Tuesday 19 December 2017

Diwani wa Sombetini Kupitia Chadema amesema yuko tayari Kujiunga CCM kama waliomuua Mawazo watapatikana

Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga amesema yupo tayari kurudi (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.


Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.

"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo hiyo" alindika Ally Banaga

Wawili wakamatwa na kilo 64 za madawa ya Kulevya

Wakazi wawili wa Dar es Salaam wamekamatwa eneo la Kilambo mkoani Mtwara lililopo mpakani na nchi ya Msumbiji wakiwa na pakiti zenye uzito wa kilo 64 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga alisema watuhumiwa walikamatwa Desemba 7 wakiwa na dawa hizo zikitokea mkoani Pemba nchini Msumbiji kuingizwa Tanzania.

Sianga alisema pakiti hizo zilifichwa kwenye gari na kila moja ilifungwa kwa ujazo wa kilo moja.

Alisema watuhumiwa walipokamatwa walipelekwa kwa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya ukaguzi wa kina.

Monday 18 December 2017

ROSE MHANDO AJIUNGA RASMI CCM

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho unaofanyika Mjini Dodoma.

Nasary Afunguka baada ya TAKUKURU kutupilia mbali Ushahidi wake


Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh.Joshua Nassari leo ameandika kupitia Moja ya ukurasa wake wa Mitandao ya kijamii maneno haya baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi alioutoa kwa madiwani walionunuliwa na Kujiunga ccm

Mahakama kuu ya mwachia Huru Sheikh Issa Ponda

Mahakama Kuu imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru. Alishtakiwa kwa kesi ya kutoa maneno ya uchochezi.

Friday 15 December 2017

WASHTAKIWA WA MAPENZI YA JINSIA MOJA WAACHIWA HURU MWANZA

Washtakiwa wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.


Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma leo Desemba 15, baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi, Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka ni dhaifu mbele ya macho ya sheria.
Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote kuwa wanawake.

Thursday 14 December 2017

ASKARI AMPIGA RISASI ASIKARI MWENZIE KWA WIVU WA MAPENZI

Akizungumza na waandishi wa habari mtu wa karibu na askari hao amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa askari hao ni wivu wa mapenzi ambapo marehemu pamoja na mtuhumiwa ambaye ametambulika kwa jina la Faustine Masanja wameona nyumba moja.

Amedai marehemu alipofika asubuhi kazini ndipo mtuhumiwa Masanja alimpiga mwenzake risasi ya kichwa na alipokimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru alifariki dunia.

ALIYEKUWA MBUNGE WA SIHA KUPITIA CHADEMA AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM






Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ajiuzulu nafasi hiyo pamoja na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Disemba 14, 2017.

Wednesday 13 December 2017

RAIS WA KOREA KASKAZINI AMJIA JUU TRUMP KUHUSU JERUSALEMU

Rais wa Korea-Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uamuzi wa Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel hauna maana yeyote.
Mpango wa Marekani kuamisha ubalozi wake Tel Aviv na kuhamia Jerusalem ni jambo la kukemewa.
Kim Jong Un anapinga uamuzi wa Trump kuhusu jiji la Jerusalem.
Rais wa Korea-Kaskazini amesema kwa kejeli kuwa iwapo kuna taifa linaitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jerusalem.

FAMILIA YA BEN SAANANE YA ANDIKA HAYA KUKUMBUKA SIKU YA KUZALIWA KWA BEN SAANANE

Ni mwaka mmoja na siku kadhaa tangia Ben Saanane atoweke/atoweshwe katika mazingira tatanishi.
Leo Ben, anamitiza miaka kadhaa tangia kuzaliwa kwake. Happy beloved birthday bro, hero and comrade!

Naelewa namna Baba, Mama, dada, kaka na ndugu zako wanavyo jisikia, ulikuwa kaka mkubwa, lango la familia, tegemeo, ulikuwa sehemu ya furaha ya familia, Leo walio kulea wanaumia, walitamani siku ya leo mshereheke siku hii pamoja, ila imekuwa tofauti, siku imekuwa ya mawazo na mateso kuliko tegemeo.
Masonokeno na Maumivu yao tumeyaishi, machozi katika mioyo yao hayakuwahi kauka, furaha yao imekuwa ya msimu, kila wakijaribu kupata furaha, kukosenaka kwako kunaondosha

Tuesday 12 December 2017

Babu wa Loliondo aoteshwa tena, Atabiri ummati Kurudi kupata huduma ya Kikombe

Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu Babu wa Loliondo akitoa huduma ya kikombe kwa wagonjwa
NGORONGORO . Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu Babu wa Loliondo aliyehudumia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kwa dawa aliyoitoa kwa kipimo cha kikombe amedai ameoteshwa kuwa umati utarudi kijijini Samunge kupata dawa.
Amesema ana uhakika wa jambo hilo kwa kuwa hata mwaka 2011 kabla ya maelfu ya watu kufika nyumbani kwake alioteshwa, hivyo amejiandaa kuweka miundombinu bora zaidi na hasa ujenzi wa vibanda atakavyovitumia kutoa huduma.
Mchungaji Mwasapile alisema hayo jana Jumapili Desemba 10,2017 mbele ya ujumbe wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda aliyekuwa mkoani Arusha kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Miongoni mwa waliofika kupata ‘kikombe’ kwa gharama ya Sh500 mwaka 2011 walikuwemo wafanyabiashara maarufu, wanasiasa na viongozi waandamizi serikalini.
Akizungumzia dawa yake anayodai inatibu maradhi mengi amesema kwa sasa anaitoa kwa watu wachache wanaofika kijijini hapo.

Monday 11 December 2017

HATUA YA 16 BORA UEFA , CHELSEA USO KWA USO NA BARCELONA HUKU REAL MADRID NA PSG

Kikosi cha Klabu ya chelsea 
Chelsea wamepangwa kukutana na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa.
Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United wakutana na Sevilla wanaocheza La Liga nao Liverpool wakutane na FC Porto ya Ureno.

MIILI YA WANAJESHI WA TANZANIA WALIOUAWA kONGO KUWASILI LEO NCHINI

Wanajeshi wa Kulinda amani Nchini Kongo wakitoa heshima za Mwisho kwa wanajeshi waliopoteza maisha katika shambbulio lililofanywa na waasi nchini humo

Dar es Salaam. Miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini leo.

Taarifa ya ofisi ya habari ya JWTZ imesema miili ya askari hao itawasili nchini leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa kumi na mbili jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Mwenyekiti na Katibu wa ACT wazalendo Singida ajiunga CCM


SINGIDA: Mwenyekiti wa ACT wazalendo, Wilfred Kitundu na Katibu wake Loth Thomas wamejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM.Wadai kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli

Friday 24 November 2017

EMMERSON MNANGAGWA AAPISHWA KUWA RAIS WA ZIMBABWE... JIONEE LIVE ANAVYOAPISHWA

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kutawazwa leo Ijumaa, siku tatu baada ya mtangulizi wake Robert Mugabe kuachia ngazi kwa shinikizo la jeshi na chama chake cha Zanu-PF.

Aliyekua makamu wa rais anamrithi Mugabe, baada ya uhasama kati yake na mkewe Mugabe, Grace Mugabe, kutokea na kusababisha kufutwa kazi na kukimbilia nchini Afrika Kusini.

Grace Mugabe alitaka kumrithi mumewe, baada ya kukalia kiti cha makamu wa rais wa Zimbabwe.

Bw. Emmerson alirejea siku ya Jumatano jioni, siku moja tu baada ya mtangulizi wake kujiuzulu.


Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .

Upinzani unamtaka Emmerson Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi".

Vyombo vya habari vya serikali vimesema kuwa Robert Mugabe atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bw. Munangagwa.

Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare, huku waandalizi wakiwataka wa Zimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.


UNAWEZA KUANGALIA HAPA NAMNA SWALA KA KUAPISHWA KWA RAIS WA ZIMBABWE LINAVYOENDELEA
👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Wednesday 22 November 2017

MSANII MATATANI KWA KUTOA VIDEO AKILA NDIZI KWA MADAHA


Msanii wa kike wa muziki wa Pop nchini Misri ajulikanaye kwa jina la, Shyma amejikuta mikononi mwa polisi Jumamosi ya wikiendi iliyopita baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la ‘ I have Issues’ kwa kosa la kuonekana akila tunda aina ya ndizi kwenye video hiyo kwa mbwembwe mbele ya wanaume.

ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS ZIMBABWE KUAPISHWA RASMI KAMA RAIS WA TAIFA HILO

  ​


Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Taifa la Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa huenda akaapishwa rasmi leo au kesho kuwa Rais mpya wa nchi hiyo. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Sheria wa Chama cha ANU-PF.

Bwana Mnangagwa ataliongoza taifa hilo hadi wakati wa uchaguzi mkuu mwakani. Mugabe aliwamua kujiuzulu ikiwa ni dakika chache kabla ya Bunge la nchi hiyo alijaanza mchakato wa kumuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Tuesday 21 November 2017

NASA ya Kenya Kumwapisha Odinga kama Rais wa kenya Jumanne

Wakati Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Kenya Jumanne ya wiki ijayo, Umoja wa Vyama vya Upinzani (NASA) nchini humo pia umetangaza kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa

CCM YAMREJESHA KUNDINI SOPHIA SIMBA UPYA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.

Friday 17 November 2017

KENYA: ASKOFU ASLIMU NA KUGEUZA KANISA KUWA MSIKITI


Habari zilizotufikia kutoka Kenya, Askofu Charles Okwany ambaye baada ya kuichagua dini ya Kiislamu kuwa mwongozo wake wa wokovu duniani na Akhera amechagua jina la Ismail Okwany.

Amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Amesema baada ya kusilimu, kanisa alilokuwa akihurbiri, lililoko katika eneo la Nyalgosi kaunti ya Homa Bay magharibi mwak Kenya, ambalo lilijulikana kwa jina la God’s Call Church of East Africa sasa limegeuzwa jina na kuwa Msikiti wa Jamia wa Nyalgosi.

Wananchi Mikoa Yote Kupimwa UKIMWI

MIKOA yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi.


Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha Siku ya Ukimwi duniani Desemba Mosi. Kaulimbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo jana.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam. Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na ushauri nasaha.
Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili Ukimwi na huduma ya kupima kwa hiari.


Chanzo-Habarileo

Wednesday 15 November 2017

ALiyekuwa makamu wa Rais Zimbabwe Atangazwa Kuwa rais wa Chama cha ZANU-PF



ZIMBABWE: Aliyekuwa Makamu wa Rais, Emerson Mnangagwa atangazwa kuwa Rais mpya wa Chama cha ZANU-PF
> Mapema leo atua Uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Manyame

Jeshi la Zimbabwe la kanusha kufanya mapinduzi

Jeshi la Zimbabwe limekanusha madai kwamba mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kuiondoa serekali, na kudai kwamba rais Robert Mugabe na familia yake wapo salama.Katika taarifa iliyotolewa na jeshi kupitia televisheni ya taifa, imeelezwa kwamba jeshi linalenga wahalifu wanaosababisha shida za kijamii na kiuchumi na kuwafikisha mbele ya sheria.

Thursday 9 November 2017

Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya imedhibitika ni Fake: Wema sepetu ahusika

PICHA: Dogo Janja akionekana anatia saini kwenye cheti cha ndoa
Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja yabainika kuwa reel na sio real, Uwoya ampora Wema dili la million 400 toka kituo kikubwa cha TV barani Afrika !
Nyuma ya sarakasi ya kile kinachosemekana ni ndoa kati ya staa wa wa filamu nchini Irene Pancras Uwoya na dogo wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kuna mengi, Amani limeibuka na jipya.
Ubuyu wa motomoto uliolifikia gazeti la Amani mapema wiki hii, ulidokeza kuwa, hapana shaka kuwa kilichokuwa kikiendelea kati ya Uwoya na Dogo Janja si ndoa bali ni tamthiliya inayotarajia kuanza kurushwa na kituo kikubwa cha runinga barani Afrika.

Monday 6 November 2017

HESLB yatoa majina ya mikopo awamu ya tatu 2017/2018


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578.

Friday 20 October 2017

RASMI : MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017/18 YATANGAZWA, SOMA HAPA

Baraza la Mitihani taifa ( NECTA) limetangaza matokeo ya darasa la saba leo tarehe 20/10/2017
kupata matokeo hayo  BOFYA HAPA 👇👇👇👇
                                   MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017/18

Thursday 12 October 2017

MCHEZAJI WA ZAMANI WA CHELSEA NA AC MILAN GEORGE WEAH ASHINDA URAIS LIBERIA




Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea akitokea Ac Milani George Weah amefanikiwa kushinda nafasi  ya urais iliyoachwa wazi na aliyekuwa rais Mstaafu Eileen nchini Liberia kwa kuwabwanga washindani wenzake 19 waliokuwa wakiwania kiti hicho cha urais.

Wednesday 27 September 2017

Zanzibar na Uingereza ndio nchi pekee zilizopogana vita kwa muda Mfupi , dakika 40

Unaambiwa ukishangaa ya Musa utaona ya firauni, na siku hizi watu wanasema akili za mtu anazijua mwenyewe. Ili kudhibitisha hayo najaribu kukuletea simulizi hizi za kweli zilizotokea nyakati tofauti tofauti katika uso wa dunia. Siku zote migogoro huwa inatokea katika maisha ya binadamu na kunakuwa na sababu za kimasilahi kusababisha migogoro hio, wakati mwingine kumekua na migogoro ambayo mantiki za kimasilahi hazionekani, nakusababisha watu au pande mbili kwenda mbali Zaidi kiasi cha kutanagaza vita. Zifutazo ni vita vilivyo wahi kutokea kayika historia ya dunia na kuonekana za ajabu sana kulingana na sababu, muda au mbinu zilizotimika.

Wednesday 6 September 2017

Manji avuliwa udiwani baada ya kushindwa kuhudhuria vikao

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amevuliwa nafasi ya udiwani wa kata ya Mbagala Kuu baada ya kushindwa kuhudhuria vikao kutokana na kukabiliwa na kesi Mahakama ya Kisutu.

Watoto wawili kati ya wanne waliokuwa wametekwa wapatikana wakiwa wamekufa

Wananchi wakishuhudia zoezi la uopoaji wa miili ya watoto wawili

ARUSHA: ​ Watoto wawili  Ikram na Maureen waliokuwa wametekwa wamepatikana katika shimo la choo ambalo bado halijaanza kutumika. Muda huu askari ndio wanafanya utaratibu wa kuwatoa.

Chanzo cha uhakika kinasema mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita kabla ya kukamatwa na kusema walipo watoto hao.

Mwanafunzi awekewa sh. bilioni 2.2 na bodi ya mikopo kimakosa

Eastern Cape, Afrika Kusini. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu alilala masikini na kuamka tajiri baada ya kukuta akaunti yake ikiwa na Dola 1 milioni za Marekani sawa na Sh2.2 bilioni kutoka katika bodi ya mikopo ya wanafunzi.

Alijiona mwenye bahati na kuanza kuzitumbua, asijue kumbe alikuwa akichochea kugundulika haraka kwa kuwa ndani ya wiki mbili kitumbua chake kiliingia mchanga.

Viongozi wanne wa CUF wanaomuunga mkono prof .LIPUMBA wamefariki kwenye ajali wakitokea Dodoma

Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho.

Thursday 31 August 2017

Je Mahrez atajiunga na timu gani ? soma hapa

Riyad Mahrez ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya kikosi cha Algeria na kurudi Ulaya ili kukamilisha uhamisho wake hadi klabu mpya kulingana na shirikisho la soka nchini Algeria.
Winga huyo wa Leicester aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika uwanja wa King Power na amehusishwa na vilabu vingi huku Roma ikiwa tayari imewasilisha ombi la kumununua mchezaji huyo mara tatu , ombi la mwisho likiwa lile la dau la £32m.

Monday 14 August 2017

Waziri Mkuu aagiza wananchi wasizuiwe kuonyesha mabango

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka mabango yanayoonyeshwa na wananchi kwa viongozi wa kitaifa wanapowatembelea yasiwe yanazuiwa kwa vile yanakuwa yanaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Majaliwa alisema hayo baada ya kuona mabango yaliyoinuliwa na wananchi kwenye mkutano wake na wananchi mwishoni mwa juma lililopita mjini Sikonge mkoani Tabora huku wananchi hao wakitakiwa kuyashusha.
“Siku nyingine msirudie na kuanzia sasa waacheni wananchi waonyeshe mabango yao kwani ndiyo njia wanayotumia kuonyesha hisia zao kwa yale wanayokumbana nayo na kuwasababishia kero,” alisema Majaliwa.

Friday 21 July 2017

Mawakili Kigali walaani kukamatwa Rais wa wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu

Baadhi ya Mawakili jijini Kigali wamekosoa kitendo cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam cha kumkamata rais wa chama cha wanasheria Tundu Lissu ambaye alikuwa njiani kuelekea jijini humo kuhudhuria mkutano.
Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.
”Huu ni mpango wa kumdhoofisha, kwanini asingekamatwa jana?” amehoji wakili wa kujitegemea Rwebangiza Kiondo kutoka Tanzania, ambaye yupo jijini humo kwa shughuli za kufuatilia uchaguzi wa Rwanda.
Wakili Rwebangiza ameiambia BBC, kuwa Polisi wanatumia nguvu nyingi kupambana na Mwanasheria huyo ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake.
”Unamkamata Wakili akiwa katika pilika za kutekeleza wajibu wake, tena kwa kumshtukiza utafikiri ni jambazi anayetafuta, sikatai kwamba huenda pana hoja lakini kwanini umshtukize, mtu ambaye ni mbunge?”

magazeti ya leo tarehe 21.7.2017


Monday 17 July 2017

TETESI ZA USAJILI LEO TAREHE 17/7/2017

Kulingana na gazeti la Sky Sports Klabu ya chelsea inataka kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang , katika harakati hizo chelsea imeongeza dau lake kutoka paundi milion 65 hadi kufikia paundi ilion 70 kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo baada ya kumkosa Romeu Lukaku aliyetua Man U .

Thursday 13 July 2017

Ajira mpya 10,184 kuziba waliachishwa kazi kwa vyeti feki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Ilimnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam jana.
“Mgawanyo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki.

Wednesday 12 July 2017

Tetesi za usajili leo tarehe 12.7.2017



Klabu ya Chelsea iliyo na maskani yake jiji la London imetuma ofa ya paund million 65 kwaajili ya kumsajili mshmbuliaji wa Borusia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gaboni.
Meneja wa Chelsea Antoni Conte ametuma ofa hiyo baada ya kukosa saini ya aliyekuwa mchezaji wa Everton Romeo Lukaku ambaye sasa amejiunga na mahasimu wao Manchester United jumatatu ya wiki hii. Mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo uekuja baada ya Chelsea chini ya meneja wake Conte kuonekana hana mpango na Diego Costa kwa msimu ujao ,Kwa Upande wa Dortmund wamefungua milango kwa mchezaji huyo kuuzwa , ripoti kutoka gazeti la “The Sun ” zineleza kuwa Pierre-Emerick Aubameyang anatamani sana kucheza ligi ya Uingereza. Aubemeyang aliibuka mpachikaji bora wa magoli katika ligi ya ujerumani msimu wa 2016/17, PSG na AC MILLAN pia zinafuatilia saini ya mchezaji huo kwa karibu zaidi

Tuesday 11 July 2017

MCHUNGAJI :Ni rahisi kufanya ngono na walokole kuliko wasio walokole



MCHUNGAJI WA KANISA LA KIPENTEKOSTE AMESEMA KUWA NI RAHISI KUFANYA NGONO NA WASICHANA WANAOKWENDA KANISANI KULIKO AMBAO HAWAENDI KANISANI.


Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste huko Afrika Kusini amesema kuwa ni rahisi sana kwa mhubiri kufanya ngono na wasichana wanaokwenda kanisani kuliko ambao hawaendi kanisani.
Mchungaji Benard Pumalaka amesema hayo Jumatano iliyopita baada ya kuokoka.
Amesema kuwa wengi wanaojiita "manabii" ni maarufu kwa ngono na wasichana na wake za watu.
Bernard alisema "kabla sijawa mchungaji wa Pentekoste, nilikuwa nimelala na watu wawili tu-mke wangu, na mwanamke mwingine mmoja tu.
Lakini nilipopata uchungaji nimelala na wanawake zaidi ya 200 ktk miaka kumi! Na nimepata utajiri mkubwa kwa kuwadanganya waumini wangu.
Nimejipatia fedha nyingi,magari na nyumba kwa kuwahadaa waumini wangu.Hakika sikuwa na Yesu ndani mwangu."

Monday 10 July 2017

Ngeleja arejesha hela alizopewa na Rugemalira

Mbunge wa Sengerema na waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kushoto) akionesha nakala ya risiti aliyokabishiwa na mamlaka ya Mapato nchini (TRA) baada ye kurejesha serikalini kiasi cha Sh40.4 milioni alizopewa kama msaada toka kwa mfanyabiashara James Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing Ltd. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.

Thursday 6 July 2017

JAY-Z athibitisha mamake mzazi ni mpenzi wa jinsia moja

JAY-Z na mkewe BeyonceMsanii wa muziki wa Rap JAY-Z ameonekana kuthibitisha kuwa mamake ni mpenzi wa jinsia moja
Kulingana na maneno ya wimbo wa albamu yake 4:44, msanii huyo alisema:Mama alikuwa na watoto wanne lakini ni mpenzi wa jinsia moja licha ya kujifanya kuwa muigizaji.
Haijalishi kwangu iwapo ni mume ama mke nataka kukuona ukifurahi baada ya chuki zote.
Mapema katika kipindi chake chote cha kazi ya muziki JAY-Z aliandika nyimbo zilizokuwa na maneno ya watu wa mapenzi ya jinsia moja lakini akawacha kurekodi nyimbo zenye maneno hayo
Maneno hayo ya muziki yapo katika wimbo unaoitwa Smile ambao pia unashirikisha picha ya mamake Gloria Carter akisoma shairi.

Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette

Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette toka timu ya Lyon kwa dau la pauni Milioni 52.6 na kuvunja rekodi ya usajili ya timu hiyo.
Usajili wa kiungo wa Kijerumani Mesut Ozil ndio ulikua usajili wa bei ghali zaidi klabuni hapo aliposajiliwa mwaka 2013, kutokea Real Madrid kwa dau la pauni 42.4.
Lacazette amesaini mkataba wa miaka mitano kuwatumika washika mitutu hao wa London, mshambuliaji huyu atasafiri na timu wikiendi hii kuelekea Sydney kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki.
Msimu uliopita, Lacazette alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ufaransa alikozipasia nyavu mara 28 na ameshapiga jumla ya mabao 129 katika mechi 275 tangu alipoanza kuichezea timu ya kwanza msimu wa 2009/10.

Sunday 4 June 2017

NAMBA YA SIMU YA BEN SAANANE YATUMIKA WHATSAPP

Wakati hofu ikiwa imetenda baada ya jumla ya miezi minane kupita tangu alipopotea kwenye mazingira ya kutatanisha, matumaini mapya yameanza kuibuka baada ya simu yake kuonekana imetumika kwenye mitandao ya kijamii.
Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitoweka mwaka jana na kumekuwapo na hisia nyingi kuwa huenda alishafariki dunia kutokana na kuwa, hakuna yeyote anayefahamu alipo kijana huyo aliyekuwa akichipukia katika siasa nchini Tanzania. 
Kwa mujibu wa gazeti la TanzaniaDaima, simu ya Ben jana alitumika majira ya saa tatu asubuhi ambapo ilionekana namba yake ikijitoa kwenye makundi ya WhatsApp. Imeelezwa kuwa namba yake ilijitoa kwenye makundi mengi huku ikiwaacha na mshangao mkubwa wajumbe (members) wa makundi hayo. Hofu ya kuwa kijana huyo hayupo hai ilichangiwa na jibu alilolitoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa bungeni ambapo alisema, “familia ya mtajwa (Ben Saanane) aliyetangulia mbele za haki au vinginevyo, uchunguzi wa suala lake utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa.” Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe Aprili 20 mwaka huu aliyetaka kujua kwanini serikali imekuwa kimya sana kwenye suala la kupotea kwa msaidizi wake.

Sunday 28 May 2017

Tetesi za Usajili Uingereza leo



Mshambuliaji wa Atletical Madrid aliyehusishwa kwa mda mrefu kuhamia Klabu ya Manchester United Antoine Griezman amewakatisha tamaa mashabiki wa man u baada ya kuandika katika akaunti yake ya twitter kuwa bado anafurahia kubaki A.Madrid na taarifa zinazomhusisha na kutaka kuhama ni za uongo zipuuzwe.

Mshambuliaji wa Chelsea na nchezaji wa timu ya taifa ya Ghana Christin Atsu aliyekwa akikipiga kwa Mkopo katika club ya Newcastle inayofundishwa na kocha wa zaman wa Mabingwa wa Uingereza kwa sasa Chelsea Rafael Benitez amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja utakaombakisha katika kla
bu hiyo kwa ada ya uhamisho wa £6 million.

Manchester city wamewapiku jirani zao Manchester United kwa kumfanikisha kupata saini ya mchezaji wa Monaco Bernardo Silva kwa kiwango cha £43million . Huku klabu ya napoli ikifanikiwa kumbakiza mchezaji wake mahiri Dries Mertens ambaye mkataba wake ulikuwa unakaribia kufika kikomo , Dries Mertens ameingia mkataba mpya na klabu yake hadi 2022.
Mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund Aubameyang ameweka wazi kuwa anatamani kubadili mazingira na anatamani kufana kazi na klabu nyingine tofauti na Borussia Dortmund hata hivyo timu za ligi kuu nchini uingereza kama vile Chelsea zinamvizia mshambuliaji huyo hatari , chelsea chini ya meneja wake Conte inamwinda kinda huyo ili kuziba nafasi ya Diego Costa anaetimkia China msimu ujao na kuungana na wachezaji wenzake wa zaman kama Oscar , Ramirez na Dembaba.
Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa imeingia kwenye vita kali na klub ya newcastal katika kuwania saini   ya mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anamtolea macho mchezaji wa kimataifa wa Ujermani na klabu ya Borussia Dortmund Mario Gotze ili kuziba pengo la mshambuliaji wake Philippe Coutinho
anaetazamiwa kujiunga na miamba wa soka nchini Uhispania Barcelona.

Katika hali ya sintofahamu wamiliki wa Arsenal juzi walikuwa wamemwahidi kocha wa Arsenal arsen wenger kuwa atapatiwa mkataba wa miaka miwili endapo watapata matokeo mazuri dhidi ya chelsea katika fainali ya kombe la FA , hata hivyo Wenger haku chezea bahati hiyo alifanikiwa kutwaa kombe la FA kwa kuwachapa Chelsea 2-1 , hivyo inatazamiwa wenger akaongezewa mkataba wa miaka miwili

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKANUSHA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI LILILOSAMBAA MITANDAONI.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na Tangazo la nafasi za kazi linalosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo ''Facebook na WhatsApp'' likionyesha kwamba Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa tangazo la kazi lenye jumla ya nafasi wazi 188 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Watu hao mwenye nia ovu kwa makusudi wameamua kusambaza taarifa za uongo zenye kichwa cha Habari Tangazo la Nafasi za Kazi likiwataka watanzania wenye sifa na uwezo kutuma maombi ya kazi kwenye portal ya ajira kwa ajili ya kujaza nafasi hizo huku wakijua kuwa tangazo hilo sio la kweli kwa kuwa Serikali haijatangaza nafasi hizo hali ambayo imeleta usumbufu kwa jamii na wadau mbalimbali.

Saturday 27 May 2017

Njiwa ashikwa na mfuko wa 'uliojaa madawa ya kulevya'

Maafisa wa forodha nchini Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba madawa ya kulevya katika mkoba mdogo mgongoni, gazeti la Kuwait, la al-Rai limeripoti.
Jumla ya tembe 178 ziliipatikana katika mfukop huo uliokuwa umepachikwa mgongoni mwake, gazezi hilo lilisema.
Ndege huyo alinaswa karibu na jumba la forodha jijini Abdali, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
Mwanahabari wa Al-Rai alisema kuwa madawa hayo ya kulevya yalikuwa aina ya ketamine, nusukaputi ambayo pia hutumiwa kama dawa haramu katika sherehe.
Abdullah Fahmi aliiambia BBC kwamba maafisa wa forodha walijua mbeleni kuwa njiwa walitumiwa kusafirisha madawa ya kulevya, lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kunasa njiwa katika harakati hizo.

Thursday 18 May 2017

Kikwete ateuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza la wakimbizi duniani

Aliyekuwa rais wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, taarifa kwa vyombo vya habari ilimtaja Bwana Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Canada Lloyd Axworthy.

Wednesday 17 May 2017

Malima afikishwa kortini kwa kumshambulia askari

Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa
mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi. Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi. Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alitenda kosa.