Monday, 18 December 2017

Nasary Afunguka baada ya TAKUKURU kutupilia mbali Ushahidi wake


Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh.Joshua Nassari leo ameandika kupitia Moja ya ukurasa wake wa Mitandao ya kijamii maneno haya baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi alioutoa kwa madiwani walionunuliwa na Kujiunga ccm


Anaandika Mbunge wa Jimbo Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.

Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi. 
Post a Comment