Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Leonidas Gama akimkaribisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini Bw. Alvaro Rodriguez alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo.
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez, alikutana na Mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na kufanya naye mazungumzo.
Miongoni mwa mambo waliyojadili ni maandalizi ya shughuli na matukio kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa (UN@70 ).
Katika mazungumzo yao walikubaliana
kufanya shughuli ya upandaji miti kuzunguka Mlima Kilimanjaro na
kusafisha sehemu ya mji kabla ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa mkoa alikubaliana na wazo hilo na kusema shughuli hiyo inafaa kufanyika katikati ya mwezi wa Agosti.
Wawili hao wakipiga picha ya pamoja.
Wakiagana.
No comments:
Post a Comment