Mwenyekiti wa taifa wa chama ch wananchi CUF Profesa Haruna Lipumba
amechukua fomu ya kugombea urais kupitia chama cha wananchi CUF huku
akitaja vipaumbele vyake kuwa atahakisha rushwa katika utawala wake
inakoma sambamba na kuhakisha kuwa tatizo la ajira na ukosefu wa lishe
kwa watoto linapatiwa ufumbuzi wa kudumu ambapo amesisitiza kuwa
umasikini walio nayo watanzania ni matokeo ya rushwa kukithiri
inayotokana utawala mbovu wa chama cha mapinduzi.
Akihutumbia umati wa wanachahama wake walioojitokeza kumsindikiza huku wengine wakiifuatilia hotuba hiyo moja kwa moja
kupitia ITV Profesa Lipumba amesema inashangaza kuona kuwa
watunambo ni mafisdi wakubwa badala ya kuwa magerezani wapo majukwaani
wanasaka uongozi.
Aidha akasema kuwa umefika wakati wananchi kufanya maamuzi juu ya
hatima yao na kutambua kuwa CCM kamwe haiwezi kuwaletea maendeleo kama
kwa kipindi chote hicho ilishindwa.
Awali katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamaad amesema
kuwa kwa sasa nchi inahitajika kiongozi ambaye ana uwezo mkubwa wa mambo
na ambaye atalifikisha taifa katika ngazi zingine na siyo mwingine bali
ni Profesa Lipumba.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa CUF Mh Juma Haji Duni amesema
kwa kipindi kirefu chama cha CUF kimekuwa kikijitahidi kuihakisha kuwa
mabadilko ya kweli yanapatikana ila wananchi wanaonekana bado
wanashindwa kuzitambua jitihada hizo na sasa umefika wakati kuiweka
pembeni CCM.
No comments:
Post a Comment