Maafisa wa polisi nchini Tanzania
Polisi nchini
Tanzania wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia
Jumanne wiki hii hadi hali ya usalama itakapotulia
Katika taarifa
iliotumwa katika vyombo vya habari walinda usalama hao wamewataka
wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za
nchi.
Taarifa hiyo imesema kuwa polisi hawatasita kumchukulia
hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa
kitakachokaidi agizo hilo.
Aidha maafisa hao wamewataka wananchi
kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na
badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa
taifa la Tanzania.
Polisi nchini Tanzania imeripoti kupokea
taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya kisiasa vikitaka kufanya mikutano
na maandamano .
Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao
mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la
kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
CHANZO: BBC