Friday 19 February 2016

Papa Francis: Donald Trump 'si Mkristo'

Papa Francis asema Donald Trump si mkristo
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump la kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani si la kikristo.
Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si Mkristo.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.

Thursday 18 February 2016

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015 HAYA HAPA


Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
Baraza hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 121 kutokana na sababu za kiafya na watahiniwa hao wataruhusiwa kufanya mitihani ambayo hawakuifanya katika mtihani wa kidato cha nne, mwaka 2016.
Aidha baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 87 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani ambapo kati yao 25 ni wa kujitengemea na 52 ni watahiniwa wa shule wakati 10 ni wa mtihani wa maarifa (QT)
Amezitaja shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizofanya vizuri zaid kuwa ni Kaizerege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls ya Mbeya, Canossa ya Dar es salaam, Marian Boys ya Pwani, Alliance Rock Army ya Mwanza, Feza Girls Dar es salaam, Feza Boys ya Dar es salaam na Uru Seminary ya Kilimanjaro.
Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 ni pamoja na Pande ya mkoani Lindi, Igawa ya Morogoro, Korona ya Arusha, Sofi ya Morogoro, Kurui ya mkoani Pwani, Patema ya Tanga, Saviak ya Dar es salaam, Gubali ya Dodoma, Kichangani ya Morogoro na Malinyi ya Morogoro.
Kwa upande wa watahiniwa, Dkt Msonde amesema kati ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri zaidi, wanne na wasichana na sita ni wavulana.
Mwanafunzi aliyeongoza ni msichana Butogwa Charles Shija wa Canossa, akifuatiwa na msichana mwingine Congcong Wang wa Feza Girls na wa tatu ni mvulana Innocent Lawrence wa Feza Boys.
Wengine ni Dominick Marco Aidano wa Msolwa, Sang'udi E Sang'udi wa Ilboru, Asteria Herbert Chilambo waCanossa, Belinda Jackson Magere wa Canossa, Humfrey Martine Kimanya wa Msolwa, Bright B Mwang'onda wa Marian Boys na wa 10 ni Erick R Mwang'ingo wa Marian Boys.
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.


BOFYA HAPA KUPATA MATOKEO

Tuesday 9 February 2016

Zouma kuwa nje miezi sita Chelsea


Image copyrightReuters

Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Manchester United.
Zouma, atafanyiwa upasuaji kwenye kwenye goti lake ambalo aliumia Jumapili uwanjani Stamford Bridge baada ya kutua vibaya aliporuka kupiga mpira kwa kichwa.
Uchunguzi umethibitisha kwamba aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo hilo.

Maelfu wauawa kinyama Syria

Image copyrightD
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema maelfu ya raia wa Syria waliowekwa kizuizini wamekuwa wakifa kinyama kwa maelfu kwa kiwango kinachofikia uhalifu dhidi ya binadamu.
Maafisa wa Umoja wa mataifa waliofanya uchunguzi huo wanasema raia wa Syria ambao wamekuwa wakiunga mkono waasi au kuipinga serikali wamekuwa wakikamatwa hapo hapo.
Wakati huo huo Wakati Majeshi Syria yakiendelea na mapambano katika mji wa Allepo, Uturuki imesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuwapa misaada wale waliokimbia makazi yao kutokana na vita.

Sunday 7 February 2016

Mamake rais Assad wa Syria amefariki

Mamake rais wa Syria Assad afariki
Vyombo vya habari nchini Syria vinasema kwa mamake rais wa Syria Bashar al-Assad ameaga dunia mjini Damascus akiwa na umri wa miaka 86.
Anissa Makhlouf al-Assad alikuwa mjane wa rais wa zamani wa Syria Hafez Assad na wote walijaliwa jumla ya watoto sita.

Leicester City yatembeza kichapo kwa Manchester City kwenye uga wa Etihad

Leicester City yatembeza kichapo kwa Manchester City kwenye uga wa Etihad
Ligi ya soka ya EPL nchini Uingereza iliendelea leo kwa mechi kali ya kusisimua kati ya Manchester City na Leicester City.
Wenyeji Manchester City walitapatapa mbele ya mashabiki wao na kushindwa kuondoka na ushindi wala sare.
Wageni Leicester City ambao wanazidi kutia fora msimu huu, walitamba mbele ya Manchester City na kufanikiwa kuwacharaza 3-1.
Magoli ya Leicester City yalifungwa na Robert Huth katika dakika ya 3 na 60, na Riyad Mahrez katika dakika ya 60.
Sergio Aguero aliifungia Manchester City goli la kufutia machozi katika dakika ya 87.
Ushindi huo umeiwezesha Leicester City kuendelea kujikita kileleni na pointi 53 huku Manchester City ikibakia na pointi 47.

Tetemeko baya lakumba Taiwan

Tetemeko la ardhi Taiwan
Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi.

Saturday 6 February 2016

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Diwani wa CUF Muleba akamatwa , Ataja Aliyemtuma

 
Kijana huyu anaitwa "Simon Shilage" ana umri wa miaka 22, Yeye kwa kushirikiana na mwenzie mmoja ambaye bado hajapatikana ndio waliomuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg.Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.
Kijana huyu amekamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka. Amekutwa na panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga. Alipohojiwa amekiri kwamba ni kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe.Muliga kwa kumkata mapanga.

Virusi vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo

Mtoto aliyeathirika ka virusi vya Zika

Virusi hai vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo ya wagonjwa,wanasayansi wa Brazil wamesema.
Matokeo hayo hayamaanishi kwamba ugonjwa huo unaweza kusambazwa kupitia maji maji hayo ya mwilini.Sababu kuu ya kuenea kwa virusi hivyo ni kupitia kuumwa na mbu,lakini wanasayansi wanachunguza njia nyengine.
Huku maambukizi ya Zika yakiwa sio makali,ugonjwa huo umehusishwa na maelfu ya watoto waliozaliwa na kasoro.

Balozi wa Tanzania aridhishwa na hali Bangalore

Kijazi
Balozi Kijazi amesema wenyeji na Waafrika wanafaa kuwa wakikutana na kujadiliana

Balozi wa Tanzania nchini India John Kijazi amesema ameridhika kwamba serikali ya nchi hiyo imeweka mikakati ya kutosha kuwalinda wanafunzi, kufuatia kisa ambapo wanafunzi wanne walishambuliwa mjini Bangalore Jumapili.
Akizungumza baada ya kutembelea pahala ambapo wanafunzi hao walishambuliwa, na mmoja wao kuvuliwa nguo, Bw Kijazi amesema huenda kisa hicho kilitokana na suitafahamu.
“Kilicho muhimu ni tuangalie siku za usoni kwa sababu tusipofanya hivyo tutapotea. Tunahitaji kutatua tatizo la sasa lakini pia tuangalie mikakati ya muda mrefu,” ameambia wanahabari.
“Nimeridhishwa na hatua za kiusalama ambazo zimechukuliwa na serikali hapa. Kuna maafisa ambao wamesimamishwa kazi.”
Balozi huyo alikata kutaja kisa hicho kama cha ubaguzi wa rangi.
“Hatukutaka kuangazia masuala ya ubaguzi wa rangi na mambo mengine kwa sababu nadhani vyombo vya habari vinapendezwa sana na hilo. Tumejadiliana kuhusu masuala halisi na hatua madhubuti ambazo tayari zimechukuliwa na serikali ya hapa,” amesema.
Bw Kijazi alisafiri hadi Bangalore akiandamana na maafisa wawili wa wizara ya mambo ya nje ya India ambapo walikutana na waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Karnataka Dkt G Parameshwara na wakuu wa polisi wa jimbo hilo.
Polisi mjini Bangalore wamewakamata watu tisa kuhusiana na kisa hicho.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Soldevenahalli pia amesimamishwa kazi kwa tuhuma kwamba hakuchunguza kwa undani kisa hicho baada ya mmoja wa wanafunzi hao kupiga ripoti.
Konstebo wa polisi pia amesimamishwa kazi kwa kutochukua hatua kuzuia wanafunzi hao wasishambuliwe na umati.

Mwanamume ‘aliyeota mizizi’ Bangladesh

Abdul Bajandar 
Familia ya Abdul Bajandar ilishindwa kugharimia matibabu yake
Serikali ya Bangladesh imesema itagharimia upasuaji wa kumtibu mwanamume ambaye anaugua ugonjwa unaofanya mtu kupata dutu zinazofanana na mizizi ya mti mwilini.
Waziri wa afya wa Bangladesh Mohammad Nasim alitangaza hilo baada ya kumtembelea Abul Bajandar, hospitalini Alhamisi.
Bw Bajandar anaugua ugonjwa ambao kisayansi unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi.
Ni ugonjwa wa kinasaba ambao humfanya mtu kuota vidutu kwenye ngozi. Hujulikana sana kama “ugonjwa wa binadamu mti”.

Kompyuta Zilizoibwa Kwenye ofisi ya Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Philip Mpango.

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa  na TV.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.
Ameyataja magari hayo  kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV  na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV .Pia  walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo wamekamatwa.

Friday 5 February 2016

Afrika Mashariki yakataa kuitenga Burundi

Viongozi wa Afrika mashariki
Bunge la Afrika Mashariki halitaitenga Burundi katika jamii ya Afrika Mashariki.
Hatua hiyo inajiri baada ya mswada kuwasilishwa na Muungano wa mawakili wa Afrika pamoja na wanaharakati wa Afrika wakisema kwamba Burundi inafaa kutopewa uongozi wa Jamii ya Afrika mashariki hadi pale taifa hilo litakapomaliza mgogoro uliosababishwa na rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Na baada ya saa sita za kujadiliana ,kamati ya maswala ya kieneo na utatuzi wa migogoro ilitoa ripoti yao kuhusu kuzorota kwa haki za kibinaadamu nchini humo.
Ombi hilo kutoka kwa muungano huo wa mawakili ,linapendekeza hatua kadhaa ikiwemo kuondolewa kwa Burundi kutoka kwa jamii ya Afrika mashariki na badala yake kuliwekea vikwazo taifa hilo.

Mgodi waporomoka Afrika Kusini

wachimba mgodi
Takriban wachimba mgodi 52 wamekwama ardhini ndani ya mgodi wa dhahabu mashariki mwa Afrika Kusini ,kulingana na chombo cha habari cha News24.
Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi ,kulingana na daktari mmoja wa kutoa matibabu ya dharura Jacques Ainslie.
Mojawapo ya shimo liliporomoka na kuwanasa wachimba mgodi 52.
Kufikia sasa asilimia 70 ya wachimba mgodi hao ama wafanyikazi 30 wameokolewa,bwana Ainslie alikiambia chombo cha habari cha News24.
Wachimba mgodi waliojeruhiwa wamesafirishwa katika hospitali moja kwa matibabu.
Hatahivyo,watu watatu bado hawajulikani waliko na bwana Anslie amesema anashuku huenda wamekwama katika chumba ambapo mporomoko huo ulianza.

India: Wengine 'waliomvua nguo' Mtanzania mbaroni

GariGari la wanafunzi hao liliteketezwa
Washukiwa zaidi wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini India kuhusiana na kisa ambapo mwanafunzi Mtanzania alipigwa na kuvuliwa nguo mjini Bangalore.
Washukiwa wengine wanne wamekamatwa na kufikisha tisa, jumla ya washukiwa wanaozuiliwa na polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia wamesimamishwa kazi, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Watatu hao wanatuhumiwa kukataa kupokea malalamiko kuhusu kushambuliwa kwa mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake wa tatu.
Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya ndani ya jimbo la Karnataka.

Clinton na Sanders wakabiliana kwenye mdahalo

Sanders ClintonSanders na Clinton ndio wagombea pekee waliosalia chama cha Democratic
Hillary Clinton na Bernie Sanders wamekabiliana kuhusu kudhibitiwa na matajiri wa Wall Street pamoja na sera ya mashauri ya kigeni, kwenye mdahalo wa kwanza wa chama cha Democratic msimu huu kushirikisha wagombea wawili pekee.
Bi Clinton amemweleza Bw Sanders kama mtu mdhanifu ambaye hataweza kutekeleza mambo mengi anayopgania.
Bw Sanders naye amesema Bi Clinton ni mtu ambaye amejikita sana katika mfumo wa sasa wa utawala na hawezi kutekeleza mageuzi.
Mdahalo huo wa runingani katika jimbo la New Hampshire ulikuwa wao wa kwanza tangu kusalie na wagombea wawili pekee chama cha Democratic wiki hii.