Rais wa Korea-Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uamuzi wa
Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel hauna maana
yeyote.
Mpango wa Marekani kuamisha ubalozi wake Tel Aviv na kuhamia
Jerusalem ni jambo la kukemewa.
Kim Jong Un anapinga uamuzi wa Trump kuhusu jiji la
Jerusalem.
Rais wa Korea-Kaskazini amesema kwa kejeli kuwa iwapo kuna
taifa linaitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jerusalem.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ufaransa cha AFP ni
kwamba msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea-Kaskazini amesema kuwa
Marekani inatishia amani na utulivu ulimwenguni .
Ujumbe wake ulimalizia kwa kusema kuwa Korea-Kaskazini ipo
bega kwa bega na wapalestina na waarabu wanaopigania haki yao
No comments:
Post a Comment