Sunday, 11 May 2014

China imeahidi kushirikiana na Kenya ili kuifanya biashara kati yao ikue kwa uwiano zaidi.


Waziri Li Keqiang asema China itachukua hatua za kuhimiza uwiano kati yake na KenyaAhadi hiyo imetolewa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alipokutana na rais Uhuru Kenyatta leo asubuhi jijini Nairobi.
Li amesema ingawa biashara inaamuliwa kutokana na mahitaji na utoaji sokoni, hata hivyo, China itajitahidi kuhimiza uwiano katika biashara kati yake na Kenya.
Katik mkutano huo waziri mkuu Li alitaja hatua mbalimbali zitakazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa urahisi kwa Kenya kutangaza bidhaa zake nchini China, na kuhamasisha kampuni mbalimbali za China kuwekeza zaidi katika sekta ya utengenezaji nchini Kenya, pamoja na kushirki kwenye uanzishwaji wa maeneo ya viwanda, na kuimarisha uwezo wa utengenezaji wa Kenya ili bidhaa za Kenya ziwe na nguvu zaidi ya ushindani katika soko la kimataifa.
Mwaka 2013 thamani ya biashara kati ya Kenya na China ilifikia dola bilioni 3.27 za kimarekani. China imekuwa nchi ya pili duniani inayofanya biashara zaidi na Kenya.

No comments: