Wednesday 24 June 2015

Mwalimu ashiriki ngono na wanafunzi wake

Mwalimu mmoja mkuu amekiri kufanya ngono na wavulana wawili wenye umri mdogo.
Anne Lakey, mwenye umri wa miaka 55, kutoka eneo la Stanley, katika kaunti ya Durham, amekanusha makosa 13 dhidi yake ya kufanya matendo ya aibu kwa kushikashika sehemu za siri wavulana wawili miaka ya themanini.
Lakini jaji katika mahakama ya Teesside Crown, alimpata na hatia ya makosa hayo yote baada ya kesi iliyochukua majuma mawili.
Mahakama ilisikiza ushahidi wa namna alivyokuwa akitenda matendo hayo ya kuudhi na aibu katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Atahukumiwa jela Jumatano wiki hii.

Mahakama iliambiwa kuwa baadhi ya makosa yalifanyika pale Lakey alipokuwa mwalimu wa kufundisha somo la historia akiwa na umri wa miaka 20.
Lakey, ametajwa na waendesha mashtaka kama "mnyama wa ngono", alimlenga mvulana wa miaka 15 na waathiriwa wengine wawili wenye umri wa kati ya miaka 13 au 14.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, mmoja wa waathiriwa aliwaambia majaji kuwa mama huyo wa mtoto mmoja alimuondolea ubikra pale alipomtaka amtizame alipokuwa akioga.
Lakey alifanya kazi yake ya ualimu kwa ushindi mkubwa kwani alisifiwa mno kwa kufaulisha Shule hiyo iliyokuwa imedorora kielimu na kuifanya mojawepo ya shule iliyopata mafanikio makubwa.
Lakini mnamo mwaka 2012, mojawepo wa waathiriwa alituma ujumbe kwa njia ya barua pepe hadi shuleni humo, iliyosababishwa afutwe kazi na kisha polisi wakafahamishwa.

No comments: