Tuesday, 23 June 2015

Mwanamke mwingine ajitosa urais CCM

Kada wa CCM, Ritha Ngowi akikabidhiwa mkoba wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais na Katibu wa NEC (Oganaizesheni), Dk Mohamed Seif Khatib katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana. (Picha na Fadhili Akida).IDADI ya wagombea wanaochukua fomu kwa ajili ya kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana walifikia 39 baada ya mwanachama wake, Ritha Ngowi kuchukua fomu.
Ngowi, mkazi wa Dar es Salaam, anakuwa mwanamke wa tano kuchukua fomu, ambapo waliochukua fomu wa awali ni Balozi Amina Salum Ally, Waziri wa Katiba na Sheria Dk Asha-Rose Migiro, Dk Mwele Malecela na Monica Mbega.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema yeye ni msomi ambaye ana shahada ya Maendeleo ya Jamii na pia amepitia kozi mbalimbali katika ngazi za diploma na cheti. Alisema vipaumbele vyake vitakuwa ni kwenye sekta ya elimu na uchumi.
“Nimeguswa sana na kuamua kugombea nafasi ya Urais lengo langu kubwa ni kutaka kuboresha elimu na Uchumi” alisema.

Alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha kila Mtanzania anapata elimu ya msingi na asiwepo Mtanzania asiye na uwezo wa kupata kipato na atahakikisha Watanzania wanawezeshwa ili kuwe na uzalishaji.
Kwa upande wa uchumi alisema atamairisha vivuko kwa ajili ya kupunguza foleni, na wakulima watapatiwa pembejeo na mazao yao yatatafutiwa masoko.
Hata wafanyabiashara kazi zao katika mazingira mazuri na wafanyakazi wa serikali watapata mishahara mizuri itakayowezesha wananchi kuishi maisha yenye viwango. Alisema atarekebisha mishahara kuanzia ngazi ya chini.
“Unaweza kuona mtu anapokea mshahara wa Sh 350,000 hadi 450,000 anapanga nyumba na analipa ada, maslahi yao lazima yarekebishwe,” alisema.
Alipohojiwa kama ana sifa 13 za mgombea wa CCM anavyo alisema anazo sifa hizo zote ndio maana amejitokeza. Pia alipohojiwa atatanuaje tatizo la rushwa iwapo ataingia madarakani, alisema ili kuondoa tatizo la rushwa jambo la kwanza ni kudhibiti vyanzo hivyo.
Alisema kutakuwepo na mikakati ili fedha zote zinazokusanywa zifike kwenye vyanzo husika na huduma zifike mahali panapostahili.
Katika historia yake alisema amewahi kufanya kazi Shirika la Uchumi na Maendeleo ya Wanawake Tanzania (Suwata) pia aliwahi kufanya kazi Chama cha Wasioona Tanzania, pia mmiliki wa shule ya sekondari ya Jostihego iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Mawaziri 2 warudisha fomu Wakati huo huo, mawaziri wawili wanaowania kuteuliwa na CCM, kuwa wagombea wa nafasi ya Urais jana walirudisha fomu. Waliorudisha fomu ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Kilimo na Ushirika Steven Wassira.
Balozi Karume Mgombea mwingine, Balozi Ally Karume alirejesha fomu yake saa 10.35 jioni. Alichukua fomu hiyo Juni 4, mwaka huu na kwenda kutafuta wadhamini katika mikoa mbalimbali ya Bara na Visiwani, mwenyewe akisema amepata wadhamini wa

No comments: