Thursday, 29 May 2014

Abdel Fattah El Sissi anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais Misri.

Mkuu wa zamani wa jeshi Misri Abdel Fattah El Sissi anaongoza katika kura za rais wa Misri.Mkuu wa zamani wa jeshi Misri Abdel Fattah El Sissi anaongoza katika kura za rais wa Misri.


Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais huko Misri yanaonyesha mkuu wa zamani wa jeshi Abdel Fattah El Sissi anaelekea kupata ushindi mkubwa.

Matokeo ya kwanza yamempa Sissi kiasi cha asilimia 93 ya kura wakati mgombea mwingine mwenye mrengo wa kushoto Hamdeen Sabahi ana kiasi cha asilimia 3.

Waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache kiasi cha asilimia 44 hata baada ya wapiga kura kupewa siku moja ya ziada kuweza kupiga kura.Matokeo kamili yanatarajiwa wiki ijayo.

Chama cha Muslim, Brotherhood kiliwasihi  watu wagomee uchaguzi.Kinamshutumu Sissi na washirika wake kwa wizi wa kura na ujanja. Wameita urais wa Sissi ni muendelezo wa jeshi kuchukua madaraka huko Misri ambayo yalianza  mwaka jana wakati jeshi lilipomtoa madarakani  Mohamed Morsi.

No comments: