Siku
moja baada ya ITV kutangaza kundi kubwa la wahamiaji haramu
wakijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
mfumo wa ELECTRONIC BVR wakishawishi watendaji wa serikali kwa kuwapatia
rushwa ya fedha na mifugo baadhi ya maafisa uandikishaji wilaya ya
Karagwe mkoani Kagera wameizuia kwa muda kamera ya ITV kupiga Picha
wahamiaji haramu wakitaka kuonyeshwa kibali kutoka tume ya taifa ya
uchaguzi kinachoruhusu mwaandishi wa habari kufanya kazi za uchunguzi.
Mgogoro huo umetokea kwenye kituo cha uandikisha cha bomani karibu
na ofisi ya mkuu wa wilaya,makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya
Karagwe na kituo cha polisi kayanga ambapo ITV ilibaini kuwepo kwa kundi
la wahamiaji haramu wakijiandikisha kinyume cha sheria na ilipofika
kwenye eneo la tukio na kupiga picha waliibuka maafisa uandikishaji
wakazuia eneo hilo kupigwa picha kati ya mwandishi na afisa uandikishaji
kituo cha bomani kufuatia sakata hilo ITV ikazungumza na mawakala wa
vyama vya kisiasa ambao wame bainisha jinsi maafisa uandikishaji wanavyo
ruhusu wahamiaji haramu kujiandikisha kwa njia ya rushwa kinyume cha
sheria za nchi.
Alipotakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili maafisa uandikishaji afisa
uchaguzi halmashauri ya wilaya ya karagwe Bi.Ashura Kajuna
ametofautiana maelezo na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
Karagwe mhandisi Richard Luyango juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili
watumishi wa serikali.
No comments:
Post a Comment