Thursday, 18 June 2015

Wapiganaji wanne wa Daesh wakamatwa Uturuki

Wapiganaji wanne wa Daesh wakamatwa UturukiWapiganaji wanne wa Daesh wakamatwa mpakani mwa Uturuki na Syria

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na jeshi la Uturuki ni kwamba, wapiganaji wanne wa wanamgambo wa Daesh walikamatwa mpakani mwa Syria na Uturuki walipokuwa wakijaribu kuvuka mpaka huo bila ruhusa.
Wapiganaji wa kwanza walikamatwa Juni 15 wakitokea Elbeyli nchini Syria.
Jeshi la Uturuki limefahamisha kuanzisha uchungu ili kutambua sababu zilizopelekea wapiganaji hao kutaka kuingia Uturuki.
Gazeti la The Times lilifahamisha kuwa kuna baadhi ya wapiganaji wa Daesh wanaojaribu kuingia Uturuki wakijifanya kana kwamba ni wakimbizi.
Post a Comment