Monday, 26 May 2014

Maiti yatumwa kwa njia ya posta China


Mwanamke huyo aliandika kwenye Facebook kuwa alikuwa anaenda kumtembelea rafiki yake kabla ya kuuawa
Polisi nchini Japan wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo maiti ya mwanamke aliyeuawa ilitumwa kutoka Osaka hadi Tokyo kwa njia ya posta.
Inaaminika mwanamke huyo, Rika Okada, alidungwa kisu na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku ambayo ilitiwa kibandiko na karatasi iliyosema kuwa sanduku hiyo ilikuwa imemeba mwanasesere.
Sanduku hiyo, iligunduliwa ikiwa katika sehemu ya kuhifadhi vitu katika kituo cha posta.
Polisi wanasema kuwa sehemu ambako sanduku hiyo ilipatikana imewekwa, ilikuwa imekodishwa kwa kutumia kadi ya benki ya mwanamke huyo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alitoweka tangu mwishoni mwa mwezi Machi, alipotuma ujumbe wa mwisho kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa anaenda kukutana na rafiki yake wa muda mrefu ambaye alikuwa hajamuona kwa miaka mingi.

No comments: