Mhe. Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo cha mbunge wa Geita Mhe Donald Max.
Spika
wa bunge Mhe.Anna Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo
cha mbunge wa jimbo la Geita kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mhe Donald Kelvin Max kilichotokea katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili juni 23 mwaka huu.
Akiahirisha kikao cha bunge Mhe.Makinda amesema marehemu amekuwa
akiugua kwa muda mrefu hali iliyopelekea kulazwa hospitalini kwa kipindi
kirefu ambapo amesema taratibu za mazishi zinafanywa na anatarajiwa
kuzikwa jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi ya Jun 27.

Aidha wakizungumzia kifo cha marehemu Donald mMx, baadhi ya wabunge
wamesema marehemu alikuwa ni mcheshi na mwenye kuelewana na wenzake kwa
kipindi alichowahi kuhudhuria vikao vya bunge.
No comments:
Post a Comment