Thursday 31 July 2014

Maporomoko yafunika kijiji huko India


maporomoko India
Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.

Vijidudu hatari vya malaria vyagundulika


Mbu wa Malaria
Watafiti wametoa tahadhari kuwa vijidudu vya malaria visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika maeneo ya mpakani kusini mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi ya Malaria.
Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudia
matibabu baada ya kukumbana na maambukizi inaweza kusaidia kupambana na kusambaa kwa Malaria katika Asia na baadae Afrika ndani ya muda mfupi. Mamia ya maelfu ya watu hufariki kutokana na Malaria kila mwaka hasa katika Afrika.

Wednesday 30 July 2014

Al shababu yaua mwanamama kwa kutojifunga Niqab

Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga niqab kichwani.
Jamaa za mwanamke huyo mwenyeji wa mji wa Hosingow kusini mwa Somalia wanasema mwanamke huyo alikataa kujifunika kitambaa kichwani kuambatana na sheria za dini ya kislamu .
''alikuwa ameonywa ajisitiri lakini wapiganaji hao waliporejea wakashikwa na hasira walipopata kuwa hakuwa amejifunika na hivyo wakampiga risasi''.

Al Shabab yaua mama kwa kukosa Niqab
Jamaa zake wameiambia shirika la utangazaji la BBC kuwa Ruqiya Farah Yarow alikuwa amewafokea wapiganaji hao akiwataka waondoke kwake na kusema kuwa angejisitiri baadaye.
Kundi la Al Shabab linalomiliki asili mia kubwa ya maeneo ya Kusini na Katikati ya Somalia na limekuwa likishinikiza kutumiwa kwa sheria kali za kiislamu.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo amekanusha kuwa ni wao waliomuua mwanamke huyo .
Msemaji huyo anasema kuwa licha ya kudhibiti maeneo makubwa nchini humo kundi hilo bado halijatoa maelezo ya vipi wanawake wanastahili kujisitiri.

Mwanamke ajinyonga huko Tabata

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Irene Ibrahim (22), mkazi wa Tabata Kisukuru manispaa ya Ilala, amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema marehemu alikutwa kwenye shamba la Abdallah Mshindo akiwa amejinyonga kwa kutumia khanga aliyoitundika katika tawi la mti aina ya mjohoro.
Minangi alisema, tukio hilo lilitokea Julai 27 majira ya saa 1 usiku, ambako Irene alifika kwenye duka la Oliver Laurent akiwa amebeba pombe tatu aina ya viroba na dawa aina ya Mifupain nyingi mkononi huku akiwaeleza baadhi ya watu kuwa, atasafiri kwenda Amerika kisha kuingia chumbani kwake.
Alisema, baada ya kuingia chumbani kwake, hakuonekana tena mpaka walipoangalia chumbani kwake walikuta maganda ya viroba na dawa bila yeye kuwepo, ndipo alipokutwa akiwa amejinyonga shambani hapo.
Katika tukio jingine, mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga mti.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Camillius Wambura, alisema ajali hiyo ilitokea Julai 28 majira ya saa 8 usiku eneo la Masaki Kata ya Msasani, Kinondoni barabara ya Kimweri iliyohusisha gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T422 AXV iliyokuwa inaendeshwa na dereva anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 20-25.
Wambura aliongeza kuwa, gari hilo lilikuwa linatokea barabara ya Ally Hassan Mwinyi kwenda Coco Beach ndipo lilipoacha njia na kugonga mnazi uliyokuwa kandokando ya barabara  hiyo.

Tuesday 29 July 2014

Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba (IMTU) wafunguliwa kesi ya Viungo vya binadamu

Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha IMTU wakiwa mahakamaniWAHADHIRI wanne wa Chuo Kikuu cha Tiba cha IMTU, Mbezi Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na makosa mawili, likiwemo la kushindwa kufukia viroba 83 vya viungo vya binadamu.
Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Polisi, Magoma Mtani, mbele ya Hakimu Kwey Rusemwa, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Venkat Subbaiah (57), Appm Shankar Rao (64), Prabhakar Rai (69) na Dinesh Kumar (27).
Magoma alidai kuwa washitakiwa hao Julai 2014 katika eneo la Mpigi Majohe, walishindwa kufukia viroba 83 vya viungo vya binadamu walivyovitumia kufundishia wanafunzi wa udaktari kinyume na kifungu cha 128 cha sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.
Alidai kuwa washitakiwa hao kwa pamoja, pia walishindwa kuandaa hati kwa Kampuni ya Corona ya kuthibitisha kufukiwa kwa mabaki hayo.
Washitakiwa hao walikana mashitaka hayo na upande wa jamhuri ukadai upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Rusema, alisema ili washitakiwa wapate dhamana, kila mmoja awe wadhamini wawili ambao ni Watanzania na wanaofanya kazi kutoka kwenye taasisi zinazotambulika kisheria.
Wakati taratibu hizo zikiendelea, Wakili wa Serikali, Salum Ahmed aliingia mahakamani hapo na kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) ya mwaka 2002 kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Baada ya kuwasilishwa kwa ombi hilo, Hakimu Rusemwa aliwaachia huru washitakiwa hao, lakini muda mfupi baadaye walikamatwa na askari wa Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi mkali na kupandishwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili KXO 6 EFY na Toyota RV4
yenye namba za usajili T 366 AVG na kuondoshwa katika eneo la mahakama.

mwanamke jambazi sugu na wenzake watiwa mbaroni

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao hatari wa majambazi kumi, mmoja akiwa ni mwanamke anayeshiriki kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman KovaAkizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova, alisema majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea katika harakati za kuhakikisha maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
Kova alisema katika msako huo watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi na maficho yao na wakakutwa na silaha tisa ambazo ni bunduki SMG namba 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine mbili, SMG moja bila magazine na namba hazisomeki, bastola aina ya Luger yenye namba 5533K, bastola aina ya Browning yenye namba TZACR83494 S/No.7670 na risasi sita ndani ya magazine.
Alizitaja silaha nyingine kuwa ni shotgun pump action na risasi 55, Marck Iv iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine moja na risasi nne, bastola yenye namba A963858 Browning iliyokuwa na risasi moja, SMG ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic), pamoja na shotgun TZ CAR 86192 ambayo ilitelekezwa baada ya msako.
Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Maulidi Mbwate (23), mfanyabiashara mkazi wa Mbagala Charambe, Foibe Vicent (30), hana kazi mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Vincent Kadogoo (30), mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Said Mlisi (29), dereva wa bodaboda mkazi wa Gongo la Mboto na Hemed Zaga (22), dereva bodaboda mkazi wa Gongo la Mboto.
Wengine ni Mohamed Said (31), fundi kuunga vyuma mkazi wa Kigogo, Lucy Mwafongo (41), mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga, Rajabu Ramadhani (22), mkazi wa Kariakoo, Deus Chilala (30), mgonga kokoto Kunduchi, mkazi wa Yombo Kilakala pamoja na Marietha Musa (18), mkazi wa Yombo Kilakala.
“Mwanamke pekee katika kundi hilo Foibe Vicent ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji na mengine mengi, yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG. Katika baadhi ya matukio, wananchi walioshuhudia wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo,” alisema Kova.

Chadema Yaendelea kujiweka sawa

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi, Benson KigailaKATIKA kuhakikisha uchaguzi mkuu wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), unaendeshwa kwa uwazi na umakini ili kuepuka mitego ya kuchomekewa wasaliti, chama hicho kimejipanga upya na kuusogeza hadi Septemba 14 badala ya Agosti 31.
Hatua hiyo ni baada ya Kamati Kuu kubaini kwamba hakuna chombo cha kuusimamia uchaguzi huo, na sasa imeamua jukumu hilo lifanywe na Baraza la Wazee Taifa.
Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotangazwa jana na Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi, Benson Kigaila, uchaguzi wa Baraza la Wazee ndio utatangulia kufanyika Septemba 6, ili kutoa nafasi kwa chombo hicho kusimamia uchaguzi mkuu.
Kigaila alisema kuwa mkutano mkuu wa kuwachagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti Bara na Visiwani, utatanguliwa na chaguzi za mabaraza ngazi ya kitaifa.
“Hadi kufikia Julai 30, uchaguzi wa kata utakuwa umekamilika na Agosti 15, mwaka huu, uchaguzi wa majimbo na wilaya nao unapaswa kukamilika ili kuruhusu uchaguzi ngazi ya mkoa uanze hadi Agosti 30 mwaka huu,” alisema.
Kigaila alisema uchaguzi wa Baraza la Vijana (Bavicha) utafanyika Septemba 10 huku ule wa Baraza la Wanawake (Bawacha) ukipangwa kuwa Septemba 11.
“Baada ya chaguzi hizo za mabaraza kukamilika, Kamati Kuu ya sasa itakutana Septemba 12 kwa ajili ya kuandaa kikao cha Baraza Kuu kitachaofanyika Septemba 13 mwaka huu, ili kuandaa mkutano mkuu wa Septemba 14,” alisema.
Alisema baada ya mkutano mkuu, Baraza Kuu litakaa Septemba 15 kwa ajili ya kumchagua Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Visiwani ili Kamati Kuu mpya iweze kutambulishana.
Kigaila aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za kitaifa kuchukua fomu kuanzia Agosti 10 hadi 25 katika ofisi za majimbo, wilaya, makao makuu ya mabaraza hayo na ofisi za chama.
Alisema fomu hizo zinaweza kupatikana pia katika mitandao ya mabaraza hayo na chama, lakini alionya kwamba lazima fomu hiyo baada ya kujazwa irejeshwe katika makao makuu ya mabaraza hayo na chama ili iweze kulipiwa.
“Gharama zinazotozwa kwa mgombea wa uenyekiti, katibu, mratibu wa uenezi, mweka hazina na mwenyekiti wa kamati ya uratibu kama kwenye wilaya kuna jimbo zaidi ya moja ni sh. 10,000.
“Gharama za kugombea nafasi ya mwenyekiti, makamu wenyeviti, katibu mkuu, naibu katibu Bara na Visiwani ni sh. 50,000… mratibu wa uenezi na mweka hazina ni sh. 30,000, wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ni sh. 25,000,” alisema Kigaila.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Antony Komu, alisema CHADEMA inatarajia kutumia sh. milioni 700 katika  uchaguzi huo, hivyo aliwataka wagombea  wote kuhakikisha wanalipia fomu baada ya kujaza.
Hata hivyo, aliwaomba wanachama na wapenzi wa chama hicho kujitolea kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi huo ambao alisema utakuwa na watu zaidi ya 1,000 ambao watatoka nje ya Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha, Suzan Lyimo, aliwataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi zinazoendelea ili kuwa na uwiano sawa na wanaume.

Monday 28 July 2014

Shirikisho la soka la Tanzania ndio linalo wanyima ulaji wachezaji

Kwa muda mrefu sasa wapenzi, mashabiki na wadau wa soka wamekuwa wakisema umefika wakati wa kuondoka katika soka la ridhaa na kuingia soka la kulipwa.
Kauli hii ya kuondoka katika soka la ridhaa na kuingia soka la kulipwa imesemwa sana, lakini uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umeshindwa kuifanyia kazi.
Allan Goshashi 
Nasema hivyo

kwa sababu sera ya maendeleo ya michezo ya Tanzania inasema vyama vya michezo vimo katika makundi matatu makubwa ambayo ni (a) vyama vya ridhaa vilivyosajiliwa na msajili wa vyama vya michezo na kujishirikisha na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), (b) Mashirikisho ya michezo ambayo yameundwa na taasisi mbalimbali ili kutoa burudani za kimichezo kwa wafanyakazi, kuwakutanisha wachezaji wao ili wafahamiane, pia kuwashindanisha katika michezo inayohusika na kupata mabingwa wao katika ngazi ya taifa, (c) Vyama vya michezo ya kulipwa ambavyo vimesajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mwaka jana TFF ilifanya mabadiliko ya katiba yake na baada ya hapo iliipeleka BMT ili mabadiliko hayo yapate baraka za BMT hali iliyoonyesha TFF ni chama cha ridhaa kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya michezo ya ridhaa.
Chama cha mchezo wa kulipwa nchini ni Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) ambacho kimesajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Vipo vyama vingine vya ngumi ambavyo vimeingia zaidi kwenye biashara ya ngumi za kulipwa na vimesajiliwa kama makampuni kwa msajili wa makampuni katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Vyama hivyo ni TPBO na PST.
TFF ina wanachama, kushindwa kwake kujisajili kama chama cha mchezo wa kulipwa ndiyo kunaposababisha hata wanachama wake kushindwa kuingia kwenye soka la kulipwa.
Wanachama wa TFF ni pamoja na klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Nakumbuka kuna wakati katika klabu ya Yanga kulikuwa na wanachama wa klabu hiyo waliojulikana kwa jina la Yanga Kampuni waliokuwa wakitaka iendeshwe kama kampuni na wengine waliokuwa wakitaka iendelee kuendeshwa kiridhaa (Yanga-asili).
Wale waliokuwa wakitaka Yanga iendeshwe kama kampuni walishindwa kufikia lengo lao na hata leo wakitaka Yanga iendeshwe kama kampuni watashindwa kwa sababu Yanga ni wanachama wa TFF ambayo imesajiliwa BMT kama chama cha mchezo wa ridhaa.
Ndiyo, tunaweza kuona baadhi ya klabu zinasajili wachezaji kadhaa kwa kuwalipa mamilioni, mishahara mikubwa, kuwapa posho na kuwapangia nyumba, lakini ukweli utabaki bado hatuna soka la kulipwa.
Soka la kulipwa halihitaji wachezaji wachache tu walipwe vizuri, soka la kulipwa ni biashara kubwa katika kuiwezesha klabu husika kutengeneza biashara na vitega uchumi mbalimbali kwa ajili ya kujiendesha kwa ufanisi kisoka na kiuchumi.
Soka la kulipwa ni biashara, klabu zinatakiwa kuuza hisa ili kupata mitaji ya kuanzisha vitega uchumi, pia klabu zinatakiwa kuuza bidhaa zitakazokuwa na nembo ya klabu kama vile kofia, jezi, fulana na vitu vingine vingi kulingana na ubunifu wa klabu husika.

Klabu inapojiendesha kibishara ina maana inaweza kuchukua mkopo benki kama mtaji wa kuanzisha au kuendeleza miradi yake, lakini kwa mfumo huu wa soka kuendeshwa kiridhaa klabu zetu haziwezi kufanya hivyo.
Ni wazi bado tuna safari ndefu ya kuwa na soka la kulipwa kwani pia ni klabu chache ambazo angalau zinaonekana zinaweza kukidhi kigezo cha kuingia katika soka la kulipwa.
Lakini hata hivyo TFF kuendelea kusajiliwa BMT kama chama cha mchezo wa ridhaa kunafanya safari ya kupata kweli soka la kulipwa kuwa ndefu na ndiyo maana naona hatuna soka la kulipwa.

UN wafananisha Utunguliwaji wa ndege ya Malaysia na Ugaidi

Kutunguliwa kwa MH17 huenda ni Uhalifu wa Kivita
Afisa wa umoja wa mataifa anayesimamia haki za kibinaadamu Navi Pilay amesema kuwa kutunguliwa kwa ndege ya kampuni ya Malaysia Airline MH17 mashariki mwa Ukraine huenda ukawa uhalifu wa kivita.
Ukraine pamoja na mataifa ya Magharibi wanaamini kuwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi waliiangusha ndege hiyo kwa kutumia makombora yanayotoka Urusi.
Watu wote 290 walikuwa ndani ya ndege hiyo walifariki.
Hatahivyo waasi hao wamekana kuitungua ndege hiyo.
Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ametaka uchunguzi ulio huru kufanywa kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Mh17.
Ameapa kwamba juhudi zote zitatekelezwa kuhakikish kuwa mtu yeyote ambaye amekiuka sheria ya kimataifa anashtakiwa.
Taarifa hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuwa mgogoro huo umasababisha mauaji ya watu 1,100 huku serikali na waasi hao wakitumia silaha kali katika maeneo yalio na makaazi ya watu.
UN: MH17 huenda ni Uhalifu wa Kivita
Wakati huohuo majeshi ya Serikali ya Ukraine ilipata mafanikio makubwa usiku kucha dhidi ya waasi karibu na mji muhimu wa mashariki mwa Donetsk.
Bi Pillay katika ripoti yake inayohusiana na Ukraine alisema kuwa watu 1,129 wameuawa katika vita hivyo huku 3,442 wakijeruhiwa kutokana na vita hivyo vilivyozuka katikati ya mwezi wa Aprilil.
Wakti huohuo ,msemaji wa wizara ya Usalama wa Ukraine Andriy Lysenko amewaambia waandishi wa habari mjini Kiev kuwa ndege hiyo ya Malaysia MH17 ilianguka baada ya kukumbwa na mlipuko mkubwa ambao ulisababisha vilipuzi kutoboa ndege hiyo.
Msemaji huyo aliongezea kuwa visanduku viwili ya kunasa sauti vya ndege hiyo vinaendelea kupigwa msasa na wataalumu kutoka Uingereza.
Wananchi wakitoroka vita Mashariki mwa Ukraine
Kwa Upande wao Urusi wanasema kuwa wanatarajia walinda usalama wa umoja wa Ulaya OSCE watatumwa katika mpaka wa nchi hiyo na Ukraine ilikulinda amani.
Waziri wa kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema kuwa japo majeshi ya serikali yameingia katika miji ya Shakhtarsk na Torez kunahaja ya kuwepo kwa wachunguzi wa kimataifa baina ya Ukraine na Urusi.
Majeshi ya Ukraine yanasema yanalenga kudhibiti miji ya Pervomaysk na Snizhne yote iliyoko karibu na eneo kulikotunguliwa ndege hiyo ya MH17.

Kombora la tupwa na kulipua Tren ya mafuta libya


Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.

Sunday 27 July 2014

Boko haram wamteka mke wa mwanasiasa


Wanajeshi wa Cameroon
Jeshi la Cameroon linasema kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Nigeria, Boko Haram, limemteka nyara mke wa mwanasiasa mashuhuri kaskazini mwa nchi.
Mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali, na msaidizi wake wa nyumbani, walitekwa katika mji wa Kolofata, karibu na mpaka wa Nigeria.
Inaarifiwa kuwa mapigano baina ya Boko Haram na wanajeshi wa Cameroon yanaendelea.
Boko Haram imefanya mashambulio kadha kaskazini mwa Cameroon; na Jumamosi wafuasi zaidi ya 20 wa Boko Haram walifungwa nchini Cameroon baada ya kukutikana na hatia ya kupanga mashambulio.

Saturday 26 July 2014

Watalii wavamiwa na kuporwa

KUNDI la watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto na mapanga, wamevamia watalii 17 kutoka mataifa mbalimbali na kuwapora kiasi kikubwa cha fedha, kamera na kompyuta mpakato (Laptop), kisha kuwajeruhi wanne na kutoweka.
Weruweru River Lodge Tukio hilo kubwa kuwahi kutokea siku za hivi karibuni mkoani Kilimanjaro, limetokea juzi alifajiri eneo la Mailisita kwenye hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge inayomilikiwa na mfanyabiashara Cuthbert Swai, ambaye pia anamiliki kampuni ya wakala wa utalii ya Ahsante Tours ya mjini hapa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watalii hao kutoka mataifa mbalimbali, walikumbwa na mkasa huo wakiwa wamelala ndani ya mahema majira ya saa 9 alfajiri, ambako walitishwa kwa bunduki na mapanga kabla ya kuporwa mali zao.
Katika tukio hilo, watalii watatu waliporwa zaidi ya dola 2,090 za Marekani, mmoja pauni 110 za Uingereza na euro kiasi kisichojulikana, sh milioni 5.4, kamera zaidi ya nne na moja ikiwa na thamani ya sh milioni 1.5 na nyingine ikiwa na thamani ya dola 3,000 za Marekani, zaidi ya sh milioni 4.5.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizothibitishwa na Kamanda wa Mkoa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Robert Boaz, majambazi hao kabla ya kufanya uhalifu huo, waliwakusanya watalii hao eneo moja na kuanza kuwapora kila kitu walichokuwa nacho.
Hata hivyo, Kamanda Boaz hakuweza kulizungumzia tukio hilo kwa kina, ikiwamo kutaja majina ya watalii hao, uraia wao na thamani halisi ya mali walizoporwa, kutokana na kuwa katika pilikapilika za kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kupokea ugeni wa Spika wa Bunge la Nigeria.
Kamanda Boaz, aliwaambia waandishi wa habari waliofika ofisini kwake jana kuwa tukio hilo atalitolea maelezo kamili leo kutokana na kutingwa na ugeni huo.
Ofisa mmoja wa polisi aliyeomba kutotajwa jina lake, alisema kuwa miongoni mwa watalii hao walioporwa mali zao, wako wanne waliokuwa wakijiandaa kuondoka na ndege alfajiri hiyo kupitia KIA.
Aliongeza kuwa watalii hao walijikuta katika mkasa huo, baada ya dereva wa gari lililokuwa limewabeba kuwashwa kuashiria kuondoka hotelini hapo, ndipo majambazi hao walipolivamia na kuanza kuwashambulia na hatimaye kuwapora mali zao ingawa watalii hao waliendelea na safari yao.
Mmoja wa wakurugenzi wa hoteli hiyo, Stella Shangali alipoulizwa juu ya tukio hilo, hakukiri wala kukanusha kuwapo, zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na kamanda wa mkoa kwa ufafanuzi zaidi.

Akutwa amekufa Chumbani kwake

MKAZI wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, Charles Swai (48), amekutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Englibert Kiondo, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:00 mchana, ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kitandani na haukuwa na jeraha lolote.
Kiondo alisema kifo hicho kiligundulika baada ya Swai kutofungua mlango wa chumba chake tangu alipofunga Julai 23 saa 2 usiku, ndipo majirani walipochungulia dirishani na kumuona akiwa amelala na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Chang’ombe.
Alisema askari walifika eneo hilo na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki dunia. Chanzo cha kifo hakijafahamika na mwili umehifadhiwa hospitali ya Temeke. Upelelezi unaendelea.
Katika tukio jingine, dereva aliyefahamika kwa jina la Felix Mgoba (25) mkazi wa Wazo, amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na Fuso.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi (ACP), Camillius Wambura, alisema lilitokea juzi saa 5:20 asubuhi huko barabara ya Bagamoyo eneo la Boko Msikitini.

Sitta na Mbowe wapigana vijembe

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta akisisitiza jambo juzi, baada ya mkutano wa Kamati ya Maridhiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Picha
 

Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiazimia kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), viongozi wa kundi hilo wamesema hawatishwi na uamuzi huo na kwamba wataendelea kususia vikao hivyo.
Kikao kilichokuwa kiwe cha mashauriano kilichoitishwa juzi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta kiliazimia kuzifanya marekebisho baadhi kanuni za uendeshaji kwa lengo la kusimamia nidhamu wajumbe wake, hatua inayotafsiriwa kwamba inawalenga Ukawa.
Jana Sitta akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi alisema mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa yatahusisha masuala ya nidhamu, yakiwamo fujo na utoro, mambo ambayo hivi sasa hayawezi kudhibitiwa moja kwa moja na mwenyekiti wa Bunge hilo.
Sitta alikuwa akitoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake jana na kusomwa mbele ya waandishi wa habari na Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, ikieleza maazimio ya kikao ya usuluhishi alichokuwa amekiitisha kwa ajili ya kutanzua mzozo unaotishia kukwama kwa mchakato wa Katiba Mpya.
Hata hivyo, Ukawa unaoundwa na wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka Vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la 201 walioteuliwa na Rais, walisusia kikao hicho na kusababisha uamuzi uliofikiwa kuwa wa upande mmoja.
Hata hivyo, wakizungumza  jana kwa nyakati tofauti, viongozi wa Ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na yule CUF, Profesa Ibrahim Lipumba walisema hawatishwi na mabadiliko ya kanuni yanayokusudiwa kufanywa na kwamba wataendelea kususia vikao hivyo hadi hoja zao zitakapozingatiwa.
Ukawa walitoka bungeni siku chache kabla ya kuahirishwa kwa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu mwezi Aprili mwaka huu, kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatumia wingi wa wajumbe wake kutaka kufutwa kwa baadhi ya mapendekezo ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Kauli ya Sitta
Sitta aliongeza kuwa moja ya kasoro katika uendeshaji wa Bunge ni pale makundi kama Ukawa na Tanzania Kwanza yanapotambuliwa kama makundi rasmi ya Bunge Maalumu, wakati makundi rasmi ni wabunge, wawakilishi na Kundi la Wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais.
“Bunge hili lina uhuru wa ajabu ambao ni mkubwa kuliko Bunge jingine lolote, Bunge ambalo hata uongozi wake hauwezi kumchukulia mtu hatua kwa utovu wa nidhamu eti mpaka umuone mtu anafanya makosa, umpeleke kwenye Kamati ya Kanuni na hivyo ndiyo inakuwa imekwisha maana kama ana watetezi wake wanamtetea,” alisema Sitta na kuongeza:
“Matokeo yake wananchi wanalalamika kwamba hakuna nidhamu bungeni na kwamba kiti kimeshindwa kuchukua hatua, sasa unachukuaje hatua wakati kanuni zetu ndivyo zilivyo?”
Aliendelea: “Yako mambo mengi yanapaswa kufanyika na tuna siku 63 tu za kukamilisha kazi tuliyopewa sasa hatuwezi kutumia fedha za umma na watu wengine wanafanya mzaha, leo huyu anachukua posho, mara anaondoka, haya mambo lazima yatafutiwe dawa.”

Kauli hiyo ya Sitta inaungwa mkono na taarifa iliyotolewa mapema jana ikisema Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge kutokuwa na vipengele vinavyozuia utoro, ukosefu wa nidhamu na matendo mengine yanayolenga kuvuruga mchakato wa Katiba, ni kasoro ambayo lazima itafutiwe ufumbuzi katika kikao kijacho.
Taarifa hiyo inasema kitendo cha Ukawa kuendelea kususia Bunge, kinapuuza wito wa jamii kupitia makundi mbalimbali pamoja na madhehebu ya dini na juhudi za usuluhishi za kutaka kuwezesha vikao vya Bunge hilo viendelee.
“Mambo hayo yote yanazua mashaka kuhusu lengo la wasusiaji kwamba pengine ajenda ya viongozi hawa ni nyingine na siyo upatikanaji wa Katiba. Kwa mtindo huu wa kususa ni vigumu kuweza kupata mwafaka” inasomea sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Sitta.
Mbowe na Lipumba
Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe alisema haamini kwamba kauli kama hizo zimetolewa na Sitta ambaye ni msomi na mwanasiasa mzoefu anayefahamu misingi ya hoja na maridhiano.
“Kanuni hazitungi Katiba, Katiba inatungwa na utashi wa wale tuliopewa dhamana ya kufanya kazi hiyo, sasa ni kwa bahati mbaya kwamba Sitta anafikiri vitisho vya kutunga kanuni za kutubana vitasaidia, haviwezi kusaidia chochote,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Ukawa hatutishwi na mabadiliko ya kanuni, waende wakabadilishe ili dunia nzima iwashuhudie wakipitisha Katiba ya upande mmoja, wasikwepe hoja wanapaswa kutafakari mantiki ya hoja zetu na siyo kutoa vitisho vya kutulazimisha kwenda bungeni, Katiba ni hiari na wala haitungwi kwa vitisho.”
Kwa upande wake Profesa Ibrahim Lipumba alisema Bunge Maalumu la Katiba haliwezi kubadili kanuni ili kumbana au kumfuta mjumbe wa Bunge hilo bila kwanza kubadilishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
“Kwanza, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kufanyiwa marekebisho na Bunge la Jamhuri ya Muungano na siyo Bunge Maalumu la Katiba. Pili, hata Rais aliyeteua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba hawezi kuwafukuza kwa sababu haijaelezwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sasa Bunge la Katiba litaweza vipi kuwafukuza,” alihoji.
Profesa Lipumba alisema wajumbe 201 waliteuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kufafanua kuwa hata wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi nao hawawezi kufukuzwa kwa kubadilishwa kwa kanuni za Bunge la Katiba.
“Mbunge wa Jamhuri ya Muungano au Baraza la Wawakilishi ili apoteze sifa za kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba ni lazima kwanza apoteze sifa za kuwa mbunge,” alisema.
Alisema kuwa msimamo wa Ukawa ni kutoshiriki kikao cha Bunge hilo hadi hapo wajumbe wote 629 wa Bunge hilo watakapokubaliana kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi yenye msingi wa muundo wa serikali tatu na siyo serikali mbili.
Taarifa ya Kamati
Mapema katika taarifa iliyosainiwa na Sitta kisha kutolewa kwa waandishi wa habari na Hamad, inaeleza kuwa vikao vya Bunge Maalumu hilo vitaendelea mpaka mwisho hata kama Ukawa wataendelea kususia vikao vyake.
“Kuanzia Agosti 5 Bunge liendelee kwa kuzingatia upya baadhi ya kanuni zake ambazo ni kikwazo katika kuhakikisha kuwa kazi ya kujadili na kupitisha Katiba inayopendekezwa inakamilika ndani ya siku 63 zilizosalia kisheria, yaani 60 za nyongeza na tatu pungufu ya zile siku 70 za awali,” inasomeka taarifa hiyo.
Hamad alisema kikao cha juzi kimeamua Bunge hilo kuendelea kutokana na kuwa na masuala mengi muhimu ya kikatiba ambayo yanawaunganisha Watanzania, yakiwamo usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi, kuikarabati Tume ya Uchaguzi (Nec), kurekebisha kikatiba masuala ya muungano na ukomo wa vipindi vya uongozi.
Taarifa hiyo ilieleza kukerwa na mikutano ya Ukawa inayofanyika katika mikoa mbalimbali nchini. “Hatua ya baadhi ya wajumbe wa Ukawa kwenda kwa wananchi na maoni yao imekuwa siyo mwafaka na siyo wakati wake. Bunge la Katiba liwajibike katika siku za usoni kujibu upotoshwaji wowote kuhusu mchakato wa Katiba kadiri ulivyojitokeza” alisema Hamad.

Meli ya zama na abiria 21 huko malaysia

Wahamiaji haramu kutoka Indonesia wanaendelea kufariki kutokana na ajali za majini kwenye mwambao wa Malacca.

Wahamiaji haramu kutoka Indonesia wanaendelea kufariki kutokana na ajali za majini kwenye mwambao wa Malacca.
Watu watatu wamefariki na wengine wanane hawajulikanai waliko baada ya meli waliyo kuwemo kuzama maji karibu na mwambao wa Malaysia, ambako meli tatu zilizama maji hivi karibuni.

Meli hiyo ilikua imesafirisha wahamiaji haramu kutoka indonesia, Shirika la habari linalomilikiwa na polisi ya majini ya Malaysia limearifu
“Miili ya watu watatu imeondolea ndani ya maji, watu 10 wameokolewa na wengine wanane hawajulikani waliko, baada ya meli hiyo kuzama, ajali ambayo ilitokea mapema alhamisi aubuhi wiki hii”, amesema Iskandar Ishak msimamizi wa shirika hilo la habari.
Meli hiyo iliyokua imesafirisha wahamiaji haramu 21, ambao walikua wakirejea nchini Indonesia kusheherekea Al Aïd el-Fitr, siku kuu ya kislamu ya kuhitimisha mfungo wa mwezi wa ramadhan, imezama maji katika bahari katika jimbo la Johor (kusini).
Iskandar Ishak, amesema kwamba uchunguzi wa kina umeanzishwa katika bahari hiyo, katikamwambao wa Malacca kulikotokea ajali hiyo ya meli.
Takribani watu 20 kutoka Indonesia wamefariki kutokana na ajali tatu mfululizo ziliyotokea katika bahari hiyo tangu mwishoni mwa mwezi Juni, na wengine zaidi ya ishirini wamepotea, kwa mujibu wa viongozi wa taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia.

Jeshi la kanda wajiandaa kupambana na Boko Haram

Mataifa manne ya Afrika Magharibi yameazimia kuunda kikosi cha pamoja ili kukabiliana na kitisho kinachoongezeka cha kundi la itakadi kali za Kiislamu la Boko Haram, linaloendesha shughuli zake hasa nchini Nigeria.
Kila moja ya mataifa hayo ya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon, litachangia wanajeshi 700 kwenye kikosi kinachonuwiwa kuboresha mapambano ya kanda hiyo dhidi ya wapiganaji hao.
Mataifa hayo manne yanayopakana na ziwa Chad, eneo ambalo ni ngome ya Boko Haram, tayari yanabadilisha taarifa za kijasusi na yanaratibu kwa pamoja usalama wa mpakani katika eneo, lakini kuunda kikosi cha pamoja chenye ukubwa huu itakuwa hatua kubwa zaidi katika ushirikiano wao.
Tangazo la kuundwa kikosi hicho lilitolewa wakati wa mkutano wa mamawziri wa ulinzi kutoka mataifa hayo manne, lakini hakukuwa na taarifa zaidi juu ya muda au eneo vitakakopelekwa vikosi hivyo. Wapiganaji wa Boko Haram wameua maelfu ya watu tangu mwaka 2009, walipoanzisha juhudi zao za kuunda taifa la Kiislamu nchini Nigeria.

Raia zaidi wateketezwa
Matukio ya uripuaji mabomu na mashambulizi mengine yamekuwa jambo la kawaida kaskazini mwa Nigeria, lakini Boko Haram ilianza kupamba vichwa vya habari kimataifa miezi iliyopita, baada ya kuwateka wanafunzi zaidi ya 200 kutoka shule mjini Chibok. Utekaji huu ulipelekea kutolewa miito ya kuchukuliwa hatua, na ahadi kutoka kwa marais wa kanda hiyo kuanzisha vita kamili dhidi ya wapiganaji hao.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau.
Niger na Cameron zimeimarisha hasa usalama katika maeneo ya mipakani, lakini hakukuwa na ishara zozote za mashambulizi makubwa yanayovihusisha vikosi vya kanda. Shirika la kutetea haki za binaadamu la Huma Rights Watch lilikadiria wiki iliyopita kuwa wapiganaji hao wameuwa zaidi ya raia 2000 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.
Jana Jumatano, miripuko miwili katika mji wa kaduna, ambayo iliwalenga mhadhiri maarufu wa dini ya Kiislamu na rais wa zamani wa Nigeria, ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 42 katika vurugu za hivi karibuni zinazolaumiwa kwa kundi la Boko Haram.
.
Gavana Kaduna ahofia jimbo lake
Maandamano ya kutaka kurejeshwa kwa wasicha wa shule.
Maandamano ya kutaka kurejeshwa kwa wasicha wa shule
Polisi ilisema shambulio la kwanza lilifanywa na mripuaji wa kujitoa muhanga akiulenga msafara wa Sheikh Dahiru Bauchi, kiongozi wa dini ambaye ameukosoa vibaya uasi wa miaka mitano wa Boko Haram.
Shambulio lingine lililotokea saa mbili baadaye na kuuwa watu 17 lilimlenga Muammadu Buhari, moja wa wapinzani maarufu nchini Nigeria, ambaye pia aliiongoza Nigeria kama dikteta wa kijeshi kuanzia mwaka 1983 hadi 1985.
Gavana wa jimbo la Kaduna Mukhtar Ramalan Yero alitangaza amri ya saa 24 ya kutotembea usiku, na msemaji wake alieleza wasiwasi wa gavana huyo, juu ya kuripuka kwa machafuko katika mji huo maarufu kwa mapigano ya kidini katika miaka ya karibuni, kwa sababu walengwa wote wa mashambulizi hayo, Bauchi na Buhari, wanashikilia nyadhifa muhimu machoni mwa watu.

Hamas na Israeli wakubaliana kusitisha Mapigano

Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel

Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu kuanzia leo asubuhi.
Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema atendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.

Friday 25 July 2014

Wananchi wa pakistan wasambulia wachezaji wa klabu toka Israel

Mashabiki washambulia kilabu cha Israel
Mashabiki waliobeba bendera za Palestina walivuruga mechi ya kirafiki baina ya Lille na kilabu cha Israel Maccabi Haifa.
Upinzani wa mashambulizi ya Israel nchini Gaza ulipata mwelekeo mpya baada ya mashabiki kuwashumbulia wachezaji wa timu ya Maccabi Haifa katika mchuano wao wa kirafiki dhidi ya Lille nchini Ufaransa.
Vurugu hiyo ilianza katika dakika ya 84 pale mashabiki waliokuwa wamebeba bendera ya Palestina walipojitosa uwanjani na kuanza kuwashambulia wachezaji wa kilabu hiyo ya Israel.  
maccabi
Mechi hiyo iliendelea baada ya maafisa wa usalama kukwamisha vurugu na kuwatoa nje mashabiki hao. Lille ilitwaa ushindi wa mechi hiyo kwa mabao 2 kwa bila.
macca3

Stock City yamnasa kinda toka Barcelona

Stoke City yamsajili nyota wa BarcelonaKlabu ya soka nchini Uingereza, Stoke City yafanikiwa kumsajili nyota wa Barcelona Borjan Krkic kwa mkataba wa miaka minne.
Stoke City imefanya uhamisho wa mchezaji huyo aliyemaliza mkataba wake na timu ya soka ya Ajax. Stoke imesaini mkataba wa miaka minne na nyota huyo wa magoli mwenye miaka 23 .
Kiongozio wa klabu hiyo, Tony Scholes alieleza “Tumefurahi kumsajili nyota wa miaka 23, ambaye anakipaji na ni mchezaji atakaeng’aa katika siku za usoni.
Borjan aliyekuzwa na kuendelezwa katika kilabu cha Barcelona, alichezea timu A ya kilabu hicho tangu akiwa na umri wa maika 17 na kufunga magoli 26 katika mechi 120.
Ukiachana na Barcelona, Borjan pia amewahi kutinga uzi wa Milan, Roma na Ajax.

Chelsea yazindua jezi nambari 3

Chelsea yazindua jezi ya 3Shirika la adidas na timu ya Chelsea wamezindua jezi ya 3 itakayovaliwa na timu hiyo msimu huu.
Timu ya Chelsea imezindua jezi ya 3 itakayotumiwa iwapo jezi ya kwanza na ya pili zitakaribiana kirangi na jezi ya timu watakayokuwa wakichuana nayo.
Uuzaji wa jezi hiyo utaanza rasmi tarehe 6 mwezi Agosti.

Suarez Huenda akacheza Mechi dhidi ya Real Madrid

Mshambulizi mpya wa Barca Suarez
Mshambulizi wa Uruguay na Barcelona huenda Luiz Suarez huenda akashiriki katika mechi dhidi ya Real Madrid mwezi Oktoba.
Suarez ambaye alitia sahihi kandarasi ya kujiunga na Barcelona punde baada ya kuondolewa katika kombe la dunia kwa tuhuma za kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini alipigwa marufuku na FIFA kwa muda wa miezi minne.
Kandarasi hiyo iliigharimu Barca zaidi ya pauni milioni £75.
Suarez alipigwa marufuku tarehe 26 Juni siku mbili baada ya tukio kumaanisha kuwa atakuwa huru kurejea tarehe 26 Oktoba katika mkondo wa kwanza wa mechi ya El Clasico katika uwanja wa Bernabeu.
Mkondo wa pili utakuwa tarehe 22 machi mwakani.
Hata hivyo Mshambulizi huyo zamani akiichezea Liverpool hataweza kufanya mazoezi na timu hiyo kwani angali anatumikia marufuku ambayo inamzuia kushiriki mechi yeyote ile wala kuingia katika uwanja wowote ule wa kandanda.
Suarez alipomng'ata Chiellini katika kombe la dunia Brazil
Kulingana na Ratiba ya mechi za La Liga , mabingwa watetezi wa ligi hiyo Atletico Madrid watafungua kampeini ya kutetea taji lao dhidi ya Rayo Vallecano Agosti tarehe 24 ,Huku Barca ikifungua kampeini ya mwaka huu kwa kuialika Elche nyumbani kwao .
Mabingwa wa Ulaya Real Madrid nao watakuwa wenyeji wa Cordoba katika mechi yao ya ufunguzi.
Je Real itampa mfungaji mabao mengi katika kombe la dunia mwaka huu James Rodriguez nafasi katika el Clasico ?
Ama mabingwa hao watamchezesha mjerumani Toni Kroos?
Wasimamizi wa ligi hiyo ya Uhispania wanatarajiwa kuamua wiki hii iwapo watatumia povu nyeupe kama iliyotumika katika kombe la dunia kuhakikisha mahala mpira unapaswa kuwekwa ama wapi laini ya walinzi inapaswa kupigwa wakati wa free-kick .

Hatimaye Didier Drogba arejea chelsea

Mourinho na  Drogba
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.
Mourinho alidhibitisha kuwa The Blues inatafakari kurejea kwake Uingereza na kuwa anatumai uhamisho huo utatekelezwa bila hisia kali .
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
Drogba akiwa Galatasaray.
Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich .
Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.

Mabaki ya ndege ya Algeria yapatikana


Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.
Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
„Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"
Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo.
"Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"
Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo.
"Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"
Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko
"Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana."
Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema

Thursday 24 July 2014

Israel yaendelea kushambulia Gaza ; washambulia tena Shule

Israili imeshambulia makao ya wakimbizi kati shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza .
Takriban watu 15 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa vibaya baada ya majeshi ya Israeli kulipua shule inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa kuwahifadhi wakimbizi wa ndani kwa ndani wanaotoroka mashambulizi ya Isareli katika ukanda wa Gaza .
Wizara ya Afya katika ukanda wa Gaza imedhibitisha shambulizi hilo katika shule hiyo iliyoko Beit Hanoun ambayo inatumiwa kama makazi ya wakambizi wapalestina wanaotoroka makombora ya Israili.
Shambulizi hilo ni la nne kutokea katika vituo vinavyomilikiwa na Umoja wa Mataifa tangu Israeli ivamie ukanda huo yapata majuma mawili yaliyopita.
Kufikia sasa Wapalestina 725 wameuawa .
Israili imeshambulia makao ya wakimbizi kati shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza .
Waisraeli 30 wameuawa wengi wao wakiwa ni wanajeshi katika siku 16 za makabiliano kati ya Israeli na Hamas.
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Awali mwsimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia maswala ya Misaada bi Valerie Amos alisema kuwa hali ya maisha imeendelea kuzorota katika ukanda huo na kuwa kuna haja ya dharura ya kusitishwa kwa vita ilikufanikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu .
Bi Amos alisema kuwa watu laki moja (118,000) wanaishi katika kambi za umoja wa mataifa zilizoanzishwa katika shule zinazoendeshwa na UN.
Israili imeshambulia makao ya wakimbizi kati shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza .
Mkuu huyo wa UN alisema kuwa maji yamepungua na chakula pia hakitoshi kuwalisha wakimbizi hao wote .
Bi Amos amesema kuwa asilimia 44% ya Gaza hapakaliki kwa Wapalestina.
Hayo yamejiri baada ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa anasikitikia vifo vya Wapalestina lakini wajibu unamtegemea kiongozi wa Hamas ambaye bado anashikilia kuwa Israeli hainabudi kukoma kuikalia Gaza kimabavu.

Ndege ya Algeria yapotea na watu 116

Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake ilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
Afisa huyo anasema kuwa ndege hiyoya Air Algerie ilikuwa imepaa dakika 50 katika anga ya Sahara mara ya mwisho mawasiliano yao.
Ndege hiyo iliokuwa inaeelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi na wahudumu sita .
Oparesheni ya dharura ya kuitafuta ndege hiyo ieanzishwa,
Ndege hiyo nambari AH 5017 inamilikiwa na shirika la ndege la kihispania la Swiftair.
Mwandishi wa Ukomboz aliyeko katika mji mkuu wa Mali Bamako anasema kuwa kuna habari kuwa ndege hiyo huenda ilianguka katika eneo la janga la sahara kati ya
mji wa Gao and Tessalit .
Mwandishi huyo wa ananukuu ripoti kutoka kwa wanajeshi wa kulinda amani walioko huko Mali na duru za shirika la habari la AFP.
Brigadia mkuu wa majeshi ya kulinda amani nchini Mali Koko Essien, amesema kuwa maeneo hayo ya jangwani yana idadi ndogo sana ya wakaazi kwa hivyo ni vigumu kupata habari kutoka huko na inawabidi kutafuta ilikoanguka ndege hiyo.
Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Aidha Brig Essien anasema kuwa eneo hilo linamilikiwa na wapiganaji waasi .
Wamiliki wa ndege hiyo Swiftair wamesema kuwa ndege hiyo aina ya MD83 ilikuwa imeomba kubadili uelekeo wake kutokana na hali mbaya ya anga na ukungu mkubwa karibu na mpaka wa Algiers.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.
Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo.
Tukio hili la hivi punde Linaloongeza wasiwasi kuwa njia inayotumiwa na misafara ya ndege ziendazo sehemu hiyo inapitia eneo lenye utata la anga ya Mali.

Jose akiri chelsea ni moto wa kuotea Mbali msimu huu

Mourinho ametumia pauni 80 milioni kwa usajili wa wachezaji watatu msimu huu.

Velden, Austria. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa timu yake itakuwa moto wa kuotea mbali kwa miaka 10 ijayo katika Ligi Kuu England, baada ya kuwasajili Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis.

Mourinho ametumia Pauni 80 milioni kusajili wachezaji hao kutoka Ligi Kuu ya Hispania (La Liga). Fabregas hakuwa na nafasi Barcelona wakati Filipe Luis na Diego Costa waliiongoza Atletico Madrid kutwaa taji la ligi hiyo msimu uliopita.

“Timu ambayo imekuwa ikishinda kwa misimu 10 inabadilika hatua kwa hatua. Tumenunua wachezaji wapya na tunajaribu kuisuka kwa miaka 10 ijayo,” alisema Mourinho katika hoteli waliyofikia Chelsea mjini Velden, Austria jana.

“Msimu uliopita tuliishia nusu fainali, na ulikuwa msimu wa ajabu,” aliongeza. “Tulikuwa na timu ya vijana wengi wakati ule. Lakini hata sasa, tutacheza kwa ajili ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.

“Msimu ambao tunadhani tutakuwa na kikosi kizuri, ndio vijana watakapokuwa wakipata uzoefu zaidi. Wako katika hali nzuri ya kuweza kutwaa mataji.”

Licha ya kuwepo kwa ushindani wa timu kubwa za England, kocha huyo wa Blues mwenye miaka 51, alisema asingeweza kuwepo Stamford Bridge kama hawezi kufikiria kuwa Chelsea inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.

“Kama sitafikiria hilo, nitalazimika kwenda nyumbani na kumuacha mtu mwingine kuendelea na majukumu yangu kama kocha.

“Watu wanaweza kuzungumza kuhusu ligi, lakini England ndio nchi pekee ambayo timu zake tano au sita zinazoweza kutwaa ubingwa. Soka ni ushindani wa kila mwishoni mwa wiki, na hilo pekee linatokea England.

“Unapokuwa na timu mbili za Manchester, tatu kutoka London – Tottenham, Arsenal na sisi, ikiiongezeka Liverpool, hizo ni timu kubwa sita, ambazo zote zinaweza kupambana kuwania ubingwa. Na hii ndio sababu kila mmoja anaipenda Ligi Kuu ya England.”

Sumaye awaasa wafuasi wa dini Mbalimbali kuacha kupigana Vita

Mzee Sumaye
 Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema vita ya kidini na ile inayosababishwa na imani ya watu ni mbaya na mara zote huwa haina mshindi.
Sumaye aliyasema hayo mjini Arusha jana alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Dayosisi ya Arusha, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Sekondari ya Peace House.
“Tanzania hatuna tatizo kubwa katika hili, lakini hatuko salama sana. Kuna chokochoko za hapa na pale zinazoendelea zenye sura ya kiimani. Hii ni ishara ya kuwa upendo, amani na mshikamano miongoni mwetu umepungua na kuathiri umoja wetu.
“Tukiwa wamoja, sekeseke hili halitakuwa na nafasi kwetu kwa sababu hakuna dini inayofundisha chuki wala kupigana, lazima tuwe makini licha ya kila mtu kuwa na uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria,” alisema Sumaye.
Alitoa wito kwa viongozi wa dini kuwasimamia vyema waumini wao ili nchi isije ikakumbwa na balaa la vurugu za kidini, jambo ambalo alisema ni la hatari kwa usalama wa nchi na watu wake.
Alisema wakati dunia inapita katika mapito mbalimbali ya hatari, Watanzania hawana budi kung’ang’ania amani na upendo walionao kwa masilahi ya ustawi wa jamii yao.
Alisema kuna nchi nyingi duniani ambazo zimeingia katika migogoro iliyosababishwa na chuki za kidini na zimeishia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aliwataka Watanzania katu wasikubali kuruhusu hali hiyo itokee, bali waendeleze misingi ya amani, upande na utulivu vilivyoachwa na waasisi wa taifa, akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Utafiti wa kinga , Tiba ya UKIMWI waendelea kuleta matumaini

Watafiti wakitoa sampuli za damu kutoka kwa sokwe mtu katika utafiti wa Ukimwi huko Gabon
  Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.
“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).”
ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.
Mmoja wa wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kituo cha Mbeya (NIMR-MMRC), Clifford Majani ameuelezea utafiti huo kama mwanga mpya katika teknolojia ya kukabili VVU.
“Kama imepatikana teknolojia ya kukiondoa kirusi ndani ya seli ni hatua nzuri ya kukabili VVU. Hili lilionekana kuwa gumu mwanzoni,” alisema Majani.
Alisema imekuwa vigumu kuua kirusi kikiwa ndani ya seli na hata baadhi ya wanasayansi wamejaribu kutengeneza dawa itakayotambua seli zilizoathirika ili ziuawe lakini hilo likawa gumu.
“Inaweza ikapatikana dawa ya namna hiyo (inayoua seli zilizoathirika) lakini ikawa inaathiri vitu vingine ndani ya mwili. Hilo halikubaliki. Kikubwa katika ugunduzi huo ni dawa kuweza kukifuata kirusi kinakojificha na kukiondoa, jambo ambalo dawa nyingi zimeshindwa zikiwamo ARV,” alisema.
Hata hivyo, Majani alisema changamoto ambayo inaweza kujitokeza katika majaribio ya dawa hiyo ni usalama wakati wa matumizi.
“Lazima dawa hiyo ichunguzwe isije ikawa inaathiri viungo vingine pamoja na utendaji wa mwili kwa ujumla. Maana hapo ndipo dawa nyingi zinaposhindwa… Tusubiri tuone hii inaweza kuwa na matumaini zaidi,” alisema Majani.
Mkutano wa Ukimwi
Ugunduzi huo umekuja wakati wanasayansi, waunda sera na wadau wa mapambano ya VVU wakiwa wanatoa kauli za kukata tamaa kwenye mkutano wa Ukimwi unaomalizika kesho huko Melbourne, Australia.
Wanasayansi kadhaa wanaotoka kwenye taasisi kubwa za utafiti za VVU wameweka wazi kuwa tafiti nyingi zilizokuwa na matumaini zimeshindwa kufanya kazi kwa asilimia 100 baada ya dawa zake kufanyiwa majaribio kwa sababu dawa zake zinapotumika, vipimo huonyesha wamepona lakini baada ya muda VVU hurejea upya.
“Kinachoonekana ni kwamba virusi hivi hujificha sehemu fulani ya mwili ili visiathirike na kusubiri mtu aache dawa ili virejee upya kushambulia CD4,” alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya wa Magonjwa ya Kuambukiza na Kinga ya Peter Doherty ya Australia, Profesa Sharon Lewin.
Dawa mpya inavyofanya kazi
Dk Khalili alisema wametengeneza dawa yao kwa protini maalumu ambayo inakata sehemu ya seli iliyoshambuliwa na kirusi cha Ukimwi na kukivuta nje.
Baada ya kukivuta, dawa huachana na seli hiyo na kuiacha ikijitibu yenyewe na kupona kabisa kiasi cha kuendelea na kazi zake za kinga mwilini mwa binadamu bila tatizo.
VVU kwa kawaida hushambulia seli kinga aina ya CD4 na kuzifanya kama kiwanda cha kuzalishia virusi vingine.
Kwa kawaida seli ikishaingiliwa na kirusi, huacha kazi yake ya kinga ya mwili na badala yake kuchukua jukumu la kutengeneza VVU.
“Dawa yetu inafanya kazi kwa haraka, kwa makini na bila kuathiri seli,” alijigamba Dk Khalili.
Alisema tayari imefanyiwa majaribio maabara na kuonekana inafanya kazi vizuri na sasa wamehamishia majaribio kwa wanyama.

Katika maabara, alisema dawa hiyo ilifanyiwa majaribio kwa damu ya binadamu na ikaonyesha kufanya kazi kwa asilimia 100.
Dk Khalili anaamini kwamba majaribio hayo yatawachukua miaka michache... “Lakini tunaamini ni mfumo ambao utaweza kufanya kazi vizuri kwa binadamu.”
Alisema wanachofanya sasa ni kuangalia mfumo ambao utakuwa mzuri zaidi kwa ajili ya tiba ya binadamu.
Kwa namna teknolojia ya dawa hiyo ilivyo, alisema wanaweza kuitumia kwa ajili ya kuwatibu wale ambao tayari wameambukizwa na hata kuwakinga wale ambao siyo waathirika.
Uzuri wa dawa hiyo, pia alisema inaweza kutumiwa na mtu ambaye anatumia ARV pasipo kuingiliana kiutendaji.
Ugunduzi wao ulichapishwa kwenye Jarida la Taifa la Elimu ya Sayansi la National Academy of Science la Marekani na kuonekana kuvuta hisia za wengi.
Hali ya Ukimwi duniani
Akizungumza kwenye mkutano wa Melbourne, Profesa Lewin alisema tafiti za sasa zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 14 duniani wanaishi na VVU.
Alisema mamilioni ya watu hao wamekuwa wakisaidiwa kwa kutumia ARV, wakati huu ambao bado hakuna kinga wala tiba, inayoaminika.
Alisema ingawa tafiti nyingi hazijaonyesha matumaini waliotarajia ya kupata kinga na chanjo, bado juhudi zinaendelea ili kuhakikisha wanafikia mahali HIV inakuwa haina nafasi katika mwili wa mwanadamu.
Alisema pamoja na matokeo hasi ambayo yamejitokeza kwenye tafiti nyingi, bado anaamini kwamba ipo siku chanjo na tiba vitapatikana.
Wanasayansi waliohudhuria mkutano huo waliitaka dunia isiogope kutokana na kushindwa kwa baadhi ya tafiti kama ilivyokuwa kwa mtoto wa Jimbo la Mississippi, nchini Marekani ambaye alitangazwa amepona na baadaye virusi vikaibuka upya.

Ndege nyingine yaua 40


Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne.
ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio.
Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua.
Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku viwili vya kutunzia kumbukumbu ya ndege ya malaysia iliyoangua nchini Ukraine tarehe 17 mwezi huu vikiwa vimefika mikononi mwa wataalamu wa masuala ya anga ili kuchunguza ni ni kitu gani kiliisibu ndege hiyo.

Ndege ya algeria yapoteza Mawasiliano

Shirika la ndege la Taifa la Algeria, limesema limepoteza mawasiliano na moja kati ya ndege zake iliyokua ikitoka Burkinafaso kwenda Algiers kupita sahara.
Mawasiliano yalipotea dakika 50 baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji wa Ouagadougou, shirika hilo limeeleza.
Ndege namba AH 5017 ilikua na abiria 110 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo.
Chanzo cha habari kimeliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa Ndege hiyo haikua mbali na mpaka wa Algeria wafanyakazi wa ndege hiyo walipoambiwa wabadili uelekeo kwa kuwa mawasiliano yalikua hafifu na kuepuka hatari ya kugongana na ndege nyingine katika njia ya Algiers-Bamako.
Mawasiliano yalipotea baada ya kubadilishwa kwa njia.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.

Wednesday 23 July 2014

Mabeki wa Chelsea walipomkaba mchezaji mnene zaidi duniani

JUMAMOSI jioni, John Terry aliwaongoza mabeki wa Chelsea kukabiliana na mchezaji mnene na mwenye nguvu zaidi duniani, Saheed Adebayo Akinfenwa ambaye umbo lake linaleta kichekesho kikubwa kwa mashabiki wa soka.
Chelsea ilishinda mabao 3-2 wakati huu ikijiandaa na michuano mbalimbali msimu ujao, lakini walilazimika kukabiliana na Akinfenwa ambaye alikuwa katika ubora wake.
Hadi wakati anatolewa uwanjani dakika ya 60, Chelsea ilikuwa imekufa 2-0 huku Akinfenwa akimuhenyesha Terry na wenzake. Hata hivyo baadaye walifunga mabao matatu ya haraka haraka yaliyobadili matokeo ya mechi wakati Akinfenwa akiwa nje ya uwanja.
Licha ya umbo lake kubwa, Akinfenwa aliyezaliwa jijini London Mei 10, 1982 anadaiwa kuwa na kilo 86 tu lakini ana uwezo wa kubeba uzito wa kilo 180 ambazo ni mara mbili na uzito wake.
Tayari Fifa wamempitisha kama mchezaji mwenye nguvu zaidi duniani huku wakimuingiza katika Video zao za michezo ya kompyuta huku umbo lake likionekana kuwa kivutio kwa mashabiki wengi duniani.
Mlinzi wa klabu ya Vale iliyo daraja la kwanza England ambaye alicheza timu moja na Akinfenwa Northampton, Dan Jones anaeleza kwamba ni kujisumbua tu kujaribu kutumia nguvu kumkaba mchezaji huyo.
“Soka lake halibadiliki tangu tulipokuwa Northampton. Anapenda kuuficha mpira miguuni na inajionyesha wazi kwamba hana mpango wa kukimbia nao. Anapenda kukaa na mpira mguuni huku akiwasukuma walinzi kwa nguvu zake.” Anasema Jones.
“Hauwezi kushindana naye kwa nguvu kwa sababu utaishia kumfanyia rafu au atakutupa tu. Inabidi utumie akili sana wakati wa kumkaba. Inabidi usitumie nguvu nyingi sana kumkaba.”
“Wakati mwingine akipata mpira tunamuachia tu na kuangalia anachotaka kufanya kwa sababu tunajua hawezi kukimbia, yeye huwa anaaangalia watu wanaofungua nafasi tu.” Anasema Jones.
Akinfenwa amedai kwamba hajawahi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sababu makocha wamekuwa wakiliogopa umbo lake na kudhani kwamba atakuwa mzigo tu uwanjani kitu ambacho sio cha kweli.
“Nadhani naweza kutisha Ligi Kuu. Nadhani niko sawa na Didier Drogba tu. Sijacheza madaraja ya juu kwa sababu kuna mtazamo fulani wa jinsi ambavyo mwanasoka anapaswa kuwa na mimi sionekani kuwa hivyo,” anasema Akinfenwa.
“Sitaki kuonekana mjinga lakini nimefunga zaidi ya mabao 150 katika mechi 300. Waulize walinzi au makocha wa timu pinzani watakwambia jinsi nilivyo balaa.” Anasema staa huyo
“Ningependa kukutana na John Terry na kumuharibu. Ningependa kukutana na wachezaji kama Nemanja Vidic hili niwaonyeshe inakuaje unapokumbana na mtu kama mimi.” Alijigamba staa huyo mzaliwa wa Islington London.
Akinfenwa amekiri kwamba anapenda sana kula lakini hapendi kula vyakula vya kisasa na anapenda kula zaidi vyakula vya Kiafrika.
“Nakula sana, lakini sio McDonald au migahawa ya vyakula vya haraka haraka. Lakini nadhani inabidi nipewe hisa na migahawa ya Nandos kwa sababu nakula sana pale.”
Akinfenwa anavaa jezi kubwa (XXL) mara zote amekuwa akiandamwa na mashabiki wa timu pinzani ambao huwa wanaimba kuwa mchezaji huyo ana uwezo mkubwa wa kula nyama nyingi kuliko kufunga mabao mengi.
“NImekubali kwamba inabidi nikutane na mashambulizi haya. Nakubali kwamba nina umbo kubwa na ningesikitika kama nisingekuwa hivi. Mara nyingi nakumbana na haya na ninapokumbana nayo huwa nafunga.”
“Kitu kinachonifurahisha ni pale wanaposema kuwa mimi ni mnene kama Eddie Murphy. Napenda mashabiki wa timu pinzani wanaponishambulia kwa sababu mimi uwanjani naendelea kufunga tu.”
“Kama ningekuwa nasijikia kuwa mnene au mvivu, basi ningefanya kitu kupunguza unene wangu. Sijawahi kufanya mazoezi ya kupunguza uzito na makocha wengi walionifundisha wanakubaliana na ukweli kwamba umbo langu ndivyo lilivyo.”
Akinfenwa ni mmoja kati ya wachezaji waliocheza timu nyingi England. Mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 32 licha ya kutocheza katika Ligi Kuu ya England lakini amecheza klabu 14 za madaraja ya chini.
Timu hizo ni FK Atlantas, Barry Town, Boston United, Leyton Orient, Rushden & Diamonds, Doncaster Rovers, Torquay United, Swansea City, Millwall, Northampton Town, Gillingham,Northampton Town, Gillingham na AFC Wimbledon.

Israel yaua watoto wenyine kwa Bomu

UN: Israel inaua watoto na kubomoa hospitali GhazaMashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema utawala haramu wa Israel umeua idadi kubwa ya watoto na kubomoa mahospitali katika mashambulizi yake ya kinyama yanayoendelea katika Ukanda wa Ghaza. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF imetoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa, baada ya kupita wiki mbili za mashambulizi ya Israel huko Ghaza, asilimia 33 ya waliouawa shahidi katika mashambulizi hayo ni watoto. Msemaji wa UNICEF Christopher Tidey amesema, kwa ujumla hadi sasa Israel imeshaua watoto 121 wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza na kwamba watoto waliojeruhiwa ni zaidi ya 904. Jumla ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya Israel huko Ghaza ni zaidi ya 610 huku wengine wasiopungua 3,600 wakijeruhiwa. Aghlabu ya wahanga wa mashambulizi hayo ya Israel ni raia wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto. Wakati huo huo, vituo vya afya vipatavyo 18 vimeharibiwa Ghaza, huku wahudumu 20 wa afya wakijeruhiwa wakati mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina yakiendelea. Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa limesikitishwa mno na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya vituo vya afya katika hujuma za utawala haramu wa Israel dhidi ya Ghaza. WHO imesema wahudumu wa afya ni lazima walindwe wakati wote, na kuruhusiwa kufanya kazi zao. Fadella Chaib kutoka WHO amesema kuwa, idadi kubwa ya majeruhi imezidi uwezo wa vituo vya afya ambavyo awali vilikuwa vikitoa huduma kwa hali ya kawaida. Katika hujuma yake Ghaza, Utawala wa Kizayuni wa Israel mbali na kuwaua watoto na kubomoa mahospitali pia unatumia silaha za maangamizi ya umati zilizopigwa marufuku duniani. Vitendo hivyo vyote vya Israel ni kinyume cha sheria za kimatiafa na ni jinai za vita lakini madola ya Magharibi yanayoongozwa na Marekani si tu kuwa hayalaani jinai hizo bali yanaunga mkono Israel na kuipa kinga isichukuliwe hatua za kisheria.

Machafuko bado yaendelea Libya

Kuendelea machafuko nchini LibyaMachafuko nchini Libya si tu kwamba yamekuwa ni kitu cha kila siku, bali kadiri muda unavyopita, ndivyo machafuko hayo yanavyoongezeka. Habari zinasema kuwa, mapigano yanaendelea kwa siku kadhaa sasa karibu na Uwanja wa Ndege wa Tripoli na hii ni katika hali ambayo mji wa Benghazi nao unaendelea kushuhudia mauaji dhidi ya wanasiasa, maafisa wa kijeshi na raia wa kigeni. Tukio la karibuni kabisa huko Benghazi ni kuchinjwa na kukatwa kichwa kibarua mmoja raia wa Ufilipino. Habari nyingine zinasema kuwa, wawakilishi wawili kutoka miji ya Benghazi na Janzur katika Congress ya Taifa ya Libya (Bunge) wametekwa nyara na watu wenye silaha. Mauaji dhidi ya maafisa wa kijeshi wa Libya nayo yanaendelea mashariki mwa nchi hiyo. Hivi sasa hali ya Libya ni mbaya sana; na jambo hilo linaonekana katika miundo yote ya kisiasa, kiuchumi ya kijamii ya nchi hiyo. Katika upande wa kisiasa na licha ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi na kujulikana muundo wa Bunge la nchi hiyo, lakini hadi hivi sasa zoezi la kukabidhi madaraka kutoka Congress ya Taifa kwenda kwa bunge jipya halijafanyika. Sababu yake ni kuwa hali ya Libya haiiruhusu nchi hiyo kutangaza siku ya kufanyika kikao cha kwanza cha bunge hilo jipya. Katika upande wa masuala ya kijamii pia ni kwamba, hakuna umoja na mshikamano wowote wa kitaifa nchini Libya. Kila sehemu nchini humo imo mikononi mwa kabila au pote fulani la watu na kwamba ni viongozi wa kikabila ndio wanaoongoza baadhi ya maeneo ya Libya. Mfano wa wazi ni maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamejitangazia utawala wa ndani na kadiri siku zinavyopita ndivyo maeneo hayo yanavyozidi kutoka mikononi mwa serikali kuu kiasi kwamba maeneo hayo hata yameanza kuchimba mafuta bila ya idhini ya serikali ya Tripoli. Katika upande wa kiuchumi pia, maeneo mengi ya mafuta yako mikononi mwa viongozi wa kikabila. Jambo hilo limeathiri vibaya sekta ya usafirishaji nje mafuta nchini Libya na kupunguza mno pate la serikali kuu. Hali hiyo kusema kweli inaufanya mustakbali wa Libya kukumbwa na giza nene. Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, si jambo lililo mbali kuiona Libya ikigawika vipande vipande. Hali ilivyo Libya inaonesha wazi kuwa, machafuko ya nchi hiyo yanachochewa na mikono ya nje. Wanaochochea machafuko hayo ni yale madola ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanaukodolea macho ya tamaa utajiri mkubwa wa mafuta na gesi wa nchi hiyo. Tunathubutu kusema kuwa, hali ya hivi sasa ya Libya ni jinamizi kwa wananchi wa nchi hiyo, lakini wakati huo huo ni ndoto nzuri ya usingizi mnono kwa dola la Marekani na madola mengine ya Magharibi.