Thursday 17 December 2015

Raia wa Rwanda walio ng’ambo wapiga kura

KagameBw Kagame anatarajiwa bado hajatangaza iwapo atawania tena urais
Raia wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi wanapiga kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Raia wanapigia kura katika afisi za ubalozi.
Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.
Raia walioko Rwanda watapiga kura hapo kesho Desemba 18.
Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017.

Lakini kiongozi huyo ayashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki.
Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.
Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa.
Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa rais kutoka miaka saba hadi miaka mitano, na kudumisha muda wa mihula miwili, sheria hiyo haitaanza kutekelezwa hadi mwaka 2024.
Hii ina maana Bw Kagame atakuwa huru kuwania urais kwa mihula mingine miwili ya miaka mitano mitano.
Rwanda
Bunge la Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo mwezi uliopita
Uwezekano wa marekebisho hayo kuidhinishwa katika kura ya maoni ni mkubwa, kwa mjibu wa shirika la habari la AFP.
Chama cha Kagame cha Rwanda Patriotic Front, kundi la waasi wa kabila la Tutsi, kilisaidia kukomesha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyotekelezwa na Wahutu wenye msimamo kali.
Zaidi ya watu 800,000 - wengi wao Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadiri waliuawa.
Bw Kagame bado hajatangaza iwapo atawania kiti cha urais mnamo mwaka 2017 iwapo atakubaliwa kufanya hivyo.
Anatarajiwa kufanya uamuzi huo baada ya kufanyika kwa kura ya maamuzi, kwa mujibu wa gazeti la Rwanda la New Times.

No comments: