Wednesday 25 January 2017

MAHAKAMA YAFUTA MASHTAKA YA KUBENEA

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyaondoa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (46).
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, leo ameyaondoa mashtaka hayo mahakamani hapo kwa sababu hati ya mashtaka ilikuwa na utata na aiendani na kifungu cha 132 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema kifungu hicho cha sheria kinataka kosa lielezwe kwa uwazi ' kinaga ubaga'.
Alisema katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Kubenea ya kusambaza habari ya uongo yenye kichwa cha habari 'yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar' ambayo ingeweza kuleta uvunjifu wa amani, Hakimu Mashauri alisema maneno hayo pekee kisheria siyo kosa.
Akiendelea kutoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema upande wa mashtaka ulishindwa kueleza maneno yenyewe hasa ya uchochezi yenye lengo la uvunjifu wa amani.
Hivyo, Hakimu Mashauri aliiondoa kesi hiyo mahakamani hapo na mshtakiwa akaachiwa huru na kwamba upande wa mashtaka unaweza kumshtaki upya.
Hata hivyo baada ya Kubenea kuachiwa huru alikamatwa na kupelekwa polisi kati na baadaye akaachiwa kwa dhamana.

TRUMP AZIDI KUSAINI SHERIA MATATA.,SASA WAHAMIAJI MARUFUKU KUINGIA MAREKANI*

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini amri kuu kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.
Taarifa kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani baadaye Jumatano.
Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi
Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.

Tuesday 24 January 2017

Bombadier ya ATCL yatua Mwanza baada ya kupata dharura Mwanza

Ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikitoka Mwanza kwenda Dar es salaam jana ililazimika kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza dakika ishirini baada ya kuanza safari yake. Ndege hiyo iliyoruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kwa safari ya kuelekea Dar es salaam saa mbili asubuhi, ililazimika kutua kwa dharura uwanjani hapo dakika 20 baadae kwa ajili ya kurekebisha dharura ambayo mpaka muda huo ilikuwa haijafahamika. Rubani aliwataarifu abiria kuwa wanalazimika kutua uwanjani hapo kwa sababu ya dharura iliyojitokeza. Baada ya wataalamu kuikagua ndege hiyo waligundua kuwa mlango wa sehemu ya kuwekea mizigo haikufungwa kitukilichopelekea taa ya kuashiria hatari kuwaka na kumlazimu rubani wa ndege hiyo kulazimika kutua kwa dharura.

Ajali mbaya aua mtu mmoja Iringa

MTU mmoja amefariki dunia katika ajali ya basi la kampuni ya Vitu Laini lenye namba za usajili T910 linalofanya safari zake kati ya Lulanzi Kilolo na Iringa Mjini baada ya kuligonga lori lenye namba T724 AVV scania lililokuwa limebeba Mbao.
Ajali hiyo imetokea asubuhi leo hii eneo la Tagamenda Mjini Iringa wakati basi hilo likitokea Kilolo kwenda Iringa mjini na kuelekea mwelekeo wa Lori hilo.
Chanzo kimeel
ezwa ni mwendo kasi wa basi hilo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amefika eneo La tukio pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama.

Dani Alves ameingia kwenye rada za klabu TATU za China huku Shanghai SIPG ya Andre Villas-Boas ikiongoza mbio hizo


Klabu tatu za Ligi Kuu ya China zimeripotiwa kuitamani saini ya beki wa Juventus Dani Alves.
Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas ambaye kwa sasa anainoa Shanghai SIPG anaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania saini ya nyota huyo wa anayekipiga Serie A.
France Football kimeripoti kuwa Villas-Boas wa SIPG yupo tayari kumlipa Mbrazili huyo kitita cha paundi 165,000 kwa wiki kumtoa Serie A kutua kwenye ligi hiyo ya matajiri wa Mashariki ya Mbali.
Alves alitua Turin majira ya joto baada ya kuitumikia Barcelona kwa kipindi cha miaka nane, lakini ametokea kuzivutia klabu za Asia.

Wafungwa zaidi a 300 waachiliwa huru Bujumbura

Wafungwa zaidi ya 300 wameachiliwa huru hii leo kwenye jela kuu ya Mpimba Bujumbura, likiwa ni zoezi la kupunguza msongamano katika magereza mbali mbali nchini humo. Hatua hiyo ni katika utekelezaji wa msamaha wa rais Pierre Nkurunziza. Miongoni mwa walioachiwa huru ni pamoja na wale waliopatikana na hatia ya kujihusisha na vugu vugu la kupinga muhula wa 3 kwa rais huyo. Kuachiliwa wafungwa hao pia ni moja ya vigezo vilivyoowekwa na Umoja wa Ulaya ili irudi kuisaidia kifedha Burundi.

Sunday 22 January 2017

MKUU WA WILAYA YA HAI AZUIA SHAMBA LA MBOWE*

mwenyekiti wa Chadema Freeman mbowe akiwa anakagua shamba lake
MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gellasius Byakanwa, amesitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe, kutokana na kile alichosema kuwa shamba hilo lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.
Byakanwa alitoa amri hiyo jana baada ya kutembelea shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara na kukuta shughuli za kilimo zikifanyika.
Alisema Mbunge huyo pia alifanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kulingana na maamuzi ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.
“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (jana) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.

Tuesday 17 January 2017

Mtoto aliyezikwa afufuka



MBEYA: Mtoto aliyezikwa jana akutwa chumbani kwake mara baada ya mazishi
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea  .

Matokeo ya kidato cha pili haya hapa


BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016/17

Wednesday 11 January 2017

POLISI WAKAMATA NOTI BANDI ZENYE THAMANI YA SH MIL 8 MKOANI TABORA

Polisi wilayani Igunga mkoni Tabora wamewakamata watu watatu wakiwa na noti bandia za shilingi 10,000 zipatazo mia nane sawa na shilingi milioni nane wakiwa wamezihifadhi kwenye buti ya gari yao ndogo
Watuhumiwa waliokamatwa na noti hizo ni  Luneka Magasha 35) mkazi wa Igunga, Zengo Magasha (25) mkazi wa mkoa wa Lindi na James Hangalu  mkazi wa Dar es salaam
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Hamisi Selemani alithibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema kuwa polisi walipata taarifa ya kuwepo kwa watu wenye noti za bandia na baada ya taarifa hiyo walikwenda eneo la tukio na kuwakuta watu hao waikiwa na gari ndogo yenye namba za usajili  T 964 BEC

Wednesday 4 January 2017

Jeshi la polisi Dar lafanikiwa kuua majambazi wawili

Jeshi la Polisi kanda ya Dar Es Salam lafanikiwa kupambana na majambazi na kuuwa wawili. Tukio hilo limetokea maeneo ya mikocheni karibu na shule ya sekondari Feza Boy.
inasadikika kuwa majambazi hao walitaka kumvamia raia wa China ambaye jina lake tumeshindwa kulipata

Kati ya hao majambazi , jambazi mmoja jinsia ya kike ambae ndiye alikuwa dereva wa gari la majambazi hao amejisalimisha mikononi mwa jeshi la polisi.
jeshi la polisi bado linasaka majambazi wengine.
 Kwa taarifa tulizozipata jeshi la polisi kwakutumia intelejinsi yao ilifanyamsako takribani wiki nzima hadi kufanikiwa kuwapata majambazi hao.