Mbu wa Malaria |
Watafiti wametoa tahadhari kuwa
vijidudu vya malaria visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika
maeneo ya mpakani kusini mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi
ya Malaria.
Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya
Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo
havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya
malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudiamatibabu baada ya kukumbana na maambukizi inaweza kusaidia kupambana na kusambaa kwa Malaria katika Asia na baadae Afrika ndani ya muda mfupi. Mamia ya maelfu ya watu hufariki kutokana na Malaria kila mwaka hasa katika Afrika.
No comments:
Post a Comment