Friday 26 June 2015

Magonywa ya ngono yaongezeka kwa wapenzi wa jinsia moja

Wapenzi wa jinsia moja
Maradhi ya zinaa yanayosambazwa miongoni mwa wapenzi wanaume wa jinsia moja inatamausha.
Haya ni kwa mjibu wa shirika la afya ya umma nchini Uingereza.
Takwimu za mwaka 2014 zinanonesha kuwa asilimia 46 ni maambukizi ya kaswende, ilihali asilimia 32 ni maambukizi ya kisonono, huku maambukizi ya maradhi ya "chlamydia" ikiwa kwa asilimia 26.
Ripoti hiyo inasema kuwa kumekuwa na viwango vya juu vya visa ya kufanya ngono bila ya kutumia mipira ya kondomu, hali iliyozidisha kusambaa zaidi kwa maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa wanaume hao.

Sasa idara hiyo ya afya ya umma inapendekeza upimaji wa mara kwa mara wa maradhi ya zinaa.
Kote nchini Uingereza kwa ujumla, idadi ya maambukizi ya maradhi ya zinaa imepungua kwa asilimia 0 nukta 3 tofauti na mwaka uliotangulia na kufanya idadi ya walioambukizwa maradhi hayo hadi 439,243 ya visa vipya.
Kuna tofauti ya sura ya wanaume waliofanya ngono na wanaume wenzao:Mambukizi ya ugonjwa wa kaswende yalipanda kutoka 2,375 hadi 3,477. Kisonono kiliongezeka kutoka watu 13,629 hadi 18,029 Waliopatikana na maradhi ya "chlamydia" waliongezeka kutoka 9,118 hadi 11,468 Ugonjwa wa viungo vya uzazi nao uliongezeka kwa asilimia 10 kutoka watu 3,156 hadi 3,456.
Idara ya afya ya umma nchini Uingereza inaongeza kuwa watu wote walio na nguvu ya kufanya ngono walio chini ya umri wa miaka 25 wanafaa kupimwa mara kwa mara kila mwaka hasa wanapowabadilisha wapenzi wa ngono.

No comments: