Jeshi la kutuliza Ghasia wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanyisha waandamanaji |
Mabomu ya rindima Arusha tena baada ya wananfunzni wa chuo
cha ualimu Patandi kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha maeneo ya Tangeru, ili
kuishinikisa serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kumwondoa au kumfuta
kazi Mkuu wao wa chuo,
Mwandishi wetu aliyekuwepo katika eneo la tukio alimtafuta
rais ya seriikali ya wanafunzi wa chuo hicho na kumhoji “Alisema chanzo cha
Mgomo huo ni tabia ya mkuu wa chuo kuwakandamiza na kuwanyima uhuru wao wa
kufanya mambo , aliongeza kwa kusema Mkuu wetu wa chuo huwa anatushinikiza
kuchapisha na kutoa kopi za “notes’kwa ajili ya kusoma katika stationary yake
angali zipo stationary nyingi chuoni pia amekuwa akiwalazimisha wanachuo kula
katika mgahawa wake (Cafeteria) huku ikitoa huduma kwa gharama ya hali ya juu, hivyo
kufanya wanafunzi hao kushindwa kuhimili hali ya maisha katika chuo hicho
Askari wakitunza usalama |
Pia mkuu wa chuo hicho aliwazidishia hasira wanachuo hao kwa
kupiga makofi mwanafunzi hii nai baada
ya mwanafunzi huyo kuchukua kibali toka kwa mkufunzi wa zamu ili akasuke nywele
zake ndipo alikutana na mkuu wa chuo na kumdai kibali na kukichana , haikutosha
aliitisha wita mwanafunzi huyo ofisin na kumpiga kipara nywele zake , wanafunzi
wenzake walipona kuwa mkuu wao kamdhalilisha
huku akijua kuwa mwanafunzi huyo ni
mjamzito , Kitu ambacho serikali ya wanafunzi wa chuo iliona ni unyanyasaji wa
hali ya juu ndipo walipoona wafunge
barabara kwa kuchoshwa na tabia za Mkuu wao wa chuo .
No comments:
Post a Comment