Monday 30 November 2015

Sheikh Ponda aachiwa huru

Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

Friday 27 November 2015

Mganga atupwa rumande kwa kushindwa kufufua maiti

Mkazi  wa Dar es Salaam, Dunia Salumu maarufu kwa jina la Dk. Manyaunyau, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha Sh milioni 29.6 kwa njia ya udanganyifu.

Manyaunyau anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mlalamikaji, Tekra Modesta kama malipo ya kazi ya kumfufua marehemu kaka yake aliyefahamika kwa jina moja la Modest ambaye alifariki dunia miaka kadhaa iliyopita.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Flora Haule, alisema mtuhumiwa huyo ametiwa hatiani baada ya ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka kujitosheleza.

Ndoa za utotoni zaongezeka barani Afrika

Msichana mmoja kutoka NigeriaIngawa ni kinyume cha sheria kuoza wasichana walio chini ya umri katika nchi nyingi za Afrika, lakini waatalamu wanasema utekelezaji wa sheria hizo hauna nguvu na mila ya kale kuelekea wasichana na wanawage ingali na nguvu.

 Takwimu mpya zinaonyesha viwango vya kushtusha vya kuongezeka kwa ndoa za utotoni barani Afrika, na kusababisha waatalamu kukutana pamoja nchini Zambia kujadili namna ya kukomesha mila hiyi.
Ingawa ni kinyume cha sheria kuoza wasichana walio chini ya umri katika nchi nyingi za Afrika, lakini waatalamu wanasema utekelezaji wa sheria hizo hauna nguvu na mila ya kale kuelekea wasichana na wanawage ingali na nguvu.
Idadi ya watu barani Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa  mara mbili miaka 35 ijayo, na iwapo mwenendo wa sasa hautabadilika, basi hata idadi ya wasichana watakaoozwa itaongezeka vivyo hivyo, na kufikia milioni 310.

Wizara ya ulinzi ya China yaidhinisha mpango wa kuunda kambi ya jeshi nchini Djibouti

China kuunda kambi ya jeshi nchini DjiboutiWizara ya ulinzi ya China yaidhinisha mpango wa kuunda kambi ya jeshi nchini Djibouti

Wizara ya ulinzi ya China imetangaza kuidhinishwa kwa mpango wa kuunda kambi ya jeshi katika nchi ya Djibouti.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Chien, alifahamisha lengo la kuundwa kwa kambi hiyo kuwa ni kusaidiana na UN kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo ya Somalia na Ghuba ya Aden.
Wu aliongezea kusema kwamba kambi hiyo pia itasaidia kurahisisha harakati za vikosi vya kulinda amani katika kanda hiyo.

Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa moja mjini New York Marekani

Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa moja mjini New York Marekani
Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Yesu Kristu alizaliwa kwenye hori mjini Bethlehem.
Na katika tukio ambalo ni linafanana na hilo mtoto mdogo ambaye alikuwa kwenye hori amepatikana ndani ya kanisa moja mjini New York.
Inaaminika kuwa mtoto huyo mchanga ambaye ni mvulana aliachwa na mama yake, katika eneo takatifu la kanisa hilo siku ya Jumatatu jioni.
Mtoto huyo alipatikana na padre Christopher Heanue anayesimamia kanisa hilo.
Padre huyo amesema alishangazwa sana na tukio hilo ila alijawa na huruma nyingi.
Amesema kanisa ni mahala ambako watu wanaohitaji misaada na makao huenda na kwa kuwa papa Francis amekuwa akihubiri na kuhimiza waumini wote wawe na huruma, na zaidi ya yote mwaka huu ni mwaka wa huruma, amefarajika sana kuumpa mvulana huyo matumaini na mahala pa kuishi kwa kuwa anahitaji huruma na malezi.

Thursday 26 November 2015

Man U yajiweka pabaya kusonga mbele UEFA

Man U vs PSV
Kikosi cha Manchester United bado kipo kwenye wakati mgumu kuhakikisha kinafuzu hatua ya mtoano ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kufuatia ulazimishwa sare ya bila kufungana na ya timu ya PSV kwenye uwanja wa Old Trafford mchezo uliopigwa usiku wa Jumatano November 25, 2015.
Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa upande wa United ambao walitawala mchezo huo kwa kila idara lakini hawakufanikiwa kutumbukiza mpirakwenye nyavu za wapinzani wao.
Jesse Lingard alipana nafasi nzuri ya kufunga  lakini mpira ukagonga mwamba huku shuti la Morgan Schneiderlin likiokolewa.

Bunge la Uingereza la jadili kuhairishwa kwa uchaguzi Zanzibar

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/11/mtz14.jpgHALI ya kisiasa na kufutwa kwa uchaguzi wa urais pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar hatimaye imetua na kujadiliwa katika Bunge la mabwanyenye la nchini Uingereza.
Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya wapinzani wawili wa kisiasa visiwani humo, Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa Kwanza ambaye pia alikuwa mgombea wa urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuendelea na vikao vya siri vinavyoshirikisha marais wastaafu wa Zanzibar.
Sakata hilo liliibuka jana nchini Uingereza katika kikao cha Bunge ambapo mbunge Lord Steel wa Aikwood kutoka Chama cha Liberal Democrat, alitaka kujua tathmini ya Serikali ya Uingereza kuhusu uchaguzi nchini Tanzania, hasa ule wa Zanzibar na kilichoelezwa kwa Serikali ya Tanzania au Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola kuhusu uchaguzi huo.

Didier Drogba ataka Ukocha chelsea

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.
Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.
Drogba, ambaye kwa sasa anasakata soka ya kulipwa huko Canada, aliifungia the Blues mabao 164 katika enzi yake huko Stamford Bridge.
"Ningependa kuihudumia klabu hiyo hata baada ya kukamilika kwa kipindi changu cha uchezaji''
''Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa mkufunzi kwa sababu klabu hiyo ilinifaa sana nilipoanza'',alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 37.
''Kwani siwezi kuwa meneja ? kwani siwezi kuwa mkurugenzi wa kiufundi,mkufunzi wa chuo cha mafunzo ya wachezaji ama hata mshauri wa washambuliaji ?

Wednesday 25 November 2015

Rubani wa Urusi aokolewa Syria

Rubani wa Urusi aokolewa Syria
Urusi inasema kuwa msaidizi wa rubani wa ndege ya kijeshi iliyodunguliwa na Uturuki hapo jana ameokolewa na kurejeshwa katika kambi yao ya kijeshi iliyoo Syria.
Urusi inasema kuwa afisa huyo yuko katika hali njema katika kambi ya kijeshi ya Lattakia.
Wizara ya ulinzi nchini Urusi inasema kuwa rubani mwingine na mwanajeshi aliyeshiriki katika operesheni ya kwenda kuwaokoa marubani hao wa ndege iliyodunguliwa nao waliuawa.
 
Ubalozi wa Urusi na taarifa kutoka kwa serikali ya Syria zinasema kuwa rubani huyo aliokolewa na wanajeshi wa Syria
Ubalozi wa Urusi na taarifa kutoka kwa serikali ya Syria zinasema kuwa rubani huyo aliokolewa na wanajeshi wa Syria na anarudishwa kwenye kambi ya jeshi la urusi eneo la Lattakia huko Syria.
Moscow inasema kuwa operesheni nchini Syria zitaendelea kuwakabili wapiganaji wa Islamic State na makundi mengine ya kijihadi.
Aidha Urusi imesema kuanzia leo ndege zinazoelekea kutekeleza operesheni za mashambulizi dhidi ya makundi ya kijihadi zitapewa ulinzi mkali na ndege za kivita.
Vilevile mitambo ya rada ya Urusi itatumika kuimarisha ulinzi wa angani katika maeneo ya mipakanai ya Syria.
Mitambo ya rada ya Urusi itatumika kuimarisha ulinzi wa angani katika maeneo ya mipakanai ya Syria.
Mitambo hiyo itawekwa katika kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Lattakia.
Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.
Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.

Kilimanjaro stars yapaa , Zanziber Heros yabanwa

Michuanao ya Cecafa Chalenji Cup Imeendelea tena jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi.
Zanzibar ilifungwa bao 4-0 na Uganda ikiwa ni Mechi ya Kundi B.
Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na Pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali.

Barcelona washusha mvua ya magoli kwa As Roma

Barcelona wakiwa nyumbani walichomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya As Roma.
Buyen Munich wakiichapa Olympiakos bao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakila hio kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0.
BATE Borislov wakifungana bao 1-1 na Buyer Liverkusen , FC Porto wakilala bao 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia bao 2 – 0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.
Michuano hiyo inatarajia kuendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa.
Miongoni mwa mechi hizo ni Man United dhdi ya PSV Eindhoven, Atletico Madrid na Galatasaray, Juventus dhidi ya Man City na Shakhtar Donetsk watawaalika Real Madrid.

Tuesday 24 November 2015

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake

Tahadhari ya kusafiri na mashambulio ya kigaidi
Serikali ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo inasema taarifa zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State, al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake

Tahadhari ya kusafiri na mashambulio ya kigaidi
Serikali ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo inasema taarifa zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State, al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.

Monday 23 November 2015

Said Kubenea kumburuza Spika wa bunge Job Ndugai Mahakamani


Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema atamfikisha mahakamani Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kuvunja kanuni baada ya kuwaingiza polisi ndani ya ukumbi wa chombo hicho.

Polisi hao waliingia ndani ya ukumbi huo wiki iliyopita wakati Rais John Magufuli alipofika kwa ajili ya kuhutubia Bunge.

Kubenea alisema kitendo cha askari kuingia ndani ya Bunge kwa mara ya mwisho kilitokea nchini Uingereza mwaka 1930 na hakijawahi kutokea tena isipokuwa nchini.

ZINEDINE ZIDANE AMESEMA HIVI KUHUSU YEYE KUCHUKUA NAFASI YA RAFAEL BENITEZ

1622E2AB000005DC-0-image-a-22_1448238461341
Baada ya mechi ya El Classico zikavuma tetesi kwamba Zinedine Zidane anatakiwa kuchukua nafasi ya Rafael Benitez kwenye club ya Real Madrid.
Tetesi hizo zilipewa kasi baada ya mchezaji wa Brazil Rivaldo ku-post kwenye instagram yake kwamba ni wakati wa Real Madrid kumpa nafasi Zidane ajaribu ku-manage club hiyo kama Pep Gurdiola alivyopewa nafasi na Barcelona.

Baada ya Madrid Kuchapwa na Barcelona benzema ajikuta akihudhuria mazoezi mwenyewe


Benzema 2
Mshambuliaji Karim Benzema jana Jumapili alitokea pekee kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Madrid kufanya mazoezi baada ya kocha Rafael Benitez kuwapa ofa ya mapumziko wachezaji wa kikosi cha kwanza siku ya Jumapili kutokana na kipigo cha goli 4-0 kutokana kwa mahasimu wao Barcelona.

16 wauawa katika ufyatulianaji wa Risasi marekani

Polisi wamesema walikuwa njiani kwenda kutawanya watu ufyatuaji wa risasi ulipotokea
Watu 16 wamejeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi katika bustani moja mjini New Orleans, polisi wamesema.
Msemaji wa polisi Tyler Gamble amesema maafisa wa polisi walikuwa njiani kuvunja mkusanyiko mkubwa wa watu katika bustani ya Bunny Friend Park mjini pale risasi zilipofyatuliwa.
Ambiulensi ziliwapeleka watu 10 hospitalini, Bw Gamble alisema, na wengine walikimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya kibinafsi.

Wapinzani wachukua dola Argentina

Macri
Macri alikuwa ameshindwa kwenye duru ya kwanza

Mgombea wa chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais Argentina, huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa.
Baada ya karibu kura zote kuhesabiwa, Bw Macri alikuwa na 52% akilinganishwa na Daniel Scioli aliyepata 48%.
Shangwe na vigelegele vilitanda katika makao makuu ya kampeni ya Bw Macri baada ya kura za maoni runingani kuonyesha alikuwa ameshinda.
Bw Macri, meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli, ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires, kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi Oktoba.
Lakini wote wawili hawakuweza kushinda moja kwa moja na duru ya pili ikaandaliwa, mara ya kwanza kwa uchaguzi kuingia duru ya pili katika historia ya Argentina.
Ushindi wa Bw Macri ndio wa kwanza katika zaidi ya mwongo mmoja kwa upinzani wenye kuegemea siasa za mrengo wa kati kulia.

Saturday 21 November 2015

Rais wa Mali atangaza hali ya Hatari

MaliWengi wa mateka waliokolewa
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza hali ya hatari nchini humo baada ya shambulio kwenye hoteli moja mjini Bamako kuua watu zaidi ya 20.
Bw keita ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa siku 10, pamoja na siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Watu wenye silaha wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Kiislamu walishambulia hoteli ya Radissom Blue mjini Bamako na kushikilia mateka watu 170.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha hakuna mateka zaidi wanaoshikiliwa.
Makundi ya Al-Qaeda Afrika Kaskazini na kundi jingine la al-Murabitoun yamedai kuhusika kwenye shambulio hilo

Thursday 19 November 2015

Nadal amchapa Andry Murray

Nadal amchapa Murray
Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa upande wa wanaume Rafael Nadal,amemshinda muingereza Andry Murray.
Nadal ameshinda mchezo huo kwa jumla ya seti 6-4 6-1, mchezo uliofanyika katika uwanja wa O2 Arena.
Nae Stan Wawrinka anayeshikilia nafasi ya nne kwa ubora alimfunga mpinzani wake David Ferrer aliyeko katika nafasi ya saba kwa jumla ya seti 7-5 6-2.
Murray atacheza na Wawrinka katika mchezo wa mwisho wa makundi siku ya ijumaa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa amri kushikiliwa kwa afisa wa juu

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa amri kushikiliwa kwa afisa wa juu anayetuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya dola bilioni mbili zilizotarajiwa kununua silaha za kukabiliana na wapiganaji wa Boko Haram.
Afisa huyo Sambo Dasuki alikuwa mshauri wa masuala ya usalama ya taifa kipindi cha utawala wa Rais aliyemaliza muda.

Wednesday 18 November 2015

Rufaa ya Sepp Blatter na Platini yakataliwa


Sepp Blatter na Michel Platini
Maombi ya rais wa FIFA Sepp Blatter na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michel Platini ya kupinga kusimamishwa kazi kwa siku 90 waliowekewa na kamati ya Fifa yamekataliwa.
Wawili hao walisimamishwa kazi mnamo mwezi Octoba huku kamati ya Fifa ikichunguza madai ya ufisadi dhidi yao.

Ufaransa yawaua wapiganaji 33 Syria

wapiganaji wa islamic state mjini Raqqa

Mashambulio ya Ufaransa na mataifa mengine dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa nchini Syria siku ya jumapili yamewauwa takriban wapiganaji 33,wanaharakati wamesema.
Kundi la wapiganaji wa haki za kibinaadamu kutoka Syria limesema kuwa wengi walifariki wakati vituo vya kukagua watu vilivyoshambuliwa.

Saturday 14 November 2015

Anna Makinda aukimbia Uspika

Anna Makinda
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo mengine.

Awali mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.

Ubelgiji yashauri raia wake waondoke Burundi

Burundi
Raia wa Burundi wamekuwa wakitoroka mitaa mingi ya mji wa Bujumbura
Ubelgiji imewashauri raia wake kuondoka Burundi, huku Muungano wa Ulaya nao ukipunguza maafisa wake wanaohudumu huko kutokana na kuongezeka kwa machafuko.
Balozi wa EU nchini humo Patrick Spirlet amesema hatari ya kutokea mapigano zaidi imeongezeka.
Hayo yamejiri huku idara ya Amani ya Usalama ya Muungano wa Afrika ikikutana mjini Addis Ababa kujadili mpango wa kutuma walinda amani nchini humo.

Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.

ParisMashambulio kadha yametokea mjini Paris
Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.

Wednesday 11 November 2015

Buhari atangaza baraza lake la mawaziri

AdeosunBi Adeosun ameteuliwa waziri wa fedha
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatimaye ametangaza wizara na mawaziri watakaozisimamia, miezi saba baada yake kushinda uchaguzi wa urais.
Nafasi muhimu ya waziri wa fedha ameikabidhi mwanauchumi Kemi Adeosun, aliyesomea Uingereza kabla ya kurejea Nigeria na kuhudumu kama kamishna ya fedha jimbo la Ogun.
Jenerali mstaafu Mansur Dan Ali atakuwa Waziri wa Ulinzi, na kazi yake kuu itakuwa kuongoza vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.
Gavana wa zamani wa jimbo la Lagos Babatunde Fashola ameteuliwa waziri wa kawi, ujenzi na makazi na anakabiliwa na kibarua cha kutatua mzozo wa umeme Nigeria.
Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mkulima Audu Ogbe ameteuliwa waziri wa kilimo.
Nigeria ina ardhi kubwa ambayo ikutumiwa vyema inaweza kubuni nafasi za kazi na kupunguza utegemezi wa mafuta, wadadisi wanasema.
Kuzinduliwa kwa baraza hilo lenye mawaziri 36 kumefanyika miezi saba baada ya uchaguzi wa urais.
Buhari
Buhari alishinda uchaguzi uliofanyika Machi
Bw Buhari aliyechaguliwa Machi alikuwa ameahidi kukabiliana na ufisadi na ukosefu wa usalama, na aliahidi kuteua watu wenye ujuzi na wasio na ila.
Mhariri wa BBC Hausa Mansur Liman anasema baraza hilo la Rais Buhari litashangaza watu na hasa uteuzi wa Bi Adeosun kuwa waziri wa fedha. Wengi walitarajia Okechukwu Enelemah, aliyeteuliwa waziri wa biashara na uwekezaji, angeteuliwa waziri wa fedha.
Rais Buhari pia ameshangaza wengi kwa kumteua mkuu wa zamani wa jeshi Jenerali Abdurrahman Dambazau kuwa waziri wa mambo ya ndani. Wengi walitarajia angeteuliwa waziri wa ulinzi.
Amina Mohammed, mshauri wa zamani wa mkuu UN Ban Ki-Moon kuhusu maendeleo endelevu, alitarajiwa kuteuliwa waziri wa mipango lakini ameteuliwa waziri wa mazingira.

Mchezaji achunguzwa kwa kutishia mbwa

OaklandKlabu ya mchezaji huyo ilishindwa kwenye mechi hiyo
Mchezaji wa Oakland Raiders Ray-Ray Armstrong anachunguzwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za ‘kubweka’ na kujipiga kifua mbele ya mbwa wa polisi.
Armstrong, 24, anadaiwa kuinua shati lake na kumchokoza mbwa huyo kabla ya mechi ya NFL dhidi ya Pittsburgh Steelers Jumapili.
Akipatikana na hatia, huenda akashtakiwa na kosa la kumchokoza mbwa wa polisi, ambalo ni kosa la ngazi ya tatu jimbo la Pennsylvania.

Teodore Obiang kuwania tena urais Equatorial Guinea

ObiangObiang ameongoza taifa hilo kwa miaka 36
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema, ambaye ameongoza taifa hilo kwa miaka 36, amesema atawania tena, shirika la habari la AFP limeripoti.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 alisema kupitia kituo cha redio cha taifa kwamba ameungwa mkono na chama chake kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka saba mwaka ujao.
Chama cha Obiang cha Democratic Party of Equatorial Guinea kilishinda viti 99 kati ya 100 vya ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2008.
Alishinda uchaguzi wa urais mwaka mmoja baadaye kwa kupata 95% ya kura.
Obiang ni mmoja wa viongozi waliokaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika.