Sunday 14 April 2019

Mwanafunzi adukua mtandao wa serikali na kujiajiri, Afrika Kusini


Mwanamme mmoja nchini Afrika Kusini anasakwa na polisi kwa madai ya kudukua data za serikali katika Sekta ya Afya kisha kujiajiri mwenyewe na kwamba amekuwa akipokea mshahara kuanzia mwezi Juni mwaka wa 2018.
Bright Chabota ambaye alisomea kozi ya uhandisi wa tarakilishi, Computer Engineering ni wa asili ya Zambia ila mamaye ni wa asili ya Zulu nchini Afrika Kusini. Inaarifiwa hakuwahi kwenda kazini ila amekuwa akipokea mshahara kila mwisho wa mwezi.
Kulingana na serikali, Chabota aligunduliwa baada ya kubainika kwamba hajakuwa akilipa kodi, vilevile ada za bima ya matibabu nchini humo.

Tuesday 2 January 2018

Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela.

Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu.
Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake.
Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu.
Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita.

Tuesday 19 December 2017

Diwani wa Sombetini Kupitia Chadema amesema yuko tayari Kujiunga CCM kama waliomuua Mawazo watapatikana

Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga amesema yupo tayari kurudi (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.


Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.

"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo hiyo" alindika Ally Banaga

Wawili wakamatwa na kilo 64 za madawa ya Kulevya

Wakazi wawili wa Dar es Salaam wamekamatwa eneo la Kilambo mkoani Mtwara lililopo mpakani na nchi ya Msumbiji wakiwa na pakiti zenye uzito wa kilo 64 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga alisema watuhumiwa walikamatwa Desemba 7 wakiwa na dawa hizo zikitokea mkoani Pemba nchini Msumbiji kuingizwa Tanzania.

Sianga alisema pakiti hizo zilifichwa kwenye gari na kila moja ilifungwa kwa ujazo wa kilo moja.

Alisema watuhumiwa walipokamatwa walipelekwa kwa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya ukaguzi wa kina.

Monday 18 December 2017

ROSE MHANDO AJIUNGA RASMI CCM

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho unaofanyika Mjini Dodoma.

Nasary Afunguka baada ya TAKUKURU kutupilia mbali Ushahidi wake


Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh.Joshua Nassari leo ameandika kupitia Moja ya ukurasa wake wa Mitandao ya kijamii maneno haya baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi alioutoa kwa madiwani walionunuliwa na Kujiunga ccm

Mahakama kuu ya mwachia Huru Sheikh Issa Ponda

Mahakama Kuu imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru. Alishtakiwa kwa kesi ya kutoa maneno ya uchochezi.