Kufuatia taarifa kuzagaa mtaani
kwamba, afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro
kafutiwa kibarua chake kwenye klabu hiyo ya Jangwani, uongozi wa timu
hiyo umeamua kulitolea ufafanuzi jambo hilo ili kuondoa utata na maswali
mengi yanayoulizwa na mashabiki wa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania
bara kwa msimu uliopita.
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga
Dkt. Jonas Tiboroha amesema, hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo na
kuongeza kuwa Jerry Muro bado ni afisa habari wa Yanga na ni mfanyakazi
halali wa klabu hiyo na hakuna kikao kilichoitishwa kuchukua uamuzi huo.
“Hakuna ukweli juu ya jambo hilo,
Jerry bado ni afisa wa habari na mahusiano na ni mfanyakazi wa Yanga,
na hicho kikao si dhani kama kilifanyika maana mimi ndiye ninaeitisha
vikao na sijaitasha kiako cha hivyo”, amesema.
“Nimeshangaa hata mimi kwasababu
nimeona kwenye ‘groups za WhatsApp’ jana, nikasema hizi taarifa
zinapotoka wakati mwingine siyo yeye. Nimeshawahi kuongea wakati
mwingine unakuta taarifa zimeandikwa kwenye blogs, sasa sijui huyu mtu
aliyeandika yeye taarifa amezitoa wapi”, alifafanua.
“Mashabiki wa Yanga waelewe
kwamba, Jerry Muro bado ni mtumishi wa Yanga na bado ataendelea
kuwahabarisha habari za Yanga. Tunajaribu kuangalia na kuchunguza chanzo
cha hiyo habari ni nini”, Tiboroha alimaliza.
Awali, kulikuwepo na taarifa
zilizo zangaa kwenye mitandao ya kijamii (social networks) kwamba afisa
habari wa Yanga Jerry Muro ametimuliwa kunako klabu hiyolakini habari
hizo hazikwenda ndani zaidi na kusema sababu zilizopelekea Yanga
kumtimua Muro.
No comments:
Post a Comment