wasichana waliotekwa na Boko Haram
Maafisa wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa
zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa kutoka
kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake
hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita
karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali
ya Nigeria imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna
walivyotoweka wasichana hao.
wapiganaji wa Boko Haram
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai
kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara
walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria
amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi
ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Bado wasichana wengine hawajapatikana
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram
wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi
Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi
ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea
kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.
No comments:
Post a Comment