Wednesday 29 April 2015

Rais kikwete azindua Meli kubwa za kivita yenye ukubwa wa mita 60

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini ambazo zitakazowezesha usalama wa uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.
Mara baada ya uzinduzi Rais. Kikwete amezikabidhi kwa kamandi ya jeshi la wanamaji hafla iliyofanyika makao makuu ya kamandi hiyo yaliyopo kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema meli hizo zinafanya Tanzania iandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za kisasa kwa mara ya kwanza nchini.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,Dk.Hussein Mwinyi, amesema, meli hizo zitakuwa tegemeo kubwa katika kulinda eneo la maji ya tanzania na rasilimali zake ikiwamo gesi asililia,samaki kwani zina uwezo wa kasi kubwa katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hasa uharamia.
 
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema,lengo la kuwa na meli za jinsi hiyo ni katika jitihada za kuhakikisha jeshi linakuwa na silaha za kisasa za kivita na kutoa mafunzo huku balozi wa china nchini, Lui Youging, akimpongeza Rais Kikwete kwa jitihada za kuimarisha ulinzi wa taifa lake.
 
Meli hizo zimepewa majina ya melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na  melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete ambaye anatarajia kumaliza kipindi chake cha uongozi Novemba mwaka huu.

No comments: