Wednesday, 24 June 2015

Ebola yaibuka mjini Freetown

Bango lenye elimu kwa umma Sierra Leone
Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili wapya wanaougua ugonjwa wa ebola na kwamba wamegunduliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.
Hapo awali ilidhaniwa kwamba mji huo ulikuwa hauna maambukizi ya ugonjwa huo,na hakukuwa na wagonjwa walioripotiwa hapo kabla kwa muda wa wiki kadhaa.
Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwasababu vituo vyote vya karantini na vitendea kazi vyake vilikuwa vimefungwa mjini Freetown.
Na akaongeza kusema kwamba kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.

Nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.

No comments: