Wednesday, 31 December 2014

Kiongozi wa juu wa Al-shabab auwawa

Askari wa Somalia wakifanya ulinzi huko Mogadishu, Somalia.
Serikali ya Somalia, inasema mkuu wa ujasusi wa Al-Shabab aliuwawa katika shambulizi moja la anga la Marekani, karibu na mji wa Saakow.
Taarifa iliyotolewa na idara ya usalama wa taifa ya Somalia, na idara ya ulinzi  Jumanne, imesema Abdishakur Tahlil aliuwawa na watu wengine wawili katika shambulio la Jumatatu.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa, Tahlil alikuwa anasafiri kati ya Saakow na kijiji cha Jawari ambapo gari lake lilishambuliwa na kuharibika vibaya.
Kundi hilo lenye uhusiano na Al-Qaida, la Al-Shabab, linajaribu kuiondoa serikali ya Somalia, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi ya Kislam yenye msimamo mkali.
Msemaji wa Marekani alisema Jumatatu, kwamba maafisa hawaamini kama kulikuwa na raia yoyote katika shambulio hilo.
Mwezi September, shambulizi lingine la anga la Marekani liliua kiongozi wa Al-Shabab Ahmed Abdi Godane.
Majeshi ya Somalia, na Umoja wa Afrika, yamefanikiwa kuwashambulia na kuwarudisha nyuma wanamgambo wa Al-Shabab, katika miaka ya hivi karibuni.

Ndoa za jinsia moja zaanza kufungwa huko uskochi

Joe na mwenzake Brown wakifunga ndoa nchini Uskochi

Harusi ya kwanza ya watu wa jinsia moja imefanyika huko Uskochi .
Joe Schofield na Malcom Brown walifunga ndoa katika sherehe iliofanyika katika eneo la Trade Hall Glasgow huku Susan na Gerrie Douglas -Scott wakifanya harusi yao katika eneo la faragha mjini humo.
Sheria hiyo mpya ya watu wa jinsia moja ilianza kufanya kazi Uskochi mapema mwezi huu.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na waziri wa kwanza wa Uskochi.
Susan na mwenzake Gerrie wakifanya ndoa yao huko Uskochi
Nicola Sturgeon na mashirikishi wa chama cha Green Party Patrick Harvie MSP walishuhudia ndoa ya Susan na Gerrie naye mshairi wa kitaifa wa Uskochi Liz Lochhead na waziri wa serikali ya Uskochi Marco Biagi MSP wakihudhuria sherehe ya bwana Schofield na mwenzake bwana Brown.
Susan mwenye umi wa miaka 54 na Gerrie Douglas-Scott mwenye umri wa miaka 59 wanaishi mjini Galsgow ambapo walikutana miaka 18 na wana watoto wakubwa watano.
Walioana mwaka 2006 na kuamua kufanya sherehe mwaka huu.

Tuesday, 30 December 2014

Moto wateketeza maduka 18, magari na pikipiki Tanga

Lori lililoteketea kwa moto


MOTO mkubwa umeteketeza maduka 18 katika mtaa wa Kwakivesa wilaya ya Handeni mkoani Tanga baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kugonga nguzo ya umeme kupinduka na kisha kuanza kuwaka moto uliosambaa hadi kwenye maduka hayo.
Taharuki hiyo imetokea leo majira ya saa 5:00 asubuhi baada ya lori hilo lililokuwa kwenye mwendo kasi kutaka kumkwepa mwendesha bodaboda na kujikuta likiacha njia na kugonga nguzo ya umeme na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi huo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa moto huo ulitokea saa 5.asubuhi katika mtaa huo kufuatia roli la mafuta aina ya Fuso kugonga nguzo ya umeme na kusababisha betri kutoa cheche zilizosababisha moto kuanza kuwaka. Kamanda Kashai amesema roli hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Ali Makelele ambaye bado hajapatikana huku utingo wake aliyemtaja kwa jina moja la Mfundo akiwa amekimbizwa hospitali ya Wilaya ya Handeni kwa matibabu Zaidi baada ya kuungua vibaya.
“Moto ulianza kuliteketeza roli hilo la mafuta na baadaye ukasambaa kwenye maduka jirani ,hali ilikuwa mbaya sana, hadi sasa hatujajua hasara iliyopatikana, tutakapokuwa na taarifa kamili tutawataarifu“, amesema kamanda Kashai.
Aidha mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kuwa moto huo ulishika kasi kwa haraka kutokana na hali ya hewa kuwa ya upepo mkali licha ya juhudi za wananchi kuuzima lakini uliwashinda nguvu.
Aidha jeshi la polisi limelaani mtindo unaoota mizizi hivi sasa wa wananchi kujichukulia sheria mkononi kwani baada ya tukio la moto kutokea kikosi cha zimamoto kutokea Korogwe kilifika katika eneo la tukio lakini badala ya kuachwa kufanya kazi yake kikashambuliwa.
Shambulio hilo la wananchi kwa zimamoto limesababisha hasara ikiwa ni pamoja na kuvunjwa vioo vya gari, kupotea kwa vitendea kazi pamoja na baadhi ya askari wa zimamoto kujeruhiwa.
SOURCE :MWANANCHI

Miili ya watu 40 waliopotea na ndege yapatikana

Missing AirAsia flight found in Java Sea (AP)
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.

Wavamia na kumteka Mtoto Mwanza

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola

Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ametutaarifu  kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.
Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

Monday, 29 December 2014

Messi kupewa tuzo ya Heshima Hispania

Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kitampa Lionel Messi tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.
Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.
Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.
Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi ya Atletico Madrid.
Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote.

Ndge iliyopotea yaendelea kutafutwa

Airasia iliotoweka
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

Monday, 22 December 2014

Azam uso kwa uso na El Merreikh ya Sudan

Mabingwa Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2013/14 , Azam FC wamepangwa kucheza na Timu ya El Merreikh ya Sudan.
Mechi hiyo ya Ligi wa Mabingwa Afrika itakuwa ya kwanza kwa Azam FC katika kampeni zao za kuwania na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hii ni mara ya kwanza timu hiyo kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa ya Caf ni kwamba Azam FC itaanzia nyumbani Dar es Salaam na kumalizia ugenini mechi ya pili mjini Kharthoum.
Wakati huo huo Timu ya Yanga itaanza kampeni yake ya Kombe la Shirikisho kwa kuivaa BDF IX ya Botswana inayomilikiwa na Jeshi la nchi hiyo.
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza ratiba ya michuano hiyo.
Yanga itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini dhidi ya Waswana hao waliowahi kung'olewa na Timu ya Simba.

Rais Kikwete azungumza na wazee juu ya sakata La Escrow

Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.
SOURCE: BBC

Sunday, 21 December 2014

Korea kazkazini sasa yaionya Marekani

Rais wa Korea Kazkazini Kim Jong un .

Korea Kazkazini sasa inataka uchunguzi wa pamoja na Marekani kufanywa kuhusu wizi wa mtandaoni uliosababisha kampuni ya Sony Pictures kuahirisha maonyesho ya filamu ya ucheshi inayomdhihaki raia wa Korea kazkazini Kim Jong-un.
Imesema kuwa shtuma hizo za shirika la ujasusi nchini marekani FBI kwamba Pyongyang ndio iliotekeleza uovu huo inaliharibia jina taiafa hilo.
Chombo rasmi cha habari nchini humo kilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni ambaye jina lake halikutajwa akisema kuwa taifa lake litachukua hatua kali iwapo Marekani itakataa ombi hilo.
Taifa la Korea Kazkazini hapo awali lilikuwa limeunga mkono uvamizi huo wa kampuni ya Sony likisema kuwa ni kitendo cha haki.
Rais Obama amesema kuwa Marekani itajibu shambulizi hilo la mtandaoni wakati utakapowadia

Friday, 19 December 2014

Vikosi vya Libya vyaanzishwa tena mashambulizi

Wapiganaji wazidi kushambuliana nchini Libya tangu kuanguka kwa utawala wa Muamar Gadaffi
Shambulizi lililolenga kituo muhimu cha mafuta mashariki mwa Libya halikufua dafu kutokana na mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na vikosi vya serikali vinavyotambuliwa kimataifa.
Kamanda mmoja wa jeshi la wanahewa anasema kuwa mashambulizi ya angani yaliwalenga watu wenye silaha waliokuwa wakisonga mbele katika kituo cha mafuta cha Al-Sidra ambapo watu wengi waliuawa.
Zaidi ya miaka mitatu tangu kuanguka kwa utawala wa kanali Muamar Gadaffi serikali hasimu bado zinapigania madaraka nchini Libya
Source: BBC

Balotelli afungiwa mechi moja na faini juu

Chama cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii.
Adhabu hiyo itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi ya elimu.
Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi.
Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia.
Baada ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa "makosa".
Balotelli aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema: "nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru la FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.
Balotelli alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli ameifungia magoli mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya Liverpool tangu atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi
Chama cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii.
Adhabu hiyo itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi ya elimu.
Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi.
Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia.
Baada ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa "makosa".
Balotelli aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema: "nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru la FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.
Balotelli alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli ameifungia magoli mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya Liverpool tangu atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi

Rais wa Kenya aidhinisha sheria Mpya ya usalama


Rais Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.
Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.
Vyombo vya habari vimesema baadhi ya vipengee vya sheria hio ninabana uhuru wa vyombo vya habari na hata kutishia kwenda mahakamani.
Mswada huo kabla ya kutiwa saini na kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na katiba.
Vurugu katika bunge la Kenya wabunge walipokuwa wanajadili mswada wa sheria kali ya usalama
Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.
Polisi pia ndio watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au kuonyeshwa katika vyombo vya habari.
Vyombo vya habaro vinasema haya yanakwenda kinyume na uhueu wa vyombo vya habari.
Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu.

Haruna Moshi Kulipwa na Diamond

NYOTA wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’, ambaye kwa sasa anakipiga Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, atakuwa akilipwa mshahara wake na watu watatu akiwemo mwanamuziki Diamond Platinum.
Boban amesajiliwa katika timu hiyo baada ya kushindwana na Mbeya City dakika za mwisho za dirisha dogo ambapo   atakuwa analipwa Shilingi laki nane.
Mmoja wa viongozi wa Friends Rangers, alisema kwamba Diamond atakuwa anatoa Shilingi laki nne, kuna mdau mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina lake atakuwa anatoa Shilingi laki tatu, huku wananchi wanaopenda timu hiyo watakuwa wanatoa Shilingi laki moja.
“Daimond amekuwa akimkubali sana Boban na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anarejea uwanjani kwa kasi ndio maana ameamua kujitolea kwa kutoa mshahara wake nusu,” alisema kiongozi huyo.
Katika mechi yao ya juzi waliyoicheza Uwanja wa Makurumla uliopo Magomeni Mwembe Chai, Dar es Salaam, dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walishinda bao 1-0, Diamond alitoa Shilingi laki tano kama kuwatia moyo kujituma kwa bidii wakati wote wa mechi hiyo iliyokuwa ya kuvutia.

Prof Tibaijuka akataa kujiuzulu " Asema hana hatia

Tibaijuka


Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.


Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka.

Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2015 yatangazwa

Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza  mwakani  kutokana na matokeo ya darasa la saba  ambapo wanafunzi  427,60 kati ya  844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi  844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.
Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.

Mahakama nchini Uingereza yamnyima haki ya kufanya tendo la ndoa na MkeweMahakama nchini Uingereza imemzuia mwanamume mmoja kufanya tendo la ndoa na mke wake ambaye ana matatizo ya kiakili kwa sababu hana uwezo wa kutoa ruhusa kwa mumewe.

Mwanamke huyo mwenye urmri wa miaka 39 ana ugonjwa wa kiakili wa kiwango cha nne na saba na ni mke mwenza wa mwanamke wa mke wa kwanza wa mumewe.

Mama huyo ana watoto wanne na kwa sasa na yuko chini ya uangalizi wa kituo cha afya kinachowashughulikia wagonjwa wenye matatizo ya akili.

Lakini jaji aliambiwa aamue iwapo anaweza kurejea kwa mumewe wa miaka 18 ambaye anataka kumwangalia katika nyumba yao ya mjini London.

Mume huyo anayejulikana kama SA alihoji kwamba ni haki yake kufanya tendo la ngono na wakeze,iwapo wana akili timamu ya kuweza kukubali na kwamba ni jukumu lao kukubali.

Alitaka mwanamke huyo kurudi nyumbani ili aweze kutekeleza tendo la ngono na wake zake wawili kwa siku tofauti.

Lakini Jaji Justice Mostyn ambaye alisema kuwa ndoa ya wake wengi chini ya sheria ya kiislamu ni halali lakini ni haramu nchini Uingereza aliamuru kwamba mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina TB hana akili timamu ya kufanya uamuzi wa kutenda tendo la ngono,na kwamba si vyema yeye kurudi nyumbani.
Wana ndoa


Alisema:''Ushahidi unaonyesha wazi kwamba TB hajui tishio la kiafya linalomkabili.Alishindwa kulinganisha uja uzito na tendo la ngono.Mwathiriwa hajui vile watoto wake waliovyoingia katika tumbo lake kama anavyoeleza.Ijapokuwa alifurahia tendo la ngono hakujua kwamba alikuwa na haki ya kuchagua na kukataa. Kwa kweli tabia ya SA,kama ilivyo katika utamaduni na dini yake ni kwamba ana haki ya kutaka kufanya tendo la ngono na wakeze na kwamba wanawake hao wana jukumu la kukubali''.

Jaji huyo amesema kuwa juhudi za kumuhamasisha TB kuhusu tendo la ngono ,haki zake na hatari iliopo zimefeli.

Aliongezea kuwa TB licha ya kuwa amepata watoto wanne na mke huyo bado angepenbda kufanya tendo la ngono naye.

Maelezo ya hatua hiyo yamepatikana katika uamuzi uliondikwa na jaji huyo baada ya kusikilizwa katika mahakama ya utetezi ambayo inatathmini maswala kadhaa yanayohusiana na watu wagonjwa na wasioweza kujitetea.

Jaji Mostyn alikuwa ametakiwa kufanya uamuzi na shirika la London la Borough of Tower Hamlets linalosimamia maswala ya wanawake.

Mahakama iliambiwa kuwa wana ndoa hao walikuwa na uhusiano wenye utata na kwamba kulikuwa na wakati wa ghasia za kinyumbani wakati mume anapokuwa na hasira.

Wednesday, 17 December 2014

Mwanafunzi afia gesti akitoa Mimba

Wanafunzi wakielekea Shule
MWANAFUNZI  wa kidato  cha tatu katika shule ya Sekondari ya Tongoni nje kidogo ya jiji la  Tanga,  (jina tunalihifadhi) amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe mwanafunzi huyo alikutwa amekufa juzi katika nyumba ya kulala wageni iliyopo barabara ya 21 jijini Tanga.
Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kwamba mwanafunzi huyo aliingia saa 4.00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba.
“Baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye alituuliza kama wameingia mwanafunzi huyo na mwenzake, tulipomwonyesha chumba  walichoingia naye akakodi chumba cha jirani ndipo tukaona wote wakijifungia kwenye chumba kimoja,” alisema mhudumu.
Mhudumu huyo alisema baada ya muda wa saa moja, mvulana na mzee huyo wakaaga kwamba wanatoka huku wakisema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika. Akithibitisha habari hizi, Kamanda Massawe alisema taarifa ya tukio hilo ilitolewa na mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni Jijini Tanga.
“Tatizo ni kwamba nyumba hii ya wageni wahudumu wake hawakuwapa wageni hao daftari ili waorodheshe majina yao hivyo inakuwa vigumu  kuwafahamu,” alisema Kamanda Massawe na kufafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja.
Kamanda Massawe alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.

Nape akiri madudu ya CCM yawanufaisha UKAWA uchaguzi wa serikali za mitaa

Nape
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kilifanya makosa katika baadhi ya maeneo ambayo yamekigharimu na kusababisha wananchi kupiga kura za hasira kukiadhibu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi huo ambao umeonyesha kuvinufaisha vyama vya upinzani kupitia umoja wao wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Nape alisisitiza kwamba makosa hayo ndiyo yaliyosababisha wapinzani kujinyakulia mitaa kadhaa kwa wepesi.
“Tumejifunza na tumekuwa tunajaribu kila wakati kubadili mfumo wetu wa kura za maoni lakini bado kumekuwa na matatizo. Kwa mfano, kuna Mtaa Mwenge Dar es Salaam, wanaCCM waliamua kumchagua mgombea wa upinzani baada ya jina la waliyempenda kutorudi,” alisema Nnauye na kuongeza:
“Tunajua kwamba kuna maeneo mengi ambayo wapinzani wameshinda. Ukiangalia CCM tulifanya makosa katika kumweka mgombea, hivyo kusababisha hasira ambazo kwa kweli zimewafurahisha wapinzani lakini sisi zimetugharimu,” alisema.
Alisema chama chake kitafanya tathmini ili kubaini kama sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kupoteza baadhi ya mitaa.
Hata hivyo, Nape alisema wapinzani hawapaswi kuufurahia ushindi walioupata, bali iwe ni changamoto kwao katika kuhakikisha wanawatumikia wananchi waliowaamini

Mechi ya nani mtani jembe yambebesha virago Maximo

Mechi ya Mtani Jembe nchini Tanzania, inayozikutanisha timu mbili za jijini Dar es Salaam zenye ushindani wa jadi, za Simba na Yanga imegeuka uwanja wa machinjio kwa makocha wa Yanga kwa mara ya pili mfululizo.
Mechi kama hiyo ilipofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa magoli 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi. Mwaka huu ni zamu ya kocha Marcio Maximo kufungashiwa virago vyake baada ya kunyukwa mabao 2-0 katika mechi ya Mtani Jembe iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na huu ukiwa ni mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba tu ya ligi kuu ya Vodacom ya nchi hiyo.
KOCHA Maximo ambaye alipokelewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki na wanachama wa Yanga mwezi Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu yao, amewaaga rasmi wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwambia kuwa kuanzia hiyo jana hakuwa kocha wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda.
Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."
Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi".
Mchezaji mwingine wa timu hiyo alisema "Hakuna mchezaji kwa kweli aliyependezwa na kitendo cha uongozi, yaani kwenye mazoezi asubuhi ilikuwa kama msiba, 'mood' ya kufanya mazoezi iilisha kabisa, yaani hakuna aliyekuwa na hamu ya kuendelea na mazoezi.
"Tumefanya kidogo mazoezi tukaondoka, ukiangalia ni sawa tumefungwa cha muhimu ilikuwa ni kukaa chini na kuzungumza na kuangalia cha kufanya, kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi, mimi sijaona haja ya kumfukuza kocha hasa kipindi kama hichi."
Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh alikiri Maximo kuwaaga wachezaji kabla ya mazoezi ya timu hiyo kwanza akiwapa moyo wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali.
"Kwa kweli inasikitisha hakuna mchezaji wala mtu aliyefurahia, kama yupo labda kimoyomoyo ila dah imetuumiza, ni mazoea cha muhimu tugange yajayo hayo mengine tuwaachie viongozi."alisema Saleh
Mchezo wa Mtani Jembe ambao ni wa kujifurahisha na kuongeza utani kati ya timu hizo, umegeuka kuwa kipimo cha ubora wa kocha hata kama kocha huyo anafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu. Hadi wakati anafukuzwa, kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo, timu yake inashika nafasi ya pili baada ya Mtibwa inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na michezo saba tu iliyochezwa.
Baadhi ya mashabiki wameunga mkono uamuzi wa kumtimua Maximo wakisema timu haikuwa na uwezo wa kupambana na timu pinzani, huku wengine wakipinga uamuzi huo kuwa haukustahili kuhukumu uwezo wa kocha huyo katika mchezo mmoja wa kirafiki na kusahau nafasi inayoshikiliwa na timu katika msimamo wa ligi kuu.

Chelsea yatinga nusu fainal Capital One

Chelsea, wakicheza katika uwanja wa iPro Stadium waliwachabanga timu ya Derby County, Bao 3-1 kwenye Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup, na kutinga Nusu Fainali.
Eden Hazard, ndie alianza kuipatia Chelsea, goli la kwanza dakika ya 33 kabla ya Filipe Luis, kufunga goli la pili dakika ya 56 huku Andre Schurrle, akihitimisha ushindi kwa goli la dakika ya 82.
Bao la kufutia machozi kwa Derby lilifungwa na Craig Bryson, Dakika ya 71.
Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali Sheffield United, waliwashangaza Southampton kwa kuwabanjua Bao 1-0.
Bao la ushindi la Sheffield lilifungwa na McNulty, Dakika ya 63. Southampton walibaki 10 baada ya Gardos kupewa Kadi Nyekundu.
Leo Usiku zitachezwa Robo Fainali nyingine mbili ambapo Liverpool, watakuwa Wageni wa Bournemouth.
Huku katika uwanja wa white Hart Lane Tottenham Hotspur watawakaribisha Newcastle United.

Wananchi waandamana kumwondoa Rais wao huko Haiti

Rais wa Haiti Michel Martelly
Mamia ya raia wa nchini Haiti wameandamana katika mitaa ya Port-au-Prince wakishinikiza Rais Michel Martelly kuondoka madarakani.
Hata hivyo maandamano hayo yamegeuka vurugu baada polisi kutumia mabomu ya mchozi kuwatawanya waandamanaji hao. polisi wamepambana na waaandamanaji hao ambao wamekuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi mitaani.
Madai ya raia hao ni kumtaka Rais Martelly kuitisha uchaguzi na kuunda serikali,ambapo uchaguzi ulitakiwa kuitishwa miaka mitatu iliyopita.
Waziri mkuu wa Haiti Laurent Lamothe, siku ya jumapili aliamua kuachia ngazi baada ya shinikizo la siku mbili.Maoni kutoka vyama vya upinzani ni kwamba wanamtaka rais Martelly kujiuzulu. Awali Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameitaka Hait kuitisha uchaguzi mara moja.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana, Jumanne, kufuatia sakata la uchotaji wa fedha kutoka akaunti ya ESCROW ambapo zaidi ya dola milioni 120 zilihamishwa.
Mwanasheria mkuu, pamoja na baadhi ya wanasiasa na maafisa waandamizi wa serikali walituhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha kufanyika kwa miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta.
Leonard Mubali ameandaa taarifa ifuatayo:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali.
Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Jaji Werema amesema ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali ilipeleka pendekezo kumtaka Jaji Werema kuwajibika
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe
Kamati hiyo ya Bunge pia ilipendekeza kuwa waziri wa Nishati na Madini, waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwanasheria mkuu, katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
Pia maazimio ya Kamati ya kudumu ya bunge ilipendekeza kuwa, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na makampuni binafsi imeisababishia Tanesco hasara ya mabilioni ya fedha na kutishia uhai wake wa kifedha, serikali iwasilishe mikataba husika bungeni au kwenye kamati zake kwa lengo la kutekeleza vema wajibu wake wa kuimamia na kuishauri serikali.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana

Monday, 15 December 2014

Diamondi awakera wasanii wa Kenya

Diamond awakera wasanii wa KenyaMsanii maarufu wa Tanzania Diamond amewakera wasanii kutoka mji wa Mombasa akiwemo msanii mashuhuri Nyota Ndogo

Diamond ambaye aliwatumbuiza mashabiki wake katika tamasha lililoandaliwa mjini Mombasa aliwakera wasanii wenzake kutoka Mombasa akiwemo nyota wa pwani Nyota Ndogo.

Diamond anasemekana kumwomba mwandalizi wa tamasha hilo kuwaondoa wasanii wote waliokuwa katika sehemu ya VIP wakiwemo wasanii mashuhuri Susumila na Nyota Ndogo.

Wasanii mjini Mombasa waliungana kumkashifu Diamond na mwandalizi wa tamasha hilo huku DJ Delph akisusia kuhudumu katika tamasha hilo.

Wasanii hao walisema kuwa lilikuwa jambo la kusikitisha kuona kuwa wasanii kutoka pwani ya Kenya walibaguliwa wakiwa nyumbani.

Ushabiki wamtia matatani mwanamke huko Saudi ArabiaMchezaji na shabiki sugu wa soka mwanamke nchini Saudi Arabia, amejipata mashakani baada ya kuingia katika uwanja uliokuwa na mashabiki wanaume.

Viwanja vya soka nchini humo vina masharti yake , kwani wanawake na wanaume hawaruhusiwi kuchanganyikana.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, shabiki huyo mwanamke aliingia uwanjani akiwa amevalia kama mwanamume.

Aliingia uwanjani akiwa amevalia kofia kubwa iliyokuwa imefungwa na kitambaa cheusi cha kujitanda kichwani pamoja na mavazi meupe ya timu iliyokuwa inacheza ugenini.

Alikaa mbali na mashabiki wengine wanaume akiwa peke yake kazingirwa tu na viti.

Lakini hapo ndipo unga ulizidi maji kwani aliweza kutambuliwa

Polisi walimkamata na kusema kuwa watampeleka kwa maafisa wakuu.

Lakini raha aliyoipata shabiki huyo sugu licha ya masaibu yake ni kwamba klabu aliyokuwa anashabikia iliibuka na ushindi.

Mfanyakazi wa ndani aliyemtesa mtoto Unganda ahukumiwa kwenda jela Miaka 4

 Jolly Tumuhirwe apatikana na hatia ya kumtesa mtoto mdogo na kufungwa jela miaka 4
Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya kwa kumchapa mtoto wa mwajiri wake, amehukumiwa jela miaka minne kwa kosa la kumtesa mtoto.
Kisa cha yaya huyu kilizua hasira miongoni mwa watu wengi katika mitandano ya kijamii pale kanda ya video iliibuka mitandaoni ikimwonyesha yaya huyo akimchapa na kumkanyaga mtoto mwenye mwaka mmoja unusu.
Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, alinaswa kwa kamera ya siri akionekana akimchapa na kumkanyaga mtoto huyo pamoja na kumzaba kofi.
Mnamo siku ya Ijumaa, Jolly alikiri kumshambuilia mtoto akisema alikuwa analipiza kisasi kwani mamake mtoto huyo naye alikuwa amezoea kumchapa.
Hata hivyo mama huyo alikanusha madai ya Jolly ambaye polisi walikuwa wamesema wangemshitaki kwa kosa la jaribio la mauaji ila kiongozi wa mashitaka akasisitiza kuwa ingekuwa vigumu kuthibitisha hilo.
Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha kulingana na makosa yake kwa kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi alisema aliweka kamera ya siri nyumbani kwake baada ya kuwa na shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya video iliyomuonyesha Jolly akimtendea unyama mtoto, ilitoka kwenye kamera ambayo Bwana Kimanzi aliweka nyumbani kwake baada ya kushuku kuwa mtoto wake alikuwa anatendewa unyama na pia baada ya kumapata mtoto wake akiwa na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa polisi na kisha kuisambaza kanda hio kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi alisema: "sio juu yetu kuamua adhabu anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai kuwa hili ni funzo kwa wafanyakazi wengi wa nyumbani kwamba huwezi tu kwenda kwa nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na kutarajia kuondoka tu kama ulivyoingia. ''

Tetesi za usajili UlayaManchester United wanataka kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Gareth Bale, mwenye miaka 25, toka klabu ya Real Madrid kwa dau la £90milion, pesa za mauzo ya Bale zitatumika kuwasajili nyota Eden Hazard wa Chelsea na kinda wa Liverpool Raheem Sterling.

Kocha wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier, ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo wa timu ya New York Red Bulls yuko tayari kumpa ofa kiungo Steven Gerrard kujiunga na miamba hao wa ligi ya Marekani.

Manchester City imeingia katika vita na timu ya Manchester United katika mbio za kuwania saini ya mlinzi kisiki Mats Hummels, wa klabu ya Borussia Dortmund,Man City wako tayari kutoa kitita cha £47milioni ili kumtwaa mchezaji huyo.

Klabu yaTottenham wanafanya jitihada za kumsajili mshambuliaji Eran Zehavi, toka timu ya Maccabi Tel-Aviv inaaminika mchezaji huyo anapatika kwa kwa dau la £1.6milioni. Tottenham wanataka kuondoa tatizo la safu ya ushambuliaji inayoshindwa kufanya vizuri msimu huu.

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amewataka Reds na meneja Brendan Rodgers kutoa £ 20milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Wilfried Bony mwenye 26, toka Swansea katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Inter Milan wanapigana vikumbo na Ajax pamoja naReal Sociedad kuwania kupata nafasi ya kumchukua kwa mkopo winga kinda Adnan Januzaj. Manchester United wako tayari kumuachia winga huyo mwenye miaka19, akapate uzoefu Zaidi baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Miss wa Afrika kusini ashinda Miss worldMiss South Africa Rolene Strauss ameibuka mrembo wa dunia wa mashindano ya Miss World 2014, akiwashinda zaidi ya warembo 120 katika shindano lililofanyika jijini London, Uingereza.

Mshindi huyo wa shindano la Miss World 2014 alivikwa taji la urembo na mshindi wa Miss World 2013, Megan Young kutoka Ufilipino na kushangiliwa na mshindi wa pili na wa tatu, ambao ni Miss Hungary Edina Kulcsรกr na Miss Marekani Elizabeth Safrit. Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa mtandao wa Internet, mshindi huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya udaktari na anafurahia kucheza michezo ya golf, netboli na kuendesha baiskeli na kujisomea vitabu vya burudani na elimu.

Washindi wa tano wa mwanzo katika mashindano ya urembo ya mwaka huu walikuwa kutoka Uingereza, Marekani, Hungary, Australia na Afrika Kusini.

Shindano la Miss World 2014 pia lilikuwa na mshindano tanzu na mataji mengi, ambayo yalifanyika kuelekea siku ya fainali kuu.

Kwa mara ya kwanza, washindani watano walitangazwa kuwa Warembo wa Miss World 2014 wenye Lengo: Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss Brazil, Miss Indonesia and Miss Guyana

Thursday, 11 December 2014

Baskeli ya tengenezwa kwa dhahabu

Baiskeli ya dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni
Ni rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununu baisekli wengi wakitaka bei nafuu. Nyingi ya baiskeli nchini Uingereza huuzwa kwa pauni 1,000 shilingi lakini moja na arobaini pesa za Kenya.
Kwa wengi nchini humo hizo ni pesa nyingi sana.
Gia za baikeli hii zimetengezwa kwa dhahabu
Hata hivyo baikeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni laki mbili na hamsini au milioni 36,250,000 pesa za kenya. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la Ferari, kukufahamisha tu.

Baiskeli hio ambayo ilitengezwa na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie imetengezwa kwa dhahabu kutoka kwa mikono na vyuma vyake vyote. Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24.
Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.
Mkurugenzi w akampuni iliyotengeza baiskeli hii anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo
Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkrugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.
"baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.''
Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,'' aliongeza kusema mkurugenzi huyo.
Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.

Saturday, 6 December 2014

Danny Sserunkuma (Simba) na Emerson Oliveira wawakuna wengi

Simba yamnasa Danny Sserunkuma.
katikati ni Dany sserukuma
Usajili wa nyota wapya wa kigeni umegeuka kete ya ushindi kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe 2 baina ya Simba na Yanga inayotarajiwa kuchezwa Desemba 13 jijini Dar es Salaam.
Jana, viongozi wa klabu hizo walitambiana, wakiwataja nyota wao wapya, Danny Sserunkuma (Simba) na Emerson Oliveira kuwa ndio wataziwezesha klabu zao kuibuka na ushindi.
Wakizungumza kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Simba ilijinasibu kuwa imesajili mtambo wa mabao, wakati Yanga ikijibu kuwa itamweka mfukoni kupitia kiungo wao, mpya Mbrazili Emerson.
Msemaji wa Simba, Humphrey Nyasio alisema: “Sisi ndiyo mabingwa watetezi wa Nani Mtani Jembe, tulishinda mabao 3-1 mwaka jana, hivyo kwa mwaka huu tutatoa kipigo kikali zaidi kwani tumesajili mtambo wa mabao ambao utaanza kazi siku hiyo, tumemsajili Sserunkuma, kazi kubwa iliyomleta hapa ni kufunga mabao, hivyo Yanga wajiandae kuona moto wake,” alisema msemaji huyo.
Meneja masoko wa Yanga ambaye aliiwakilisha klabu hiyo, George Simba alijibu: “Sisi tutahakikisha pesa zote, Sh80 milioni tunazoshindania tunazipata, pia, tunapata kombe na ushindi kwenye mchezo huo.
“ Pia, mashabiki wetu wajiandae kupata vionjo vipya vya Kibrazili na ujio wa Emerson utaigaragaza Simba na kuandika historia mpya,” alisema meneja huyo.
Wakati hayo yakiendelea, wapenzi wa Yanga wamewafunika wale wa Simba kwenye upigaji kura za kuwania Sh80 milioni za kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo hukamilika kwa mchezo baina ya Simba na Yanga.
Matokeo yaliyotangazwa jana na meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli yanaonyesha kuwa Yanga tayari wamejinyakulia Sh70 milioni wakati Simba wanazo Sh10 milioni.
Naye Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe alisema: “Tayari, Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe 2, zimeahidi kuwatumia wachezaji wa vikosi vya kwanza, wakiwamo wale waliopo kwa kipindi kirefu na wale waliosajiliwa.”
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alitangaza viingilio vya mchezo huo akisema Jukwaa la VIP A itakuwa Sh30,000, VIP B Sh20,000, huku VIP C ikiwa ni Sh15,000.
Kwa upande wa viti vya rangi ya chungwa tiketi ni Sh15,000 huku kwa upande wa viti vya rangi ya bluu na kijani kiingilio kitakuwa ni Sh7,000.
Pia Wambura aliongeza kuwa kama ilivyo kawaida ya pambano hilo, hakutakuwa na muda wa nyongeza, iwapo timu zitakwenda sare ndani ya dakika 90, mshindi atapatikana kwa penalti.

Zitto atamani kurudi chadema ila awapa masharti

Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na chama chake cha zamani Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.
Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa “akimiss” harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.
Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini hakudokeza lolote kuhusu Chadema.
Hata hivyo, mapema wiki hii, Zitto, ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa nyadhifa zote kwenye chama hicho kwa tuhuma za kukihujumu, lakini akafanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe.
Baada ya kuongoza PAC kuchunguza wa tuhuma za Escrow na kufanikiwa kulishawishi Bunge kufikia maazimio manane ya kuwashughulikia kisheria wahusika kwenye uchotwaji huo wa fedha, kumekuwapo na wito kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema kutaka pande hizo mbili zimalizane.
“Kabla ya jambo lolote kufanyika, ili kukata kiu ya Watanzania wanaotaka kuona tunaondoa tofauti zetu, ni lazima kusema ukweli na kila upande kuwa tayari kuomba radhi hadharani pindi ikibainika ulifanya makosa,” alisema Zitto alipotakiwa kuzungumzia harakati hizo za kumrejesha Chadema.
“Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini? Lakini mimi ninaona sina kosa ndani ya Chadema. Ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka makosa yangu mimi ni nini,” alisema na kuongeza:
“Nitakuwa tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa na kama ikibainika chama kilifanya makosa, nacho kiwe tayari kuomba radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano.
“Kama hakutakuwa na ukweli itakuwa vigumu kupata mwafaka. Mimi sina tatizo. Nirudie nilivyosema bungeni kuwa nina-miss sana (ninapenda sana kuwamo kwenye) harakati za mageuzi kipindi hiki za kuiondoa CCM madarakani.”
Katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto alisema: “Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu. Napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia watambue kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki.
“Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina; waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu; na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka.”
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye binafsi aliguswa na mzozo huo, hakuwa tayari kuzungumzia kumaliza matatizo baina ya chama na Zitto.
 (sina maoni) kwa hilo. Siwezi kuzungumzia suala hili katika media (vyombo vya habari),” alisema Mbowe
Hoja ya kutaka Zitto arejeshwe Chadema imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii na kwa baadhi ya wanasiasa baada ya kuonekana kuwa karibu na viongozi wa chama chake wakati Kamati ya PAC ilipoibua ufisadi wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow wiki iliyopita.
Wakati akihitimisha mjadala wa sakata la Escrow, mbali na kueleza bayana kuwa alifurahia kuhudhuria vikao vya Ukawa kwa mara ya kwanza, Zitto alikwenda mbali na kumpongeza “kwa namna ya pekee” Mbowe kwa jinsi walivyoshirikiana katika sakata hilo.
Zitto alisema hilo lilikuwa ni jambo la kitaifa ndiyo maana wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama vyao waliungana.
Alisema mara baada ya sakata hilo kumalizika watu mbalimbali wamekuwa wakizungumzia kufanyika kwa maridhiano ili awe sehemu ya Ukawa na kwamba haoni tatizo.
“Katika hili, kipekee namshukuru kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniunga mkono katika sakata hili,” alisema Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema: “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”
Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema:
“Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo na kuanza upya harakati.”
Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema, “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”
Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema: “Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo na kuanza harakati.”

ICC yatupilia mbali kesi dhidi ya Rais wa kenya Uhuru Kenyatta

Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008.
Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la inagwa alisema muda huo haukutosha kwake yeye kuandaa ushahidi zaidi dhidi ya Kenyatta.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni naibu Rais kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Zaidi ya watu elfu moja waliuawa wakati wa ghasia hizo. Uhuru alikuwa mtu maarufu zaidi kufikishwa mahakamani na pia mshukiwa mkuu kwani alifikishw amahakamani akiwa Rais aliye mamlakani.
Hili ni pigo kubwa kwa upande wa mashitaka, wengi wlaioana keshi dhidi ya Kenyatta kama mtihani mkubwa katika historia ya mahakama hio.
Upande wa mashitaka ulitaka mahakama kuupatia muda zaidi ili upate ushahidi zaidi,dhidi ya Kenyatta kama vile taarifa za akaunti yake ya benki.
Upande wa utetezi uliteta kuwa ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha kesi hio inapaswa kutupiliwa mbali.

Tetesi za usajili ulaya

joel campbel
ManchesterUnited inaweza kutumia mpaka kiasi cha pauni milioni 350 kwa kipindi cha miaka miwili katika kusajili wachezaji wapya.
Hii inaweza kufikiwa kama watafanikiwa kuwasajili kiungo Kevin Strootman 24,toka roma, na beki wa Borussia Dortmund Mart Hummels, 25,pia inasadikika kocha Louis van Gaal anamtaka beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne, 23.
Arsenal wako tayari kurekebisha safu yao ya kiungo kwa kumuwania kiungo Morgan Schneiderlin, toka Southampton kwa dau la pauni milioni 15 pia wako tayari kutoa pauni milioni 8 kwa beki Tyrone Mings, 21,wa Ipswich Town.
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard
Inter Milan wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambulaiji Joel Campbell, wa Arsenal raia wa Costa Rica pamoja na kiungo wa Tottenham Erik Lamela 22.
Henrique Pompeu wakala wa mshambuliaji wa Colombia Jackson Martinez 28, ameeleza kuwa mteja wake huyo hato ondoka katika timu yake ya Fc Porto japo timu za Arsenal, Liverpool and Tottenham zimekua zikimuwania.
Meneja wa Newcastle Alan Pardew, anawasiwasi nyota wake Moussa Sissoko,ataondoka St James' Park kuelekea Arsenal katika usajili wa dirisha dogo mwezi januari.
Real Madrid na Paris St-Germain wanapigana vikumbo kuweza kupata saini ya mshambuliaji Eden Hazard.Huku chelsea wakiwa tayari kumboreshea kandarasi yake ya sasa nyota huyo wa ubelgiji mwenye miaka 23.
Kiungo wa kibrazil Luca Silva,21,anayechezea klabu ya Cruzeiro yuko tayari kuzikata ofa za Manchester United na Arsenal ili kujiunga na miamba wa hispania Real Madrid.
Timu Leicester City itajaribu kutaka kumrejesha tena kwenye ligi ya Epl mshambuliaji Jermain Defoe, 32,toka klabu ya Toronto Fc.

Thursday, 4 December 2014

Phedejee azikwa ndani ya gari la kifahari Nigeria

Picha za mtu aliyezikwa ndani ya gari lake la Hummer SUV jeep nchini Nigeria
Katika siku za hivi karibuni picha za mtu ambaye alizikwa ndani ya gari aina ya Hummer SUV Jeep nchini Nigeria zimekuwa zikienea katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo.
Picha hizo zilitoka katika mtandao wa twitter wa msichana mmoja raia wa Kenya anayetumia jina @Sankorie katika mtandao wake ambaye alishangazwa na kusema kuwa wanaume wa Nigeria ni matajiri hadi wengine huzikwa ndani ya magari yenye thamani ya juu,swala ambalo haliwezi kufanyika nchini Kenya.

Mwanafunzi aliyekua ana nadi ubikra akoma

Mwanafunzi anayesomea udaktari nchini Marekani ambaye alikuwa ana nadi ubikra wake, amesitisha shughuli hiyo baada ya watu wachache sana kujitokeza wakiwa tayari kuulipia ubikra wa mwanamke huyo.
Pamoja na hilo Kern hakua na uhakika kuhusu ukweli wa waliojitokeza kulipia ubikra wake.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Daily Mail.
Mwanafunzi huyo, Hanna Kern alikuwa ana nadi ubikra wake chini ya jina ambalo sio lake 'Elizabeth Raine' kwa hofu ya watu kumtusi. Pia hakuweka sura yake kwenye mtandao hadi alipofanya mahojiano na jarida la Haffington post.
Kern ana umri wa miaka 28 na ana digrii ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Washington, nchini Marekani.
Kern ni mwanafunzi wa hivi karibuni aliyenadi ubikra wake kwenye mtandao bila matokeo aliyoyataka.
Hata hivyo alilazimika kuusitisha mnada wake baada ya kukosa kupata kima alichokitaka na hata pia kukosa kupata wanaume wengi waliovutiwa na kampeini yake na kuhofia kuwa waliojitokeza kuulipia sio watu wakweli.
Pia alieleza kuwa alisumbuka sana kiakili kutokana na umaarfu aliopata baada ya kufichua jina lake la kweli na kuonyesha sura yake.
Alikunukuliwa akisema baada ya kukosa kufanikiwa kupata hela alizozitarajia, hana wasiwasi na hilo kwani amapeta funzo na kujua kwa nini kampeini kama hizi huwa kazifanikiwi.
Wa mwisho aliyejitokeza kulipia ubikra wake alikuwa ametoa kima cha dola 801,000,lakini mwanafunzi huyo aliamua kutoendelea na juhudi zake kwani hakufurahishwa na pesa hizo.
''Nimeamua kusitisha kempeini yangu, na kurejea katika msomo yangu ya udaktari.''
''Bado ninaamini kuwa ubikra ni kitu kizuru na pia ninaamini kuwa mwanamke anapaswa kuachwa afanye anavyotaka, '' ingawa kwa sasa masomo ndio ninayotaka kushughulika nayo,'' alisema Kern.