Tuesday 8 July 2014

Watu 8 wajeruhiwa katika mlipuko Arusha

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali mahututi kufuatia mlipuko katika mkahawa mjini Arusha Tanzania
Mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na polisi wangali wanachunguza kilichousababisha.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na kuwajeruhi watu wanane huku mmoja akiwa hali mahututi.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Kufika sasa afisaa mkuu wa shirika la ujasusi nchini anakutana na wandishi wa habari.

No comments: