Wanachi hao pamoja na kumpogeza mbunge wao kusimamia kupinga
michango ambayo siyo ya lazima na wao sasa wamekuwa huru kwa kutokamatwa
ovyo na vyombo vya dola,wamesema barabara hiyo ambayo imetengenezwa kwa
kiwango cha chini ukilinganishwa na fedha zilizo tolewa,kutokana na
ubovu wa barabara hiyo wamekuwa wakipatashida kufuata huduma za afya na
zingine makao makuu ya wilaya ya Ikungi.
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha
Ngogosoro mbunge wa jimbo la Singida mashariki mheshimiwa Tundu Lisu
amesema pamoja na kufuatilia swala la barabara kuhakikisha fedha zilizo
tolewa zinatumika ipasavyo, kukwama kwa miradi ya maendeleo katika
jimbo la singida mashariki ni kwa sababu ya madiwani wengi wa ccm
kushindwa kuishindikiza halamashauri ya wilaya ya ikungi kutekeleza
miradi ya maendeleo kama jinsi ilivyo pangwa.
Katika hatua nyingine Mhesimiwa Tundu Lisu amewataka wananchi
kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura,kwa
kufanya hivyo itakuwa ndio njia pekee ya kuwatoa madarakani viongozi
ambao hawatekelezi majukumu yao kwa ufanisi na wanaodidimiza maendeleo
kwa kumbatia vitendo vya rushwa.
No comments:
Post a Comment