Friday, 19 June 2015

Tetesi za usajili ulaya leo


Mshambuliaji kutoka Argentina anayechezea Manchester City Sergio Aguero amesema ametulia City licha ya Real Madrid kuonesha dalili za kumtaka. Aguero, 27, anataka kuchukua Klabu Bingwa Ulaya na City (Daily Mirror) Paris St-Germain watapambana na Manchester City katika kumwania kiungo wa Juventus Paul Pogba, 22. PSG wapo tayari kutoa pauni milioni 70 wanazotaka Juve (Daily Star), winga wa Manchester United Nani, 28, aliyecheza kwa mkopo Sporting Lisbon msimu uliopita, atahamia Fenerbahce ya Uturuki kwa uhamisho wa pauni milioni 6 na mkataba wa miaka minne (Sun), Petr Cech, 33, amefikia makubaliano ya kujiunga na Arsenal kutoka Chelsea baada ya kuhakikishiwa kuwa atakuwa kipa namba moja (Daily Mirror), kuwasili kwa Cech kutasababisha David Ospina, 26, kuhamia Fenerbahce kwa pauni milioni 4 (Times), 

Crystal Palace wameambiwa lazima walipe kiasi kisichopungua pauni milioni 15 kumsajili Loic Remy, 28, kutoka Chelsea (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Chelsea Patrick Bamford, 21, aliyecheza kwa mkopo Middlesbrough msimu uliopita, ataanza mazoezi na Chelsea baada ya kukataa kuhamia Newcastle United (Times), Tottenham wanafikiria kumchukua kipa wa Genoa, Mattia Perin, 22 (Sun), Southampton hawatomuuza Nathaniel Clyne, 24, kwenda Liverpool chini ya pauni milioni 15. Tayari wamekataa dau la pauni milioni 10 (Daily Telegraph), beki wa Liverpool Martin Skirtel, 30, amekubali mkataba wa miaka mitatu na kumaliza wasiwasi wa kuondoka katika klabu hiyo (Times), Liverpool wamekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Charlton, Joe Gomez, 18 ambaye anatafanya vipimo vya afya siku ya Ijumaa (Daily Mail), Chelsea wanamtaka kiungo wa Zenith St Petersburg, Axel Witsel, 26, kuziba nafasi ya John Obi Mikel, 28, ambaye anakaribia kuondoka Stamford Bridge (Daily Express), meneja wa Inter Milan, Roberto Mancini anamtaka beki wa kulia wa Chelsea Filipe Luis, na Chelsea wamesema wapo tayari kusikia dau lao (Gazzetta dello Sport), Arsenal, Liverpool na Southampton wanatajwa kumwania Sven Bender wa Borussia Dortmund (Bild), Inter Milan imetoa euro milioni 18 kumtaka Gannielli Imbula, ingawa Marseille wanataka euro milioni 20 (RMC), Liverpool wamewaambia Manchester City kuwa hawatoweza kumpata Raheem Sterling kwa pauni milioni 40 msimu huu (Daily Mirror)
Post a Comment