Friday 4 July 2014

Mbunge wa somalia auwawa

Wanamgambo wa Al Shabab wameahidi kungeza mashambulizi yake katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wanamgambo wa Al Shabab wameahidi kungeza mashambulizi yake katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Reuters / Feisal Omar

Mbunge mmoja wa Somalia ameuawa leo alhamisi mjini Mogadiscio na mwengine amejeruhiwa katika shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Al Shabab. Shambulio la mwisho lilitekelezwa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mbunge huyo anaejulikana kwa jina la Ahmed Mahmud Hayd, ambaye aliwahi kua waziri na afisa wa cheo cha juu katiaka jeshi la Somalia, ameuawa mapema asubuhi katika mtaa wa bandari, moja ya maeneo muhimu ya mji wa Mogadiscio ambako kuna idadi kubwa ya askari polisi, wamesema mashahidi.
Watu waliokua ndani ya gari ndogo waliwafyatua risase wabunge wote wawili walipokua wakitikea katiak hoteli moja mjini Mogadicsio.

Mpiganaji wa kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda
REUTERS
“walikua wanaelekea bungeni kushiriki kikao cha bunge wakati waliposhambuliwa, na kifo cha mmoja wa wabunge hao kimethibitishwa”, Abdi Bare yusuf, ambaye ni mbunge pia ameambia wanahabari.
Wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, limekiri kuhusika na shambulio hili.
“Mpango wa kumuua mbunge huyo tulikua nao, na tumemjeruhi mbunge mwengine na walinzi wao wawili” msemaji wa wa kundi la Al Shabab, Abdulaziz Abu Musab amelishibitishia shirika la habari la AFP.
“Tutaendelea kuwafukuza wabunge wengine iwapo hawataachana na taasisi hio iliyobuniwa na twala za kimagharibi, ameendelea kusema Abu Musab akiwalenga wabunge wa Somalia.
Kundi hili la Al Shabab limeahidi kungeza mashambulizi yake katika mwezi huu mtukufu kwa waislamu uliyoanza Jumapili, ambapo wanamgambo wa kundi hili waliendesha mashambulizi tofauti wakilenga wanajeshi, mashambulizi ambayo yalisababisha maafa.

Mazishi ya mbunge wa somalia Abdiaziz Isak Mursal, alieuawa kwa kupigwa risase, Apili 22 mwaka 2014.
REUTERS/Feisal Omar
Wabunge nchini Somalia wamekua wakiuawa mara kadhaa na mashambulizi hayo. Tarehe 22 mwezi aprili mbunge Abdiaziz Isak Mursal, aliuawa kwa kupigwa risase karibu na nyumba yake mjini Mogadiscio, na watu waliyosadikiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al Shabab.

Mwanajeshi wa kiosi cha wanajesi wa Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kwenye ngome yao kaskazini mwa mji wa Mogadiscio.
Reuters/Stuart Price
Wanamgambo wa kund la Al Shabab walitimuliwa mwezi Ogasti mwaka 2011 na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika Amisom ( kinacho kadiriwa kua na wanajeshi 22,000), na baadae kudhibiti ngome zao kusini na katikati mwa Somalia, lakini bado wanamgambo hao wanashikilia maeneo makubwa ya ya vijijini.
Kwa sasa wameamua kuanzisha mashambulizi ya kuvizia na kujilipua yakilenga mji mkuu wa Somalia, Mogadiscio na kudhoofisha taasisi za taifa hilo.

No comments: