Thursday 31 March 2016

Mahakama yatupilia mbali kesi Uganda


Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imefutilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita.
Mahakama hiyo ilisema kuwa licha ya kuwepo kwa dosari nyingi za uchaguzi, matokeo ya mwisho hayakuathiriwa.

Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.

Rais wa Tanzania John Magufuli.
 Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa.
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Tuesday 29 March 2016

Wanariadha wala sabuni kwa kuwa hawajui kingereza

Sabuni
Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza.
Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily.
Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri .

Wamexico washerehekea sikukuu ya pasaka kwa kuchoma sanamu a Donald Trump

Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'
Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republicans Donald Trump.
Mojawapo ya tukio hilo la kushangaza limefanyika katika kitongoji kimoja cha wakaazi walio na kipato cha chini kiitwacho La Merced.
Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.

Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC

Tanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada
wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8 ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC akisema "imepuuza hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia" nchini humo.
''Inasikitisha kuwa demokrasia yetu inatathminiwa tu na matokeo ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,''
Waziri wa mambo ya nje bwana Augustine Mahiga
Kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar Bw Mahiga anasema kuwa Tanzania, ilifanya kila kitu kuambatana na sheria na katiba ya nchi wala hakuna tatizo ama ukiukwaji wa sheria.
Mahiga anasema kuwa huo ni uamuzi wao na kwa sababu hela hizo ni zao wanauhuru wa kuzitumia watakavyo ila anahoji kwanini uamuzi huo uliafikia bila ya majadiliano na serikali ya muungano ya Tanzania.

Monday 21 March 2016

Tetesi za Usajili barani Ulaya

Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amepewa kipaumbele kuja kuchukua mikoba ya kocha wa Aston Villa Mfaransa Remi Garde anayetegemewa kutimuliwa siku za hivi karibuni. (Chanzo Daily Mail)
Shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) linataka kujaribu kwa mara ya mwisho kumzuia mshambuliaji wa Arsenal Alex Iwobi, 19, kuchukua uraia wa Nigeria. (Chanzo Daily Mirror)
Mabingwa wa nchini Italia Juventus watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud, 29, mwishoni mwa msimu ikiwa watamkosa chaguo lao namba moja, Edison Cavani, 29, wa Paris St-Germain. (Chanzo Tuttosport kupitia Daily Express)

Watu wawili Mkoan Dar Es Salaam wamefariki dunia kwa maradhi ambayo dalili zake zinafanana na ugonjwa wa ebola.



Watu wawili wamefariki dunia kwa maradhi ambayo dalili zake zinafanana na ugonjwa wa ebola.






Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa MNH, Dk Praxeda Ogweyo alisema wamewapokea wagonjwa hao wawili,  lakini vipimo havijaonyesha kama wana ebola.  “Ni kweli kuwa tumewapokea wagonjwa hao wawili na vipimo vya mgonjwa wa kwanza kinaonyesha hana ebola, lakini bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kujua ni ugonjwa gani,” alisema.

Azam yaendeleza Kichapo dhidi ya Bidvest ya afrika Kusini

TIMU ya Azam FC leo imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar.

Mabao ya Azam FC yamepachikwa kimiani na Kipre Tchetche aliyefunga mabao matatu ‘hat trick’ na moja likapachiwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco.

Katika mechi ya kwanza, Bidvest ilipoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani Johannesburg. Safari hii imepata mabao matatu lakini ikashindiliwa mengine manne. Maana yake Azam FC imevuka kwa jumla ya mabao 7-3

Nyumba zaindelea kupigwa X Zanzibar

Watu Wasio Julikana Wasambaza Vipeperushi vya vitisho Visiwani ZanzibarSiku moja kabla ya kufika siku ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar h watu wasio julikana usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi (jana) wameziwaekea X Nyekundu nyumba kadhaa za wakazi wa Pujini katika wilaya chake chake chake na kuwaekea kipeperushi cha onyo juu ya ushiriki wao kwenye uchaguzi huo.
Moja kati ya watu walio wekewa X hizo kwenye  nyumba yake amesema wamelala walipo amka walijikuta nyumba zao zikiwa tayari zina X na kuekewa kipeperushi hicho cha onyo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kusini Pemba ilifika kijijini Pujini Kumvini na Kijili kujionea nyumba hizo zilizo wekewa X nyekundu ampapo mwenyekiti wakamati hiyo mkuu wa mkoa Kusini Pemba Bio Mwanajuma Majidi Abdalla amewataka watu wanao taka kwenda kupiga kura waende kupiga kura na kuzipuzia X hizo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Barack Obama wa Marekani aliwasili Cuba Jumapili katika ziara ya kihistoria

Rais Obama akipunga mkono mara baada ya kuwasili HavanaHAVANA - Rais Barack Obama wa Marekani aliwasili Cuba Jumapili katika ziara ya kihistoria, huku mataifa haya mawili yakiendelea na hatua za kurejesha uhusiano wao baada ya kufarakana kwa miaka 55.
Obama, rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kutembelea Cuba katika miaka karibu 90, atakamilisha ziara yake kwa hotuba ya moja kwa moja kwa watu wa Cuba akielezea dira yake ya uhusiano wa baadaye baina ya Marekani na Cuba.
Obama alishuka kutoka katika Air Force One huku kukiwa na kiwingu na mvua za rasharasha katika uwanja wa Havana kiasi cha saa kumi na nusu jioni Jumapili.

Mwandishi wa Dw apatikana

SalmaSalma alikamatwa na watu wasiojulikana Ijumaa
Mwandishi aliyewakilisha kituo cha redio cha Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) visiwani Zanzibar Salma Said na ambaye alitoweka Ijumaa, amepatikana.
Kamanda wa polisi wa Dar Simon Siro amethibitisha kupatikana kwa mwanahabari huyo.
Ukomboz  imezungumza na Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis, ambaye amesema kwa sasa Salma yumo anatoa maelezo kwa polisi Dar es Salaam

Sunday 20 March 2016

Msichana anayevuja damu machoni

Mernie-Rae
Huyu ni Marnie-Rae Harvey ambaye hutokwa na damu machoni lakini madaktari hawaelewi chanzo chake ni nini.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 anasema kuwa hawezi kutoka nje na hana marafiki kwa sababu kila mara huwa nyumbani kwao.
Amewatembelea wataalam wa macho na madaktari wa maswala ya uzazi,madaktari wa watoto na wataalam wengine kujua sababu ya tatizo hilo.

Monday 14 March 2016

Shambulio la Kigaidi laua Ivory Coast

Watu 16 wameuawa nchini Ivory Coast katika shambulio llililofanywa kwenye hoteli ya kitalii ya Grand Bassam iliyoko ufukweni.
Rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara, amesema wawili kati yao ni wanajeshi huku wavamizi sita pia wakiuawa karibu na mji wa Abidjan.
"Na bila shaka, kwanza kabisa, nitapenda kusema kuwa, hivi vitendo vya woga vya kigaidi kamwe hazitavumiliwa nchini Ivory Coast. Tumechukua hatua madhubuti dhidi yake''. amesema Ouattara.
Rais amesema hali ya usalama itazidi kudhibitiwa nchini kote.
Shambulizi hili limedhibitiwa ndani ya muda wa saa tatu mpaka nne,
Watu, waliokwenda katika eneo hilo, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa juma, wamerudishwa mjini Abidjan.

Video ya goli la Sammata alipoisaidia KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 4-1

March 13 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta alipata nafasi ya kuanza na kikosi cha Genk kwa mara ya kwanza na hili ndio goli lake la kwanza akicheza first eleven na la pili toka ajiunge na klabu hiyo.

Sunday 13 March 2016

Wafanyakazi Waliofukuzwa NIDA Wagoma Kupokea Barua Za Kuachishwa Kazi


Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) waliofutiwa mikataba ya kazi, wamegoma kupokea barua za kuachishwa kazi wakidai kwamba hawajui kilichoandikwa kuhusu hatima ya madai yao Wafanyakazi hao walikutana jana Dar es Salaam na kiongozi wao, Seif Kibangu alisema wamekubaliana kutochukua barua hizo hadi pale watakapopata ushauri kutoka kwa wanasheria.

“Licha ya mishahara ya miezi mitatu tuna madai yetu mengine ikiwamo makato ya mafao yetu yaliyotakiwa kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, pia tumekuwa tukikatwa bima ya afya asilimia tatu ya mishahara yetu hatujui hatma yake.

"Sasa leo wanataka tuchukue barua hizo tena kwa kusaini kabla ya kujua kilichoandikwa hapana tuendelee kuvumilia haki yetu tutaipata,” alisema Kibangu.

Diamond Platnum ampongeza Makonda kwa kuteleuliwa kuwa mkuu wa mkoa

Mwanamuziki Mwenye mafanikio makubwa katika mziki wa Bongo flava ametuma salamu za pongezi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika haya:

Mafanikio hujaga kwa juhudi na kuto kukata tamaa... Hongera sana my brother @PaulMakonda kwa kuchaguliwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam... nakutakika kila lenye kheri kwenye kuhakikisha Dar es salaam yetu Inang'ara  @PaulMakonda

Nimekasirika Kupata Hii Tuzo Kutoka Nigeria - Richie Afunguka Adai Alitaka zote Mbili

Richie ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Weekend Breakfast siku ya jumapili,, na kusema kuwa baada ya filamu yake kuingia kwenye hizo category mbili aliamini yeye anaweza hivyo alitaka ashinde zote mbili, ingawa kwenye tuzo za Tanzania haikuwahi kuwa nominated.

“Ningechukua zote mbili, nilipochukua ile moja nilikasirika, naamini kama ninajua, tuzo za Tanzania haikupita hata kuwa nominated, nilikwenda Nigeria nikiwa na uhakika ninaenda kushinda”, alisema Richie.

Pamoja na hayo Richie amesema sio mtu wa majivuno na kujionyesha kama ilivyo kwa wengine, kwani tuzo hiyo sio ya kwanza kuchukua, kwani alishawahi kuchukua tuzo kubwa zaidi ya hiyo mwaka 2001, pamoja na uvumilivu na bidii ndio umemfikisha hapo.

Awadhi Juma aiweka Simba kilelen leo dhid ya Prison

Wakati watani zao wa jadi Yanga wamemaliza kucheza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda kwa ushindi wa goli 2-1 March 12, Simba wao wameshuka dimbani March 13 kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Rais Magufuli kateua Wakuu wapya wa mikoa… yumo na Paul Makonda,

Magufuli awateua wakuu 13 wapya wa mikoa
Rais wa Tanzania amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais.
Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe.

Saturday 12 March 2016

Mh. Esther Bulaya kaachiwa huru

Mh Estar bulaya mbunge wa bunda akiwa kwenye office ndogo za bunge jiji daresalam baada yakuachiwa huru na mda huu anaelekea airport kwa ajiri ya safari yakwenda mwanza kwenye kikao cha kamati kuu..

Yanga yaichapa APR 2-1


YANGA SC imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia hatua ya mwisho ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji APR katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Asante kwa wafungaji wa mabao hayo, beki Juma Abdul Jaffar kipindi cha kwanza na kiungo Thabani Scara Kamusoko kipindi cha pili na Yanga sasa watahitaji hata sare mchezo wa marudiano ili kusonga mbele

Mkutano wa Donald Trump wakumbwa na ghasia

Donald Trump
Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mkutano huo ulifutwa pia kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wanaohusika na masuala ya usalama wa eneo hilo.

Kizimbani kwa kusema Rais Mugabe ni Mzee

Rais Mugabe
Afisa mmoja wa polisi amefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baada ya kulaumiwa kwa kusema kuwa rais Robert Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka 92 ni mzee sana kuwa kiongozi.
Thomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtusi mkewe rais Mugabe, Grace, kuwa kahaba kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi nchini humo.

Friday 11 March 2016

Ben Carson amuunga mkono Donald Trump

Carson na Trump
Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Ben Carson amethibitisha kwamba anamuunga mkono aliyekuwa mpinzani wake Donald Trump katika kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.
Carson alimuidhinisha katika mkutano wa pamoja na wanahabari mjini Florida huku Trump akiwa anaongoza katika kura ya mchujo wa kumtafuta atakayewania urais kupitia chama hicho kabla ya Jumanne kuu.
Bwana Carson ,aliye kifua mbele aling'atuka wiki iliopita baada ya kushindwa kuungwa mkono.

Mwanamuziki Bob Junior Akamatwa na Polisi Kwa Tuhuma za Kushirikiana na Majambazi


Msanii wa muziki wa bongo fleva Bob Junior amekamatwa na jeshi la Polisi nyumbani kwao magomeni mapipa Jijni Dar es salaam majira ya saa sita mchana wa leo.

Kwa mujibu wa chanzo cha  habari ambaye ni rafiki wa karibu wa Bob Junior ameiambia ukomboz blog.com kuwa Polisi wamemkamata Msanii huyo kwa kile walichodai kuwa wamepata taarifa kuwa Bob Junior anashirikiana na kikundi cha majambazi.

Rafiki huyo wa karibu na Bob Junior, ameiujuza mtembezi.com kuwa Msanii huyo amekuwa akipigiwa simu tangu juzi kutoka kituo cha polisi cha magomeni usalama kwamba kuna lalamiko la mtu anaye dai kutekwa na kikundi cha majambazi ambacho msanii huyo anashirikiana nacho

Friday 4 March 2016

BREAKING: Waziri Jenister Mhagama Kafanya Maamuzi NSSF Usiku Huu...Atengua Uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NSSF

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenister Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa leo Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa usiku huu imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu, uteuzi mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa zitatolewa kwa wananchi

Aliyesema hakuna Mungu nchin Urusi ashitakiwa

KrasnovAkipatikana na hatia, Krasnov huenda akafungwa jela mwaka mmoja
Mwanamume aliyeandika kwamba hakuna Mungu katika majibizano mtandaoni ameshtakiwa kusini mwa Urusi.
Viktor Krasnov aliripotiwa kwa polisi na wanaume wawili waliokasirishwa na lugha aliyoitumia wakati wa majibizano katika mtandao wa kijamii wa Kirusi wa VKontakte mwaka 2014.
Mtandao huyo hufanana sana na Facebook na ni maarufu sana.
Ameshtakiwa Stavropol kwa kosa la "kutusi hisia za waumini”.
"Matusi” kama hayo yaliharamishwa kisheria mwaka 2013 baada ya kesi ya Pussy Riot.
Wakati wa majibizano hayo, Bw Krasnov anadaiwa pia kupuuzilia mbali Biblia na kusema ni “mkusanyiko wa hadithi za kubuni za Wayahudi”.

Thursday 3 March 2016

Jipu la wanaotumia majina feki Mitandaon Kutumbuliwa

Mahakama
Watu wanaobuni majina bandia katika mitandao huenda wakakabiliwa na mashtaka kulingana na maelezo yaliopendekezwa na waendesha mashtaka nchini Uingereza na Wales.
Huduma ya waendesha mashtaka inasema watu wazima ni lazima washtakiwe iwpo watatumia majina bandia katika mitandao ya kijamii ili kuwanyanyasa wengine.
Pia watu wanaoweka machapisho yasio na heshima ya uongo na kusababisha dhiki na wasiwasi pia watashtakiwa.

Magufuli na Kenyatta wazindua barabara Arusha

EACRais Kenyatta aliwasili Tanzania jana kwa mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanaweka jiwe la msingi katika barabara itakayounganisha mji wa Arusha nchini Tanzania na mji wa Voi nchini Kenya.
Barabara hiyo kutoka Arusha hadi Taveta inatarajiwa kurahisisha uchukuzi na kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Ina umbali wa kilomita 234 na ni sehemu ya mradi mkubwa wa barabara inayotoka Arusha na kupitia Holili na Taveta hadi Mwatate. Jiwe la msingi limewekwa na marais hao wawili eneo la Tengeru, Arusha.
Mwaka uliopita Rais Kenyatta na Rais wa Tanzania wakati huo Jakaya Kikwete walizindua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Taveta-Mwatate/Voi iliyo upande wa Kenya.

Wednesday 2 March 2016

Tanzania na Kenya kuimarisha ushirikiano

Rais Uhuru na Magufuli katika ikulu ya rais nchini Tanzania
Kenya na Tanzania zimekubaliana kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kukuza biashara.
Katika mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameeleza kufurahishwa kuona Rais John Magufuli wa Tanzania yupo tayari kuhakikisha nchi hizo zinakuwa karibu na miradi ya maendeleo inaharakishwa.
Mradi mwingine wa maendeleo walio ujadili ni kuzalisha ajira kupitia viwanda.

Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.

'Nilikosea, nawaomba radhi watanzania' ,Rosemary Odinga
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.
''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).
''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.