Tuesday, 29 December 2015

Arsenal yapaa kileleni

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.
Arsenal walipata mabao yao kupita kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Hiddink: Chelsea waonyeshe hamu dhidi ya Man Utd

WatfordChelsea walitoka sare 2-2 mechi dhidi ya Watford Jumamosi
Kaimu meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema timu yake inafaa kuonyesha hamu ya kutaka kushinda dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford leo.
Vijana hao wameshinda mechi moja pekee kati ya tano zilizopita, nao United wameshindwa mara tatu mfululizo ligini.
Chelsea walitoka sare 2-2 na Watford Jumamosi mechi ya kwanza Hiddink akiwa kwenye usukani baada ya Jose Mourinho kufutwa.
Mholanzi huyo amesema: "Mechi yoyote kati ya Chelsea na Manchester United ni kubwa lakini hii ni ya kipekee bila shaka.”
"Natumai tutaweza kuonyesha hamu ya kutaka kushinda kama tulivyofanya sehemu kubwa ya mechi (dhidi ya Watford).”
  • LVG: Naweza kuondoka mwenyewe Man United
Klabu hiyo ya Stamford Bridge itamkosa mshambuliaji Diego Costa ambaye haruhusiwi kucheza baada ya kuonyeshwa kadi ya tano ya manjano Jumamosi.
United huenda nao wakabadilisha kikosi cha kuanza mechi baada ya kushindwa 2-0 na Stoke City Jumamosi.
Kwenye mechi hiyo, nahodha wao Wayne Rooney alianza akiwa benchi kwa mara ya kwanza tangu Januari 2014.

Chelsea v Manchester United

Takwimu muhimu

8
Mechi ambazo Chelsea wameenda bila kushindwa na United ligini na katika kombe
5
Wachezaji ambao wamepewa kadi nyekundu mechi sita za ligi kati ya Chelsea na United
  • 6 Mechi za EPL ambazo Chelsea wameshinda Old Trafford, ni zaidi ya timu nyingine
Matokeo mabaya kwa United yamezidisha shinikizo kwa meneja Louis van Gaal ambaye baada ya mechi hiyo alisema anaweza kuamua kuondoka kwenye klabu hiyo.
Alipoulizwa iwapo atakuwa bado anasimamia timu hiyo dhidi ya Chelsea, alisema: “Mtahitaji kusubiri na kuona yatakayojiri, lakini nafikiri hivyo (kwamba atakuwa bado kwenye usukani) Ninahisi uungaji mkono kutoka kwa kila mtu katika klabu.”

Tuesday, 22 December 2015

Waislamu waokoa wakristo waliotekwa na Alshabab

Waislamu waokoa wakristu waliotekwa na Alshabab
Watu wawili wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab kushambulia basi moja la abiria lilokuwa likielekea eneo la Mandera Kaskazini mwa kenya kutoka Nairobi.
Shambulio hilo la kigaidi lilitekelezwa hii leo asubuhi.
Walioshuhudia wameambia mwandishi wa shirika la utangazaji la uingereza  BBC kuwa abiria wa kiislamu waliwalinda wenzao wakristo kwa kukataa kugawanywa kwa makundi.

Marekani yashambuliwa Afghanistan

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga huko nchini Afghanistan amewaua askari sita wa vikosi vya jeshi la Marekani miongoni mwa shambulio baya kuwahi kutokea miezi ya hivi karibuni.
Mshambuliaji huyo akiwa kwenye pikipiki, aliwalenga askari wa vikosi vya muungano kati ya majeshi ya NATO na askari wa doria wa Afghanistan karibu na kambi ya vikosi vya anga. Taliban wamekiri kufanya shambulio hilo.

Friday, 18 December 2015

Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea

MourinhoMourinho alikuwa tayari amekiri Chelsea hawawezi kumaliza katika nne bora ligini
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.

Thursday, 17 December 2015

Magufuli: Elimu ya bure itapatikana Tanzania

ShuleMagufuli amesema serikali itatenga dola milioni 65 za kutumwa shuleni
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure itapatikana kama alivyoahidi.
Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu ya bure, Magufuli amesema, mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo hazijawahi kukusanywa.

Maelfu waandamana kupinga serikali ya Jacob Zuma nchini Afrika Kusini

Maandamano ya kumpinga rais Zuma Afrika KusiniMaelfu waandamana kupinga serikali ya Jacob Zuma nchini Afrika Kusini

Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walifanya maandamano hapo jana katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kwa ajili ya kumpinga rais Jacob Zuma.
Waandamanaji hao waliokusanyika katika mitaa ya miji ya Johannesburg, Pretoria, Cape Town na Port Elizabeth, walimshutumu Zuma kwa madai ya ufisadi na kuzorotesha uchumi wa nchi.
Maandamano hayo yaliongozwa na kiongozi wa zamani wa muungano wa biashara Zwelinzima Vavi aliyemlaumu Zuma kwa kumbadilisha waziri wa fedha mara mbili ndani ya wiki moja.
Mnamo tareheh 9 Desemba, Zuma alimfuta kazi aliyekuwa waziri wa fedha Nhlanhla Nene na kumteua David van Rooyen kuziba pengo hilo.
Ndani ya wiki hiyo, Zuma baadaye akamuondoa David van Rooyen na kumteua Pravin Gordhan kuwa waziri mpya wa fedha.

Raia wa Rwanda walio ng’ambo wapiga kura

KagameBw Kagame anatarajiwa bado hajatangaza iwapo atawania tena urais
Raia wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi wanapiga kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Raia wanapigia kura katika afisi za ubalozi.
Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.
Raia walioko Rwanda watapiga kura hapo kesho Desemba 18.
Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017.

Wednesday, 16 December 2015

Miili ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la Mexico la Guerrero

Miili ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la Mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana.
Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco.
Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo.
Vipimo vya DNA vinatarajiwa kuchukuliwa kutoka katika familia za wanafunzi hao waliokufa, kuweza kujua kama ni kweli ni hao, ambao hawajapatikana mpaka sasa

Tuesday, 15 December 2015

Chelsea yachapwa tena na Lester City

Wachezaji wa Leicester City wakishangilia ushindi
Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Chelsea wamezidi kuwa katika wakati mgumu msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.
Mshambulijai wa Jamie Vardy ndie aliyeanza kupeleka msiba kwa The blue baada ya kuandika bao la kwanza katika katika ya 34 ya mchezo. Winga Riyard Mahrez akaongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 48 ya mchezo.

Sunday, 13 December 2015

21 wafariki baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa nchini Urusi

Moto wazuka kwenye hospitali ya vichaa Urusi21 wafariki baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa nchini Urusi

Watu 21 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa iliyoko Voronezh, kusini magharibi mwa Urusi.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na wizara ya maafa na misaada ya dharura nchini Urusi, miili ya watu 19 ilipatikana kwenye eneo la tukio, huku wengine wawili wakiripotiwa kufariki wakati wa matibabu.
Watu wengine 55 pia wameweza kuokolewa na kuondolewa kutoka kwenye hospitali hiyo, huku baadhi yao wakiwa na majeruhi madogo ya kuunguzwa na moto huo.

Mhongo aahidi kushusha bei ya umeme

WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka. Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale.
“Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo.

Saturday, 12 December 2015

Hodgson: Itakuwa vigumu kumuacha Vardy

VardyVardy amevunja rekodi ya Van Nistelrooy iliyodumu miaka 12
Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema itakuwa vigumu kumuacha Jamie Vardy nje ya kikosi chake cha Euro 2016 iwapo mshambuliaji huyo wa Leicester ataendeleza makali yake ya sasa.
Vardy alivunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy iliyodumu miaka 12 kwa kufunga mechi 11 mfululizo Ligi ya Premia.

Makaburi matatu nchini Moscow yawekwa Wi-Fi

ChekhovMwandishi mashuhuri Anton Chekhov ni mmoja wa watu mashuhuri waliozikwa Novodevichy
Makaburi matatu yanayotembelewa sana na watu jijini Moscow yatawekewa huduma ya mtandao ya wi-fi.
Wanaotembelea makaburi hayo wataweza kutumia mtandao wa intaneti bila malipo katika makaburi ya Novodevichy, Troyekurovskoye na Vagankovo kuanzia mapema 2016 kwa mujibu wa tovuti ya Moscow City.
Mkuu wa huduma za makaburi mjini Moscow Artem Yekimov anasema lengo ni kusaidia wageni kwenye makaburi hayo kutafuta habari zaidi kuhusu watu mashuhuri waliozikwa humo.
Aidha, kuwafanya wafurahie matembezi yao makaburini.

Mtoto wa Gaddafi aachiwa huru

HannibalHannibal amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani Oman tangu 2012
Mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Hannibal, ameachiliwa huru baada ya kutekwa nyara kwa muda na kundi la wapiganaji, duru za kiusalama zinasema.
Kwenye video iliyoonyeshwa kwenye runinga ya Lebanon, mfanyabiashara huyo alionekana akiitisha habari zaidi kuhusu kutoweka kwa mhubiri mashuhuri wa dhehebu la Washia nchini Lebanon Musa al-Sadr. Al-Sadra alitoweka mwaka 1978. Alionekana kwenye video hiyo akiwa amejeruhiwa machoni.

Ronaldo atarajia kugombea urais wa shirikisho la kandanda la Brazil

Ronaldo apanga kuwa kiongozi wa CBFRonaldo atarajia kugombea urais wa shirikisho la kandanda la Brazil

Nyota wa zamani wa soka wa Brazil Ronaldo, ametangaza uwezekano wake wa kugombea nafasi ya urais wa shirikisho la kandanda la Brazil CBF.
Ronaldo alitoa tangazo hilo baada ya rais wa CBF Marco Polo del Nero kukabiliwa na kashfa za ufisadi kutoka kwa viongozi wa Marekani.
Naibu wa rais wa CBF Jose Maria Marin pia aliwahi kutangaza kuachia ngazi kutokana na kashfa za ufisadi zilizomuandama mwezi Mei.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Sao Paulo, Ronaldo alimshutumu Del Nero kwa kutumia mbinu ya kumchagua Antonio Nunes kuziba nafasi ya Marin kwa lengo la kuendeleza ufisadi.

Friday, 11 December 2015

Lipumba, Lissu wamvaa Magufuli kwa uteuzi wa baraza la mawaziri

Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini.

Tanzania yapata maabara ya kuchunguza Ebola

TanzaniaTanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.

Yaya Toure ndiye mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka 2015.

YayaHii ni mara ya pili kwa Toure kutwaa tuzo hiyo
Yaya Toure ndiye mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka 2015.
Kiungo huyo wa kati wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 32 anakuwa wa tatu, baada ya Wanigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha, kushinda tuzo hiyo mara mbili.
Mashabiki walimpigia Toure, anayechezea Manchester City, kura nyingi kushinda Yacine Brahimi, Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew na Sadio Mane.
Alishinda tuzo hiyo mara ya kwanza 2013.
Brahimi kutoka Algeria amewahi kushinda tuzo hiyo 2014 naye Mghana Ayew aliishinda 2011. Aubameyang kutoka Gabon alikuwa akishindania tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mtawalia, huku Mane, kutoka Senegal, akishindania kwa mara ya kwanza.

Wednesday, 9 December 2015

Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani.

Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani.
Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani.
Duru zinaarifu kuwa mshindi huyo wa tuzo ya Oscar pamoja na rubani wake walinusurika kufariki baada ya ndege waliokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu lake ilipokuwa ikikwenda kwa kasi kabla ya kupaa angani.

Man U yapigwa nje michuano ya UEFA

NaldoNaldo alifungia Wolfsburg mabao mawili
Manchester United wameondolewa kutoka kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kushindwa na klabu ya Wolfsburg kutoka Ujerumani Jumanne usiku.
Vijana hao wa Old Trafford waliondoka Ujerumani na kichapo cha 3-2.
Red Devils walikuwa wameanza vyema Anthony Martial alipowafungia baada ya kupata pasi kutoka kwa Juan Mata.

Sunday, 6 December 2015

Polisi: Shambulizi la kisu London ni la 'kigaidi'

Polisi wanasema Aliyemdunga kisu abiria London ni 'gaidi'
Idara ya polisi nchini Uingereza inasema kuwa inalichukulia kisa cha udungaji kisu katika kituo cha gari moshi jijini London, kama tendo la kigaidi.
Mtu mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu aliwashambulia abiria katika kituo cha treni kilichoko eneo la Leytonstone.

Gazeti latangaza kifo cha father christmas

SantaFather Christmas alifariki akiwa na umri wa miaka 227, kwa mujibu wa tangazo gazeti hilo
Gazeti moja nchini Norway limelazimika kuomba radhi baada ya kuchapisha tangazo la kicho cha "Father Christmas".
Tangazo hilo lilikuwa la "Mpendwa Father Christmas, aliyezaliwa 12 Desemba 1788", ambaye alidaiwa kufariki tarehe 3 Desemba mjini Nordkapp, ulio kaskazini mwa Norway.

Jose Mourihno azungumzia Usajili baada ya kipigo cha jana kutoka Afc Bornmouth

Mo 3Baada ya kipigo cha kushangaza kutoka kwa Bernoumoth cha goli 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge, kocha Jose Mourinho wa Chelsea ameitoa Chelsea katika kuwania nafasi nne za juu huku akisisitiza kuwa wanahitaji kupigana kwa ajili ya nafasi sita za juu.
Akiongea mara tu baada ya mchezo huo kumalizika, Jose amesema kuwa kabla ya mchezo huo wakikua na imani na mipango ya kugombana kuingia top 4 baada ya awali kujitoa katika mbio za ubingwa, na sasa anasema top 6 ndio kitu pekee wanahitaji kugombania kama timu.