UONGOZI mpya wa Simba
hautaki mchezo msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo
kiungo wa kimataifa wa Kenya, Paul Mungai Kiongera anatarajiwa kutua
nchini leo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo.
Kwa mujibu wa mmoja wa
wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, mchezaji huyo wa KCB ya Ligi Kuu
ya nchini humo, anakuja nchini kwa mazungumzo ya mwisho baada ya
mazungumzo ya awali kwa simu na kama yatakwenda vizuri, atasaini
Mkataba.
Pia kiungo Mrundi
Pierre Kwizera baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Simba anarejea
Ivory Coast kumalizana na klabu yake, Afad Abidjan ili aje kusaini
mkataba Simba.
Pia klabu hiyo inazidi
kujiimarisha zaidi ambao wapo kwenye mazungumzo na klabu za JKT Ruvu,
Ruvu Shooting na Coastal Union kwa ajili ya kuwanunua wachezaji Edward
Charles, Elias Maguri na Abdul Banda.
Kwa upande mwingine,
Simba SC itakutana na wachezaji wake ambao bado wana mikataba, lakini
haiwahitaji kwa sasa ili kujadiliana nao kuvunja mikataba yao.
Wachezaji hao ni kipa
Abuu Hashimu, beki Hassan Khatib, viungo Abulhalim Humud ‘Gaucho’,
Ramadhani Chombo ‘Redondo na washambuliaji Betram Mombeki na Christopher
Edward.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano ya kuachana na beki Mrundi, Kaze Gilbert anayetakiwa na klabu yake ya zamani, Vital’O.
No comments:
Post a Comment