Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga amesema
yupo tayari kurudi (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua
ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa
Geita, Alphonce Mawazo.
Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama
viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake
kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.
"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za
kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo
hiyo" alindika Ally Banaga
Aidha Banaga ameonyesha masikitiko yake makubwa kwa watu
ambao wanakisaliti chama hicho na kusema kuwa wamesahau kuna watu kama kina
Mawazo ambao wamekufa wakikipigania chama hicho.
"Nilishika jeneza lako nikikuangalia mwamba umelala.
Ndipo nilipoamini kuwa sio stori, mwanaume wa kweli uliyefia vitani ukikitetea
chama ambacho kuna Mambwa Koko yanakisaliti, yanakichezea yanakinajisi bila
kuhisi maumivu yako ulipotoka roho kukipigania. Nilikuita kwangu Dar es Salaam
tupumzike baada ya uchaguzi mkuu ambao CCM walikupora kwa nguvu ushindi wako,
kaka ukakataa kwa neno moja " Nikiondoka Makanda watakufa moyo, ngoja
niwape tafu, Tukutane Dodoma.....dah! Tukakutania Mwanza kwenye jeneza"
alisema Banaga
Novemba 14, 2015 aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la
Busanda kupitia CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita aliuawa kwa
kupigwa mapanga na watu wasiojulikana na kupelekea kifo chake.
No comments:
Post a Comment