Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia
huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na
kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo
alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo
alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.
No comments:
Post a Comment