Thierry
Henry ameikosoa sera ya usajili ya Arsenal ya hivi karibuni na ameitaka
klabu yake hiyo ya zamani kununua wachezaji wa wanne wa kiwango cha juu
majira ya kiangazi mwaka huu.
Mfaransa
huyo anaamini kuwa Arsenal inahitaji golikipa, beki wa kati, kiungo
mkabaji na mshambuliaji kama wanataka kushinda kombe la ligi kuu
England.
Akizungumza
baada ya suluhu ya jana ya Arsenal dhidi ya Chelsea, Henry,
amemshambulia Olivier Giroud akidai kuwa The Gunners wataendelea
kuhangaika kutafuta ubingwa kama Mfaransa huyo mwenzake ataendelea kuwa
mshambuliaji chaguo la kwanza.
“Nadhani
wanahitaji kununua wachezaji wanne-bado wanahitaji golikipa, kiungo
mkabaji na nina wasiwasi wanahitaji wachezaji wa juu, wanahitaji
mshambuliaji wa kiwango cha juu kama wanahitaji kuchukua ubingwa tena”.
“Tuna
mfano mzuri wa Chelsea. Walikuwa wanahangaika kushinda kombe msimu
uliopita. Waliingia sokoni walimnunua [Thibaut] Cortouis, [Nemanja]
Matic, Cesc [Fabregas] na [Diego] Costa, sasa mambo ni mazuri”.
No comments:
Post a Comment