Maelfu
ya watu nchini Nepal wamelala nje usiku kufuatia tetemeko kubwa la
ardhi lililoikumba nchi hiyo jana Jumamosi ambalo lilisababisha
uharibifu mkubwa na kupotea kwa maisha.
Wakazi wa mji wa kathmandu walisema kuwa hawangerudi manyumbani mwao kutokana na hofu ya kutokea kwa mitetemeko zaidi.Serikali ya Nepal inasema inaamini kuwa takriban watu 1500 wameaga dunia lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati makundi ya uokoaji yanapotafuta kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Hali mbaya ya hewa inalikumba eneo hilo na watoa huduma za dharura wanasema kuwa huenda ikavuruga jitihada za uokoaji.
No comments:
Post a Comment