Mashambulizi ya angani
yanayofanywa na Israel katika eneo la Gaza yameendelea huku oparesheni
ya Isreal dhidi ya wapiganaji wa kipalestina ikiingia siku yake ya 7.
Mashambulizi hayo yakiendelea, wapiganaji wa kipalestina nao wamekuwa wakirusha makombora ndani ya Israel.Maafisa wa Palestina wanasema kuwa takriban watu 172 wameuawa tangu mashambulizi hayo yaanze jumanne iliopita.
Israel inasema kuwa takriban makombora 1000 ya roketi yamerushwa kutoka Gaza katika mda huo.
Imesema kuwa iliidungua ndege moja ya Palestina isiyo na rubani karibu na eneo la Ashdod hii leo asubuhi.
Awali maelfu ya raia walitoroka kutoka Kaskazini mwa Gaza kufuatia onyo la israel.
Israel imeweka maelfu ya wanajeshi wake katika mpaka na Gaza huku ikitishia kutekeleza uvamizi wa ardhini.
Makomando wa Israel walitekeleza mashambulizi yao ya kwanza ardhini siku ya jumapili,ambapo walikishambulia kituo kimoja cha kurusha makombora ya roketi.
Mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka mataifa ya kiarabu wanatarajiwa kukutana mjini Cairo hii leo ili kujuadiliana kuhusu mgogoro huo huku idadi ya waathiriwa ikiongezeka.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba asilimia 77 ya watu waliouawa katika eneo la Gaza ni raia.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Israel Luteni kanali Peter Lerner amekosoa idadi hiyo akisema hi kulinga na duru za hamas na kwamba hazina ukweli wowote.
Kanali Lerner amesema kuwa israel ilisitisha baadhi ya mashambulizi yake kwa hofu ya kuwauwa raia.
No comments:
Post a Comment