Hali inatisha katika mji mkuu wa jamhuri ya Afrika Kati-Bangui ambako
vizuwizi vimewekwa majiani na mapigano kuripotiwa kati ya vijana na
vikosi vya polisi huku maelfu wakiandamana kudai serikali ya mpito
ijiuzulu.
Mizinga kadhaa imefyetuliwa katika eneo la kati la mji mkuu wa jamhuri
ya Afrika Kati -Bangui,karibu na kasri la rais katika wakati ambapo
makundi ya waandamanaji waliongozana majiani.Kwa mujibu wa shirika la
habari la Ufaransa AFP,hali ilitulia kidogo saa moja baadae baada ya
waandamanaji kulihama eneo hilo.Katika mitaa mengine na hasa karibu na uwanja wa ndege,mikururo ya watu wanaandamana wakidai serikali ya mpito ijiuzulu,wanajeshi wa kigeni waihame nchi hiyo na hasa wale wa kutoka Burundi wanaotuhumiwa kuwachia matumizi ya nguvu dhidi ya waumini wa dini ya kikristo.Watu wawili wanasemekana wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya kulinda amani vya kutoka nchi za Afrika Misca mjini Bangui.
Mji mkuu Bangui umejiinamia
Vifo na Majeruhi kufuatia mapigano mjini Bangui
Vikosi vya jeshi na polisi vimefyetua risasi hewani kuwatawanya
waandamanaji.Vizuwizi vimewekwa majiani katika mitaa kadhaa ya mji
mkuu.Hakuna magari yanayozunguka na,maduka yamefungwa.Mji mkuu mkuu huo
umejiinamia helikopta ya kijeshi ya Ufaransa tu ndio inayopiga
doria.Vikosi vya Ufaransa Sangaris na vile vya Misca vya kutoka nchi za
Afrika vimeonya "vitapambana kikamilifu na aina yoyote ya
mapendeleo".Vikosi hivyo vimetoa wito waa utulivu mjini Banguii.Matumizi ya nguvu yamepamba moto tangu siku kadhaa sasa katika mji mkuu huo wa jamhuri ya Afrika Kati.Vizuwizi kadhaa viliwekwa katika njia muhimu na mapigano kuzuka kati ya vijana na vikosi vya nchi za Afrika kufuatia shambulio la kanisani lililoangamiza maisha ya watu wasiopungua 15.
Waziri mkuu André Nzapayéké anasema kuzidi nguvu machafuko "ni njama iliyoandaliwa" na "wanasiasa walio karibu na serikali."
"Kuna baadhi ya wanasiasa wanaoingia majiani wakidai serikali ijiuzulu,watu walio karibu na serikali,na karibu na rais wa mpito na baraza la mawaziri"Anasema waziri mkuu huyo.
Miito ya walimwengu dhidi ya matumizi ya nguvu
Rais wa mpito Sanba -Panza na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-Moon wakihudhuria mkutano wa kilele Kati ya Umoja wa ulaya na
Afrika,mapema mwezi uliopita wa April
Umoja wa Ulaya unasema umeingiwa na wasi wasi wasi kutokana na
hali namna ilivyo na kuwataka viongozi waendeleze bila ya kuchoka juhudi
za kuleta suluhu ya taifa.Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki-Moon amelaani vikali mashambulio yanayoendelea ikiwa ni pamoja na lile dhidi ya kanisa kuu la Fatima mjini Bangui.
No comments:
Post a Comment