Waziri
mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa
huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa
kusini wa Sindh ikifikia 700.
Mamlaka ya kukabiliana na majanga
ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif
kuchukua hatua za dharura.Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.
Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.
No comments:
Post a Comment