Wednesday 17 June 2015

Mfanyibiashara tajiri zaidi barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote anapania kununua klabu ya Arsenal ya Uingereza.


Mfanyibiashara tajiri zaidi barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote amesema kuwa anapania kununua klabu ya Arsenal ya Uingereza.
Bilioneya huyo mmiliki wa kampuni ya kusafisha mafuta nchini Nigeria amesema fedha atakazopata kutoka kwa mauzo ya mijengo
na faida kutoka na uzalishaji wa mafuta zitamruhusu kununua klabu hiyo.
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 58 anasemekana ana mali yenye thamani ya pauni bilioni 11.5.
Dangote amekuwa shabiki sugu wa Arsenal tangu miaka ya 80.
"nikifaulu kuisimamisha kiwanda changu cha kusafisha mafuta bila shaka nitakuwa na fedha za kutosha kulipa pesa wanazouliza''alisema Dangote.
Bwenyenye mwenza kutoka Marekani Stan Kroenke anamiliki asilimia 66.64% ya kampuni inayomiliki klabu hiyo Arsenal Holdings plc.
Tajiri kutoka Urusi Alisher Usmanov anamiliki asilimia 29.11% huku hisa 62,217 zilizosalia zikimilikiwa na wachezaji wa zamani na mashabiki wa klabu hiyo.
nullArsenal ya Uingereza ndio mabingwa wa FA.
Dangote ameorodheshwa katika nafasi ya 67 katika orodha ya matajiri zaidi duniani ya Forbes.
Awali Dangote alikuwa amependekeza kununua asilimia 15.9% ya hisa zilizopewa Kroenke kwa pauni milioni £123 ambao awali zilikuwa zinamilikiwa na Bi Nina Bracewell-Smithin mnamo Aprili 2011 .
Dangote alijiondoa hata baada ya mazungumzo kuanza.
''Unajua kuwa tulikuwa wengi ambao tulikuwa tunataka kununua hisa hizo lakini wenzetu waliongeza bei maradufu hivyo tukawapisha''anasema Dangote.
Dangote anasema kuwa Arsenal inahitaji umiliki mpya ilikuchochea mabadiliko na matokeo uwanjani.
''Nafikiri hatunabudi kuleta mabadiliko afisini ilikutoa mwelekeo kwa safu ya ukufunzi''

No comments: