Watu 43 wameuawa baada ya bomu
kulipuka katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa
Uturuki. Mlipuko huo uliosababishwa na mtu kujilipua garini umetokea
karibu na eneo la mpakani la Bab al Salameh pambizoni mwa mji wa Aleppo.
Makumi ya watu pia wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Katika upande mwingine waasi wa Syria
wanaoungwa mkono na nchi za kigeni wameshambulia na kuharibu kaburi la
shahaba Uwais al Qarani katika mji wa Raqqa. Mtukufu Uwais bin Qarani
alikuwa mfuasi mtiifu wa Imam wa kwanza wa Mashia, Imam Ali bin Abi
Twalib (A.S). Makundi ya kitakfiri yenye itikadi za kufurutu ada,
yameshambulia na kuharibu maeneo mengi ya kihistoria na Kiislamu nchini
Syria katika miaka mitatu iliyopita kutokana na itikadi zao potofu
No comments:
Post a Comment