Joe na mwenzake Brown wakifunga ndoa nchini Uskochi |
Harusi ya kwanza ya watu wa jinsia moja imefanyika huko Uskochi .
Joe
Schofield na Malcom Brown walifunga ndoa katika sherehe iliofanyika
katika eneo la Trade Hall Glasgow huku Susan na Gerrie Douglas -Scott
wakifanya harusi yao katika eneo la faragha mjini humo.Sheria hiyo mpya ya watu wa jinsia moja ilianza kufanya kazi Uskochi mapema mwezi huu.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na waziri wa kwanza wa Uskochi.
Susan na mwenzake Gerrie wakifanya ndoa yao huko Uskochi |
Susan mwenye umi wa miaka 54 na Gerrie Douglas-Scott mwenye umri wa miaka 59 wanaishi mjini Galsgow ambapo walikutana miaka 18 na wana watoto wakubwa watano.
Walioana mwaka 2006 na kuamua kufanya sherehe mwaka huu.
No comments:
Post a Comment