Tuesday, 16 June 2015

SHule yahusishwa na imani ya kishirikina

Shule za kumbwa na imani za kimashetani nchini ZimbabweMwanafunzi amkata shingo mwenzake,mwalimu ahusika kuamini na kushiriki imani hizo

Wazazi wa wanafunzi wa shule za nchini Zimbabwe wameingiwa na wasiwasi mkubwa, baada ya kuzaakwa imani za kishetani katika shule hususani za mabweni.
Wiki chache zilizopita, shule inayopatika Mashonaland imewaacha raia wa Zimbabwe vinywa wazi kwa kusikia kuwa mwalimu wa shule hiyo anahusika na kuamini imani za mashetani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwalimu alishtakiwa kwa kosa la kuabudu mashetani na kupelekea wanafunzi kukubwa na “mapepo machafu”.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandishi wa habari, wanafunzi 480 wa shule ya Zinatsa wametolewa shuleni na wazazi wao kwa kuwa wameathiriwa  na imani hizo.
Na pia shule ya Chideme na shule zilizoko katika Harare, zimeripotiwa kuathiriwa na imani hizo siku chache baadae.
Mwaka jana pia kulikuwa na mashtaka ya aina hiyohiyo katika shule ya wasichana ya Nhowe ambapo mwanafunzi alimkata shingo mwanafunzi mwenzake kwa kuamini imani za mashetani.

No comments: