Watafiti
wa magonjwa wanasema kwamba janga kubwa la ugonjwa wa ebola nchini
Guinea linazidi kuongeza idadi ya vifo vya watu wanaofariki dunia kwa
maradhi ya malaria .
Utafiti huo,uliochapishwa katika jarida moja
la magonjwa ya kuambukiza nchini humo,linakadiria kwamba watu wapatao
elfu sabini na watano wanaougua ugonjwa wa malaria hawakupatiwa dawa,
pengine kutokana na kufungwa kwa vituo vya afya,ama pengine wagonjwa
walikuwa wana hofu kubwa ya kutafuta msaada wa kitabibu.Watafiti hao wanasema magonjwa yote mawili,malaria na ebola husababisha ho
ma na hofu pia inaweza kuchangia mgonjwa kutomwona daktari.
Watafiti hao wameendelea kueleza kwamba,idadi ya wagonjwa wa malaria nchini Guinea imeshuka katika baadhi ya maeneo kwa asilia sabini .
No comments:
Post a Comment