, lakini hakuna dalili za maandalizi yoyote. Haya yote yamechangiwa na Serikali yenye maandalizi mabovu,” alisema Mbowe.
Mbowe pia alishangazwa na kitendo cha Serikali kutumia fedha nyingi katika mchakato wa Katiba bila mafanikio yoyote yale, lakini hakuna kiongozi aliyewajibishwa kwa hasara hiyo.
Katika hatua nyingine, Mbowe alifafanua kuhusu urais nafasi ya urais kupitia Ukawa akisema, kwa sasa lengo lao kwa pamoja siyo bora kupata urais, bali ni kuangalia kiongozi gani atakayesimama kuwakilisha Ukawa katika nafasi hiyo.
“Kwa hivyo CCM na watu wengine wasidhani kwamba Ukawa tutagombana kwa sababu hiyo, tumejipanga na dhamira yetu ndiyo nguvu ya Watanzania walioridhia kuungana kwetu. Tunaamini CCM lazima ing’oke katika uchaguzi huu,” alisema Mbowe.
Katika hatua nyingine, Mbowe pia aliwaonya baadhi ya wanasiasa wanaounda Ukawa, kuanza kutangaza nia kwenye majimbo yenye wabunge kwa sasa. Alisema nafasi hiyo ya kutangaza nia itapatikana baada ya Bunge kuvunjwa.
Mafunzo ya FP200
Akizungumzia mkakati wa kutoa mafunzo kwa vijana wa chama hicho FP200, Mbowe alisema kuwa hata kama IGP ataweka pingamizi, lazima watatekeleza azimio hilo. Alisema IGP, akitaka kuwakachukulia hatua basi, yeye atakuwa muhusika namba moja.
“Hata Jeshi la Polisi wakizuiua lazima mafunzo yatafanyika na kama wanataka kuchukua hatua basi Mbowe akamatwe,” alisema Mbowe.

Saturday 25 April 2015

Wenger na mourinho waendelea kutupiana maneno

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango lake.
Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.
Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.

Ng'ombe amla kondoo huko kenya

Ng'ombe anayewala Kondoo Kenya


Mkulima mmoja nchi Kenya anasema kuwa mmoja wa ng'ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo.
Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba kusini magharibi mwa kaunti ya Nakuru aligundua kuwa ng'ombe wake amemla kondoo siku moja asubuhi.
Jitihada zake za kumpa ng'ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng'ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo ni kuwa , huenda tabia ya ng'ombe huyo imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana katika mimea mibichi.
Hali ya kiangazi ambayo ilimalizika hivi majuzi huenda imesababisha mifugo kukosa madini yanayopatikana kwenye nyasi mbichi. Mwaka 2007 ndama mmoja nchini India alinaswa kwenye mkanda wa video akila kuku.

Thursday 23 April 2015

Marekani yajiimarisha Bahari ya Arabuni

Meli ya kivita ya Marekani USS Theodore Roosevelt.
Marekani imethibitisha inazifuatilia meli za Iran zinazoshukiwa kuwa zimechukuwa silaha kuwapelekea waasi wa Kihouthi nchini Yemen wakati ikiimarisha uwepo wake kijeshi katika Bahari ya Arabuni.
Meli ya kivita ya Marekani USS Theodore Roosevelt.
Jeshi la majini la Marekani limepeleka meli yake ya kivita ya USS Theodore Roosevelt ikisindikizwa na meli yenye kubeba makombora ya USS Normandy kuhakikisha kile ilichosema njia muhimu za bahari katika eneo hilo zinabakia kuwa wazi na salama na kufanya idadi ya meli za kivita za Marekani katika eneo hili kufikia tisa.
Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa ulinzi wa Marekani ambaye amezungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP msafara wa meli za Iran unajumuisha meli tisa zikiwemo mashua mbili za doria lakini mahala hasa unakoelekea msafara huo hakujulikani.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Kanali Steven Warren amekanusha repoti kwamba meli za Marekani zimeagizwa kuzuwiya meli za Iran zenye kuwapelekea silaha Wahouthi.
Meli za Iran yumkini zikazuiliwa
Manowari ya Iran. Manowari ya Iran.
Marekani imesema haishiriki moja kwa moja katika mashambulizi ya anga ya ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kishia wa jamii ya Wahouthi nchini Yemen lakini inasaidia kwa kutowa taarifa za kijasusi na msaada wa vifaa.
Maafisa kadhaa wa serikali ya Marekani wamedokeza kwamba yumkini Saudi Arabia,Misri na washirika wao wengine ndio zitazozizuwiya meli hizo za Iran itakapolazimika.
Inasemekana kwamba msafara huo wa meli za Iran tayari umevuka mlango bahari wa Hormuz kuondoka Ghuba na hivi sasa unaelekea upande wa magharibi ambapo inaaminika kuwa Yemen.
Upatanishi wa Iran wagonga ukuta
Rais Hassan Rouhani wa Iran. Rais Hassan Rouhani wa Iran.
Rais Hassan Rouhani wa Iran leo ametowa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini Yemen na kukomeshwa kwa mashambulizi ya anga ya ushirika unaongozwa na Saudi Arabia ili kuwezesha kufanyika kwa mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana nchini humo.
Rais Rouhani amesema"Tunataraji kwamba kila mtu atazinduka na tunatumai pendekezo la Iran litatekelezwa.Ni kusitishwa kwa mapigano mara moja,kushughulikia hali ya majeruhi na kufanya mkutano baina ya Wayemen kutafuta suluhisho na hatimae kuunda serikali yenye kushirikisha makundi na makabila yote.Tunaamini kwamba huu ni ufumbuzi ambao unaweza kutatuwa masahibu ya Yemen."
Rais Rouhani ametowa kauli hiyo muda fupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mehrabad mjini Tehran kuelekea Indonesia kuhudhuria mkutano wa Kilele wa Asia na Afrika.
Dhima ya Iran
Moshi mzito ukifuka baada ya shambulio la ghala la silaha Sanaa. (20.04.2015) Moshi mzito ukifuka baada ya shambulio la ghala la silaha Sanaa. (20.04.2015)
Unyeti wa dhima ya Iran katika mzozo huo umezidi kujitokeza leo hii wakati serikali ya Yemen ilipokataa pendekezo la Iran la kusuluhisha mzozo huo.Waziri wa mambo ya je wa Yemen Riyadh Yassin amesema juhudi zozote zile za upatanishi kutoka Iran hazikubaliki kwa sababu Iran inahusika katika mzozo huo wa Yemen.
Amesema Wahouthi na vikosi vya Rais wa zamani Ali Abdullah Saleh lazima waondoke katika miji na vijiji vyote vya Yemen ikiwemo Sanaa na Aden na kurudi katika ngome yao kuu ya kaskazini ya mji wa Saada wakiwa kama raia na kusalimisha silaha zao.
Nchini Yemen kwenyewe mzozo huo hauonyeshi dalili ya kupowa wakati idadi ya vifo vya raia waliouwawa katika mashambulizi ya anga yanayongozwa na Saudi Arabia dhidi ya ghala la makombora mjini Sanaa hapo jana ikiongezeka na kufikia 38 huku watu 532 wakiwa wamejeruhiwa.

Timu maarufu sana Dunian hizi hapa

liverpoolLiverpool inaongoza uingereza,Arsenal na Chelsea zimegawana ulaya na Manchester united ni baba lao bala zima la asia.
Takwimu hizi zimetolelewa na mtandao wa kijamii wa twitter ambao umehusisha klabu 20 duniani,
Arsenal imeongoza  Amerika ya kaskazin Na ssehemu kubwa ya laya ikiwepo austaria yote.
Manchester united imefatwa na mashabiki wengi wanaotokea bara la asia wakat Chelsea ikiwa na nguvu zaidi bara la amerika kusini
Liverpool inaonekana kusuasua sana mwaka huu na hata kupoteza matumaini ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya lakini hilo hililipi tabu klabu hiyo yenye maskani yake pale Merseyside na kuwa klabu inayoongoza kuwa na mashabiki wengi uingereza.
Arsenal inawatu wengi hasa pale London ya kusini mashariki na kuwafanya wapinzani wake wa wa karibu kutoka jiji hilo Chelsea na tottenham kuwa wanawafukuza kwa mbali.
man utd
Katika jiji la  Manchester ,  Louis van Gaal ameongeza msisimko na kuongeza kutawala eneo mbali na Gorton ambapo wapinzani City ni maarufu zaidi.
 Chelsea imetupwa  nje ya London na Arsenal, na kwa  msaada wa nguvu visiwani vya Magharibi, wakati vilabu kama Newcastle, Sunderland, Hull City, Burnley, Stoke City, Leicester City, Aston Villa, Swansea na Southampton kutawala maeneo yao ya ndani.

Zuma awatembelea waathirika wa ghasia

Südafrika Präsident Jacob Zuma
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini amewaomba raia wa kigeni kubakia nchini humo wakati wakati akikatisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia kushughulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni.
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini
Wiki tatu za ghasia zinazoongezeka dhidi ya wageni nchini Afrika kusini zimesababisha kiasi watu sita kuuwawa na kuwalazimisha wahamiaji 5,000 kutafuta hifadhi katika makambi ya muda.
Machafuko hayo , ambayo yameanzia katika mji wa mashariki wa bandari wa Durban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, yanabeba ghasia za hisia za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika kusini mwaka 2008 wakati watu 62 walipouawa.
Xenophobie in SĂĽdafrika Raia wa Afrika kusini akishikilia bango linalosema "tupinge chuki dhidi ya wageni".
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, polisi jana Jumamosi(18.04.2015) wamesema wageni waliouwawa wamefariki kutokana na kuchomwa visu mjini Alexandra , mji ulioko kaskazini mwa Johannesburg. Eneo hilo linaloishi watu masikini limekuwa lengo ya ghasia nyingi katika siku hiyo, ambapo maafisa wa polisi walifyatua risasi za mipira kuwatawanya watu waliokuwa wakifanya uporaji.
Zaidi ya watu 30 wamekamatwa usiku ya Jumamosi kuzunguka mji wa Johannesburg pekee. Akiwa chini ya mbinyo kuzuwia kurudiwa mauaji yaliyotokea mwaka 2008, Zuma alisafiri kwenda Durban kutembelea kambi wanayohifadhiwa wageni waliokimbia makaazi yao kutokana na ghasia hizo, lakini alikabiliana na mapokezi yasiyokuwa mazuri kutoka kwa kundi lililomsubiri, ambalo lilipaaza sauti, "rudi nyumbani, rudi nyumbani" na umechelewa , umechelewa".
"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika kusini anasema , nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki dhidi ya wageni.
Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha ghasia wanakaribishwa kurejea, " Zuma amesema.
Gewalt gegen Ausländer in Südafrika geht weiter Mkaazi wa Afrika kusini akiwa na gongo na ngao tayari kwa mapambano na wageni
Zuma afuta ziara
Kiongozi huyo wa Afrika kusini alitarajiwa kusafiri kwenda Indonesia jana Jumamosi, lakini alitangaza kufuta ziara hiyo "kushughulikia suala hilo nyumbani linalohusiana na mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni."
Uamuzi huo umekuja wakati hali ya tahadhari inaongezeka nchini Afrika kusini---na kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na miji mingine mikubwa-- kuhusiana na mashambulio hayo.
Nchi jirani za Zimbabwe , Malawi na Msumbiji zimetangaza mipango ya kuwaondoa raia wake. Ikiakisi wasi wasi wa kimataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema wahanga wengi walioshambuliwa, "ni wakimbizi na wanaohitaji hifadhi ya kisiasa ambao wamelazimika kukimbia nchi zao kutokana na vita pamoja na kukamatwa."
Kinachoelekezewa kidole cha lawama kwa kiasi kikubwa kutokana na ghasia hizo ni hotuba mwezi uliopita iliyotolewa na mfalme Goodwill Zwelithini, kiongozi wa kabila la Wazulu, ambapo amewalaumu wageni kutokana na kiwango cha juu cha uhalifu nchini Afrika kusini na kusema ni lazima"wafunge virago na kuondoka".
SĂĽdafrika Fremdenfeindliche Ausschreitungen Mhamiaji akikimbia wakati polisi akijaribu kuzuwia ghasia hizo
Mfalme huyo amekuwa akisema maneno yake yametafsiriwa vibaya.
Wakati mzozo huo ukiendelea, Zuma ameyataka makanisa yote kufanya sala maalum kwa ajili ya amani na urafiki leo Jumapili.
"Tunafahamu kwamba wengi wa watu wetu wanaamini kuhusu haki za binadamu na amani na kwamba wanaheshimu utu wa kila mtu anayeishi katika nchi hii," amesema katika taarifa iliyotolewa jana Jumamosi.
"Wanafahamu kwamba mahali palipo na hali ya wasi wasi na tofauti, haya yanaweza kutatuliwa kwa njia ya Afrika kusini, kupitia majadiliano, na sio kupitia ghasia na ukandamizaji."
Hasira miongoni mwa mataifa jirani na Afrika kusini
Ghasia hizo zimezusha hasira katika mataifa mengine ya Afrika.
SĂĽdafrika Fremdenfeindliche Ausschreitungen Nchini Msumbiji kundi la watu wapatao 200 siku ya Ijumaa lilizuwia kivuko cha kusini kati ya nchi hizo cha Lebombo, wakirusha mawe dhidi ya magari ya Afrika kusini.
Kundi la raia wa kigeni likijaribu kujilinda
Nchini Zambia , redio inayomilikiwa na mtu binafsi ilisitisha kupiga muziki wa Afrika kusini katika hatua ya kupinga mashambulizi hayo dhidi ya wageni. Na katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, waandamanaji walifika katika ubalozi wa Afrika kusini kulaani kile walichokiita "mauaji ya kiwendawazimu na ya kikatili" dhidi ya Waafrika wenzao.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amelaani ghasia hizo siku ya Jumamosi, akielezea "hali ya kushitushwa na kuchukizwa".

Manchester kumchukua Hammels kwa paund milion 30

over

Manchester United imeshaanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao baada ya msimu huu kuelekea mwishoni. Kiasi cha €30 million zimetengwa kwa ajili ya kumnasa mkali huyu.


Kwa muda sasa hivi Man United wamekua imehusishwa na uhamisho wa Hummels. Hummels ambae alionekana kuwa ni defender bora kwenye kombe la dunia anaonekana ni mmoja kati ya mastaa wanatarajiwa kusepa Borussia Dortmund.


Kutokana na kocha Jurgen Klopp kutangaza kusepa mwishoni mwa msimu huu basi kuna mwanya mkubwa wa mastaa wa timu hiyo kusepa pia.


Kiasi cha €30 million kimetolewa kama offer ya kwanza kumnasa Mats Hummeles ana miaka 26, amecheza mechi 181 tangu asajiliwe rasmi na Borussia na amefunga magoli 16 akicheza nafasi ya Center defender.

Ajali nyingine shinyanga yaua 10 na 50 kujeruhiwa

Polisi wakiwa katika eneo la Ajali
Jinamizi la ajali za barabarani zikihusisha mabasi zimeendelea kugharimu maisha ya Watanzania baada ya jana watu 10 kupoteza maisha na wengine 50 kujeruhiwa vibaya wakati basi la Unique Express lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora kugongana uso kwa uso na lori la Coca-Cola lililokuwa likitokea Tinde kuelekea Shinyanga.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 8.45 mchana katika Kijiji cha Ibingo, Kata ya Samuye, Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi uliosababisha dereva wake kushindwa kulikwepa lori hilo lililokuwa katikati ya barabara.
Alisema watu tisa walifariki dunia papohapo na mmoja alifia katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga akipatiwa matibabu.
Kamanda Kamugisha alisema dereva wa lori anashikiliwa na polisi mwenzake wa basi hali yake ni mbaya na amelazwa hospitali.
Alisema wengi waliofariki dunia walikuwa wamekandamizwa na vyuma hali iliyowalazimu kuomba msaada wa winchi kuliinua basi hilo na kuwatoa.
Kamanda Kamugisha aliwataka wananchi na abiria kutoa taarifa pindi wanapoona madereva wakiendesha mwendo ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwamo Diwani wa Kata ya Samuye, Amos Shija walisema walishtushwa na kishindo cha kugongana kilichofuatiwa na kelele na vilio vya abiria.
Shuhuda, John Bundala aliitaka Serikali kuendelea kuwachukulia hatua kali madereva ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani na kupoteza maisha ya watu wasiokuwa na hatia na wengine kupata ulemavu.

Timu Nne zatinga nusu fainali UEFA

Javier Hernandez akishangilia goli mbele ya mashabiki wa Real Madrid
Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.
Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.